Dr Slaa sasa ni Mzalendo

Dr Slaa sasa ni Mzalendo

Katika hii nchi kuna vituko sana mpaka mtu unajiuliza mambo mengi sana!
Leo Kuna kundi linampamba Dr Slaa na kumwita Mzalendo, mpiganaji, upinzani wa kweli, mpinga ufisadi! Lakini kabla ya Lowassa Kuhamia Chadema hawa hawa watu walikua wanamwita Padri,kiongozi wa kanisa,Babu,Fisadi anayejikopesa pesa ndani ya Chama,walimwita ni mtu aliyetumwa toka vatkani na Ujerumani! alipewa majina ya kila aina!
Leo Dr Slaa anasifiwa kinafki na watu wale wale wanamwita Mzalendo wa kweli, mpiganaji! Hawa watu wanashindwa kuelewa kwamba Dr Slaa ni Kichwa kingine anawasoma tu wanavyohangaika na mwisho wa siku aibu yao.Ni mtu ambaye ambaye anazifahamu fika shida za watanzania, ameshaketi na wenzake mezani kuumiza vichwa ili kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi October na wakaona silaha pekee ni ile iliyoachwa na wapinzani wao wakuu! Hawa hawa watu wanaelewa kua kukaribishwa Lowassa CHADEMA ni baada ya vikao vingi vya kamati kuu na kuridhia suala hilo maana Mwenyekiti hawezi kua na sauti peke yake bila ya watendaji wenzake.
Badala ya kupeana mikakati ya namna ya kupambana na nguvu inayokuja kutoka UKAWA wanabaki kummezea Dr Slaa mate huku yeye akiwachora huku yuko bize kuandaa mikakati zaidi ya ushindi mwezi October. Sawa na ile hadithi ya Fisi kumfuatilia binadamu kwa nyuma huku akusubiri mkono uanguke ili aufaidi kumbe binadamu anasonga mbele, kitu ambacho hakiwezekani.
Nionavyo mimi hata kama Lowassa asingekuja UKAWA bado nguvu ingekua kubwa kwa sababu tu kitendo chao cha kihistoria kuungana na kua wamoja mpaka wanafikia kumtoa mgombea urais mmoja,mbunge mmoja kwa kila jimbo na madiwani kwa kila kata ilikua ni ushindi tu.Sasa Lowassa ameongezea nguvu ambayo ni kubwa kwanini watu wasichanganyikiwe? Kwanini watu wasikose usingizi? Tuwe wakweli tu kwa hili jambo!

Wacha projo onesha ni wapi daktari wa kanoni padri Dr.W.Slaa alipopambwa?
 
Last edited by a moderator:
Kama CHADEMA sio tena chama cha sera na maadili, basi huu ndio wakati wa Dr. Slaa kukihama CHADEMA ili apokelewe kwa mwbembwe na CCM na kupewa ulaji. CCM nao watajiona kuwa wameirudi CDM na kubeba wale wachache ambao wanamuunga mkono Dr. Slaa, kama vile Mzee Mwanakijiji n.k., bila hivyo huu ndio utakuwa mwisho wa Slaa kisiasa.

Mtasubiri sana haitakaa itokee Dr Slaa anajua alikotoka kisiasa.
 
Wala sina shaka na Dr. Slaa the next PM
 
MAHANJU

Ila ukitizama vizuri nyote mpo sawa make hata wanaomsifu lowasa leo ni wale walimuita majina yaleyale ya ufisadi,upapa,mpaka kumuita mgonjwa n.k,kwa hyo nyote mkubali hakuna adui wa kudum kwenye siasa,samahan lakin mkuu
 
Last edited by a moderator:
Dr.slaa ndiye my role mode,,,ktk uongoz uliotukuka,usiondoke my brother Dr.slaa tumwondoe mkoloni mweus
 
Last edited by a moderator:
Kweli Lowasa kawachanganya wapenda madaraka kiasi cha kufikiri Dr.Slaa anaweza kurubuniwa kwa sifa za kijinga toka upande wa pili. Inabidi waelewe kuwa Dr.ndiye aliyeongoza mradi wa kumleta El Cdm.
 
Tundu lisu jana akihojiwa Bbc alisema slaa ndo alifanikisha ujio wa lowasa aliratibu kila kitu hizi speculation zntoka lumumba buk 7
 
Back
Top Bottom