Kwanza pole na majukumu.
Ukiwa kama kiongozi na Mtendaji Mkuu wa chama,sijafurahishwa hata kidogo na namna viongozi wako wa chini hasa ngazi za wilaya wanavyoendesha shughuli za chama ikiwa ni pamoja na hatua na maamuzi wanayoyafanya katika kipindi hiki kilichobaki kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015
Nimelazimika kukuandikia katika jukwa hili kufuatiwa maamuzi yaliyofanywa na viongozi wako wa kamati tendaji ya wilaya ya morogoro mjini ya kuwafukuza wanachama na viongozi wapato 20 pasipo kuzingatia katiba,kanuni na taratibu za chama chako.
Kati ya hao waliofukuzwa uanachama hakuna hata mmoja aliyewahi kuitwa mbele ya kikao na kusomewa tuhuma zinazomkabili.Naomba utume timu yako kuchunguza ukweli kila panapotokea matatizo ya namna hiyo ili kukijenga na kukiimarisha chama badala ya njia hii ya sasa inayotumika na kuigwa na viongozi wako wakidhani ndio staili ya kusafisha chama
Kwa bahati mbaya sana natumia simu ya mkononi lakini kesho nitabandika hapa moja ya nakala za barua walizopewa hao waliofukuzwa ikionyesha mapungufu kadhaa ikiwemo
1. Mtu mmoja kupewa adhabu mbili tofauti kwa mfano wapo ambao barua zao zinaonyesha wamefukuzwa katika chama katika aya ya kwanza lakini aya ya pili wamepewa onyo kali na kuambiwa wasirudie kosa kwani wakirudia watafukuzwa uanachama.
2.Hakuna mwanachama hata mmoja kati ya hao waliofukuzwa ambaye aliitwa kwenye kikao,kujulishwa tuhuma na kupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea,huko ni kukiuka misingi ya haki ya asili,katiba ya chama unachokiongoza na kanuni za chama.
3.Chama chako kwa morogoro mjini kinakabiliwa sana na tatizo la uongozi.Viongozi waliopo sasa hasa katibu na mwenyekiti wake wote walikuwa cuf na walifukuzwa huko kutokana na aina ya siasa waliokuwa wakiiendesha,siasa za majungu na kuwagawa wanachama,maamuzi yao ukifanya uchunguzi utagundua yanasukumwa zaidi na hisia binafsi badala ya kanuni na taratibu za chama
4.Chadema ni chama kikuu cha upinzani kwa sasa,kinahitaji kujenga misingi imara katika ngazi za chini kwa kuwajengea uwezo watendaji wake hasa kwa ngazi za msingi,kinahitaji kuwa na viongozi wasomi,wenye vipaji na weredi katika kuendesha shughuli za chama lakini kwa upande wa morogoro mjini hali si shwari.viongozi waliopo ni wale waliochaguliwa kipindi kileee ambapo chama kilichukua kila mtu ili kuziba mapengo
5.Ukifanya uchunguzi kwa umakini utagundua kuwa chama chako kinahujumiwa na viongozi wako mwenyewe kwa mfano,chanzo cha migogoro morogoro mjini ni kamati tendaji ambayo hutumia muda mwingi ofisini kwa kupiga soga,viongozi hawataki kukosolewa,hawataki kukubali changamoto,mbinu wanazotumia kuendesha chama ni za kizamani nk.
6.Kwa wanaofuatilia siasa za morogoro mjini watagundua kuwa kuna gape kubwa kati ya vijana na wazee,sababu ya kuwepo kwa gape hilo ni utofauti wa nguvu,kasi na mawazo kati ya chadema ya zamani na sasa.
7.Viongozi wa wilaya morogoro mjini mara kadhaa wamekuwa wakizuia harakati za chama kwa sababu za kipuuzi,hata pale wanapojitokeza watu wa kujitolea kuhamasisha chama wao wamekuwa mstari wa mbele kukwamisha mpaka kuwe na mazingira flani ya wao kunufaika.
8.Kwa kiongozi makini kama wewe huwez kukwepa kuhoji kwanini tangu uongoz wa wilaya uingie madarakani 2009 mpaka leo wameshindwa kuwa na ofisi yao morogoro mjini,wameshindwa kuanzisha na kuweka uongozi katika kata zote za manispaa,kusimamia uanzishwaji wa mabaraza ya chama nk
9.Hivi juzi tulisikia tetesi na baadae kuthibitishwa na vyombo vya habari kuwa chama morogoro mjini kimefukuza 15 na 5 kupewa onyo.kati ya waliofukuzwa yumo pia mbunge kivuri wa chadema morogoro mjini Mheshimiwa Amani Mwaipaja ambaye pia ni kijana mwanasheria,kuna haja ya timu yako kuchunguza namna ambavyo taratibu za uendeshaji wa chama kama zinafuatwa,bila kufanya hivyo na kuchukua hatua za haraka utajikuta umewapoteza viongozi wengi wazuri kwa mtindo wa kufukuzana bila kufuata utaratibu,hali hiyo inaweza kuwafanya wasomi na wasio wasomi kukidharau chama,it is very serious
10.Chama cha mapinduzi kinatumia mbinu mbali za kudhoofisha chadema,usipokuwa makini na hili utajikuta umepoteza viongozi wengi kwa maslahi ya ccm.kufukuzana ndani ya chama sio njia pekee na sahihi ya kuimarisha chama,kufukuza wanachama 15 au 20 bila sababu za msingi ni jambo la kushtusha sana
Chadema ni chama imara,kina viongozi wazuri ngazi ya taifa,wabunge wenye vipaji na wasomi lakini huku chini kuna matatizo makubwa sana,ni changamoto,usiruhusu maamuzi ya hovyohovyo kufanyika,hata yanapofanyika ni bora ukatuma timu yako kufanya uchunguzi kwanza ili kutoa maamuzi yenye kuonyesha mfano wa chama kinachotegemea kuingia madarakani.
Yawezekana wengine wakaona ni jambo rahisi kufukuzana chama pasipo kuzingatia misingi ya katiba na kanuni za chama lakini utabaki palepale,hatua za kuwafukuza kwenye chama pasipo kuzingatia taratibu zinaweza kuturudisha nyuma hasa sisi wenye kuamini katika mabadiliko na nguvu ya umma
Naomba kuwasilisha,