Dr Tulia Ackson anawatesa Sana mashabiki wa CHADEMA

Dr Tulia Ackson anawatesa Sana mashabiki wa CHADEMA

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
17,031
Reaction score
23,695
Tokea ndugu Tulia Ackson atangaze mwaka Huu kutaka Jimbo la Mbeya mashabiki wa CHADEMA wamekuwa wakimuandama na nyuzi zake zimekuwa nyingi Sana humu jamvini zikianzishwa na wanachadema.

Hii Hali imenishangaza kidogo kwani Tulia Ackson akigombea mbeya ukiwa wewe si mwana mbeya unapungukiwa Nini? kwani Jimbo la mbeya Lina hati miliki mbunge lazima awe ni sugu?

Hizi ndio siasa za maji taka binafsi Sina mapenzi na chama chochote Cha siasa hii imenifanya nisiwe msukule wa mtu au chama.

Kingine zaidi kilichoniacha hoi ni wapenzi wa chadema kuponda msaada aliyotoa kwa wazee hivi karibuni me nilitegemea labda waliopewa msaada ndo watoa povu lakini wanaotoa povu ni watu ambao sio wanambeya.

Me navyojuaja tulia ameanza kutoa msaada muda mrefu Wala sio kwenye kipindi hiki Cha uchaguzi nakumbuka alimpa ubalozi mwaka juzi Emanuel okwi kipindi yupo Simba wa foundation yake kusimamia zoezi la kutoa msaada wa vitanda kwa wamama wajauzito.

Cha msingi watanzania tuache chuki na siasa za maji taka chuki hazijengi yaani unamchukia mtu ambaye hata ujawahi kuonana nae zaidi ya kumuona kwenye Tv na social network unajikuta unapata stress ambazo hazikuhusu wakati stress za maisha yako tu umeshindwa kuimili.

NB: suala la uchaguzi wa Jimbo la mbeya mjini tuwaachie wanambeya wenyewe ndo wanaofahamu yupi ni mbunge wao sahihi kumchagua Kati ya Sugu au Dr Tulia Ackson.
 
Back
Top Bottom