Kwako Mheshimiwa Rais wa Moyoni wa Watanzania
Ni hivi karibuni tu kumeibuka malalamiko kutoka miongoni mwa wanachama wako kuwa kuna mgogoro na tatizo la uongozi katika jimbo la Morogoro mjini.Yawezekana wasaidizi wako hawajakupatia picha halisi juu ya kile kinachoendelea lakini kupitia jukwaa hili napenda nikuarifu japo kwa kifupi kuhusu changamoto zinazokikabili chama chako ukiwa kama kiongozi wa juu kitaifa
1. Naomba ufahamu kuwa CHADEMA mkoani Morogoro haina ofisi ya Mkoa. Ofisi inayotumika sasa ni ofisi ya chadema wilaya ambayo hutumiwa kama ofisi ya mkoa. kinachofanyika ni viongozi kupishana viti kwa mfano, kama mwenyekiti na katibu wa mkoa hawapo ofisi hiyo inatumika kama ofisi ya wilaya. anapokuja Mwenyekiti au Katibu wa Mkoa ofisi hiyohiyo inatumika kama ofisi ya mkoa
2. Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Morogoro ni Mama Susan Kiwanga lakini hakuna chochote anachokifanya katika kuendeleza chama zaidi huonekana ofisini kunapokuwa na ugeni wa kitaifa ua ziara za viongozi wa kitaifa wilayani.
3. Mwenyekiti wa Mkoa makazi yake ni Dar Es Salaam hivyo ni vigumu sana kuwa karibu na ofisi yake na kupambana na changamoto za chama
4. Viongozi wa chadema wilaya wanaendekeza zaidi majungu,siasa za chuki,siasa za makundi na matokeo yake badala ya kufanyakazi za chama ikiwemo kubuni miradi na mikakati mbalimbali ya kuendeleza chama wanatumia muda wao mwingi kujadili watu
5. Wapo viongozi waliojiuzuru nyazifa zao kwa mfano Katibu wa Bawacha Mercy na mwenyekiti wake Levina Matambo.Viongozi hao wa Bawacha hakuna chochote walichokifanya tangu washike nafasi zao, mpaka sasa wakiulizwa ni watu wangapi wamejiunga na Bawacha tangu waingie madarakani hawatakuwa na jibu la kukupa.
6. CHADEMA Morogoro ina nguvu sana lakini viongozi waliopo bado wanatumia mbinu za kizamani katika kuongoza chama, si wafuatiliaji wa mambo, na mara nyingi wakiona mtu yupo mstari wa mbele katika kufanya mambo kitaalam au kuhoji wao wanakuwa wepesi wa kumtuhumu mtu huyo kuwa ni mamluki au ametumwa na usalama wa taifa au yupo usalama wa taifa,uthibitisho wa hili upo na ukihitajika utawasilishwa. kwa ujumla ni wepesi wa kuzusha jambo badala ya kufanya utafiti
7. Wapo watu wenye moyo wa kufanya kazi za chama kwa moyo na uzalendo na ambao wapo tayari kukubali mabadiliko na kuendana na kasi ya mabadiliko lakini wamekuwa wakijengewa mizengwe waonekane kama hawana thamani ndani ya chama kwa mfano, mtu kama Abel Luanda, Katibu wa Mkoa aliyejitahidi sana kufanya kazi za chama,mwenye uwezo wa kujenga hoja na mwenye kukubali ushauri wa maana lakini alipigwa vita na Mama Susan Kiwanga mpaka akaamua kuachia nafasi zake za uongozi, wengine ni kama Mheshimiwa Aquiline Magalambula, aliyekuwa Mgombea wa Chadema Morogoro Vijijini akichuana na mama Nkya,yupo pia katibu Mwenezi wa Wilaya ndugu Elias Mwalusako ambaye amejitahidi sana kukiimarisha chama hasa kupitia mikutano ya hadhara lakini mpaka sasa anapigwa vita na majungu kuwa alihongwa na Aziz Abood ili auze matokeo ya Ubunge Morogoro Mjini
7.Mama Kiwanga ni Mbunge wa Viti maalum,Mwenyekiti wa Mkoa wa Morogoro na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa lakini ameshindwa hata jitihada zake binafsi tu kubuni mkakati wa kuwa na ofisi ya Chadema Mkoa ambayo kimsingi ingemsaidia yeye kufanya shughuli za chama kwa utulivu na ufanisi zaidi,hii ni aibu kubwa
Yapo mambo mengi sana ya kuyafanyia kazi ili chama kisonge mbele lakini naomba nitumie nafasi hii kukujulisha tu kuwa hali ya kisiasa morogoro si nzuri na hatua za haraka zinahitajika,
nimeamua kukutumia uzi huu kwakuwa siwez kukufikia moja kwa moja na kukueleza changamoto zilizopo na nimeshindwa kuzipeleka changamoto hizi kwenye ofisi za chama kwakuwa zitapokelewa na kujadiliwa na watu walewale wanaotuhumiwa kuzorotesha chama