Dr Tulia Ackson Miaka yote aikuwa wapi?

Dr Tulia Ackson Miaka yote aikuwa wapi?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,430
Reaction score
271,918
Wakuu natanguliza salamu ,

Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya , Wilaya ya Kyela , kijiji cha Kajunjumele ,utamaduni wa Kyela na Rungwe unashabihiiana kwa kiasi kikubwa sana , wakazi wengi wa Wilaya hii ni Wanyakyusa , japo kuna makabila mengine.

Tunazo ngoma za asili ambazo kwa uchache ni Mang'oma , Ipenenga , Samba nk , na tumecheza ngoma hizi kwa miaka mingi bila msaada wa hela ama chochote kutoka kwa yeyote , kama kuna aliyetoa chochote basi alitoa kama vile PDG Ndama Mutoto wa ng'ombe anavyowapa wanamuziki wa FM ACADEMIA .

Sasa cha kushangaza mwaka huu amezuka mfadhili wa ngoma za asili aitwaye Tulia Ackson , Huyu tetesi zinadokeza kwamba lengo lake si kufadhili ngoma za asili , maana alikuwepo miaka yote na alikuwa na uwezo kama huu wa leo , lakini hakufanya hivi , taarifa zinaonyesha kwamba amelenga kurubuni wakazi wa Rungwe ili achaguliwe mbunge uchaguzi ujao .

Mbinu hii ya kizamani haikubaliki , na naomba kuchukua nafasi hii kuwaasa wana Rungwe kumuogopa huyu mama kama ukoma .

Dr Tulia aliyeingia bungeni na kubebwa kwa mbeleko ya chuma hadi kwenye unaibu spika , amekuwa mstari wa mbele kudhalilisha na kunyanyasa wabunge wa upinzani , amezima mijadala mingi yenye tija ili kuokoa chama chake , huyu hawezi kuwa msaada wa Akina Mama wauza ndizi na maziwa wa ushirika au Kiwira , hafai hata kuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Makandana , hafai .

Dr Ngunangwa aliwahi kuwauliza waliokuwa wanajipitisha kwenye jimbo lake huko Njombe na kutoa zawadi za baiskeli nk , kwamba WALIKWINA ? yaani kwa kiswahili , MIAKA YOTE WALIKUWA WAPI ?

Nakala ya uzi huu imfikie JOHN MWAMBIGIJA .
 
Haya mambo yalikuwepo toka siku nyingi tena mashindano hasa. Nakumbuka tulikuwa wadogo tunayaona haya.Naona wewe akili zako zote umejaa siasa kuna watu wanaona mbali zaidi ya siasa, vile vile kufufua ngoma za asili ambazo siku nyingi zilishaanza kusahaulika anatakiwa kupongezwa badala ya kushutumiwa. Badilikeni jamani.
 
Kwani kuna ubaya akichaguliwa mkuu? Mwache tu, kila mtu ana mbinu yake ya kupata kick jimboni kwake, kama ameona ndo njia itakayomvusha haina shida, waamuzi mtakuwa nyie wananchi wa kyela kuona kma anawafaa au lah....cha kufanya hpo ni kumtafutia pinzani anayeuzika zaidi yake na aliye na rekodi ya maendeleo zaidi yake..
 
Haya mambo yalikuwepo toka siku nyingi tena mashindano hasa .Nakumbuka tulikuwa wadogo tunayaona haya.Naona wewe akili zako zote umejaa siasa kuna watu wanaona mbali zaidi ya siasa , vile vile kufufua ngoma za asili ambazo siku nyingi zilishaanza kusahaulika anatakiwa kupongezwa badala ya kushutumiwa .Badilikeni jamani.

Umeongea vyema sana, Tulia anastahili pongezi sana kwa hili.

Kwa mji mdogo kama Tukuyu, mashindano haya yanaongeza fursa kwa wafanyabiashara wa Tukuyu na Rungwe kwa ujumla ikiwepo kuongeza kwa kiasi kikubwa mzunguko wa fedha.
 
Hongera zake kwa kukumbuka ASILI yake , apewe ushirikiano
 
Umeongea vyema sana, Tulia anastahili pongezi sana kwa hili.

Kwa mji mdogo kama Tukuyu, mashindano haya yanaongeza fursa kwa wafanyabiashara wa Tukuyu na Rungwe kwa ujumla ikiwepo kuongeza kwa kiasi kikubwa mzunguko wa fedha.
Haya mashindano kwa ni ya kusini tu. Namshauri Ayafanye ya nchi nzima na yahamishiwe Dar-Es-Salaam!
 
Ngoma nyingi huko kwa wanyaki zimehusishwa na mambo ya uganga na mambo ya kishirikina. Kwa hiyo huyu msomi Acks amechagua kutegemea misukule? Nilipata kusikia ni mcha Mungu sana!
 
