Dr ulimboka akijitoa kuongoza jumuiya ya madaktari itakuwaje?

Chal

Senior Member
Oct 7, 2010
128
52
Dr Ulimboka si mwajiriwa wa serikali ni kweli, yeye ni mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari.

Kuhusika kwa dr ulimboka katika mgomo wa madaktari kunasababishwa na ukweli kuwa madai ya madaktari si katika nyongeza ya mshahara na maslahi yao tu. Hulo ni dai moja kati ya mengi ikiwamo kuboreshwa kwa huduma katika sekta ya afya.

Huenda haya madai mengine yakawa ni sababu tosha kwa Dr Ulimboka kuhusika katika kuinfluence mgomo lakini akaaminiwa na kupewa uongozi katika suala hilo.

Suala la Dr Ulimboka kutokuwa mwajiriwa wa serikali limeonekana kupewa uzito katika mjadala unaohusisha mgomo wa madaktari. Sasa hapa nahoji iwapo atajitoa kuongoza jumuiya ya madaktari je,itakuwaje?mgomo utaisha?madai mengine yatatekelezwa?

Si afiki kuwepo kwa mgomo kwani watanzania wasio na hatia ambao walipaswa kupatiwa huduma za afya katika nchi yao wanaumia na kupoteza maisha lakini pia serikali haina budi kulitazama suala hili kwa jicho la tatu ili kuweza kulipatia ufumbuzi na madaktari warudi kazini.
Nawasilisha...

 
Back
Top Bottom