Umeongea vyema sana, Tulia anastahili pongezi sana kwa hili.

Kwa mji mdogo kama Tukuyu, mashindano haya yanaongeza fursa kwa wafanyabiashara wa Tukuyu na Rungwe kwa ujumla ikiwepo kuongeza kwa kiasi kikubwa mzunguko wa fedha.
Amelenga kweli kusaidia ?
 
Dr. Tulia Alikua bonge la lecturer, nakumbuka ndiye aliotuweka sawa kwenye first year orientation ya UDSL maana tulikua very exhausted, I Will always remember her for that, na namwomba akimaliza siasa arudi nyumbani UDSL.
 
Haya mambo yalikuwepo toka siku nyingi tena mashindano hasa .Nakumbuka tulikuwa wadogo tunayaona haya.Naona wewe akili zako zote umejaa siasa kuna watu wanaona mbali zaidi ya siasa , vile vile kufufua ngoma za asili ambazo siku nyingi zilishaanza kusahaulika anatakiwa kupongezwa badala ya kushutumiwa .Badilikeni jamani.
Nani alikudanganya kwamba ngoma za asili ziliwahi kufa Mbeya ? Kama hujui kitu kaa kimya bhana , halafu hujiulizi Why Now ?
 
Wakuu natanguliza salamu ,

Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya , Wilaya ya Kyela , kijiji cha Kajunjumele ,utamaduni wa Kyela na Rungwe unashabihiiana kwa kiasi kikubwa sana , wakazi wengi wa Wilaya hii ni Wanyakyusa , japo kuna makabila mengine.

Tunazo ngoma za asili ambazo kwa uchache ni Mang'oma , Ipenenga , Samba nk , na tumecheza ngoma hizi kwa miaka mingi bila msaada wa hela ama chochote kutoka kwa yeyote , kama kuna aliyetoa chochote basi alitoa kama vile PDG Ndama Mutoto wa ng'ombe anavyowapa wanamuziki wa FM ACADEMIA .

Sasa cha kushangaza mwaka huu amezuka mfadhili wa ngoma za asili aitwaye Tulia Ackson , Huyu tetesi zinadokeza kwamba lengo lake si kufadhili ngoma za asili , maana alikuwepo miaka yote na alikuwa na uwezo kama huu wa leo , lakini hakufanya hivi , taarifa zinaonyesha kwamba amelenga kurubuni wakazi wa Rungwe ili achaguliwe mbunge uchaguzi ujao .

Mbinu hii ya kizamani haikubaliki , na naomba kuchukua nafasi hii kuwaasa wana Rungwe kumuogopa huyu mama kama ukoma .

Dr Tulia aliyeingia bungeni na kubebwa kwa mbeleko ya chuma hadi kwenye unaibu spika , amekuwa mstari wa mbele kudhalilisha na kunyanyasa wabunge wa upinzani , amezima mijadala mingi yenye tija ili kuokoa chama chake , huyu hawezi kuwa msaada wa Akina Mama wauza ndizi na maziwa wa ushirika au Kiwira , hafai hata kuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Makandana , hafai .

Dr Ngunangwa aliwahi kuwauliza waliokuwa wanajipitisha kwenye jimbo lake huko Njombe na kutoa zawadi za baiskeli nk , kwamba WALIKWINA ? yaani kwa kiswahili , MIAKA YOTE WALIKUWA WAPI ?

Nakala ya uzi huu imfikie JOHN MWAMBIGIJA .
Hivi Afrika tuna nia kweli ya Kulinda tamaduni zetu na Lugha zetu. Mimi ningependekeza, ukiwa sema mzaramo au kabila lolote lakini unaishi mkoa sio origin yako ni vizuri tukafundishwa ngoma za mkoa huo ktk level ya primary school, ukifika shule ya upili ndio uanze kucheza na nje ya TZ.
 
Mbona Mr Sugu aliingia kwa gia ya kuendeleza Hiphop Mbeya na hatukusikia yote hayo,na kuna wengine wamekuwa maarufu kwa kutukana viongozi,mwache Tulia atulie na amang'oma yake.Hata asipoleta hiyo mipalaano Tu;ia atakuwa mbunge tu .Mambo ya watu wa CCm waachie wenyewe kama vile mambo ya Chadema mlivyoachiwa wenyewe kikolo.
 
Ngoma nyingi huko kwa wanyaki zimehusishwa na mambo ya uganga na mambo ya kishirikina. Kwa hiyo huyu msomi Acks amechagua kutegemea misukule? Nilipata kusikia ni mcha Mungu sana!
Acha urongo weye ngoma za Kinyaki ni pure utamaduni hayo mambo unayoyasema labda yapo kwenu huko mabonde kuinama
 
Back
Top Bottom