Dr. Slaa naomba maoni yako ktk hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa naomba maoni yako ktk hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, Apr 26, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mh. Dk Slaa nimewahi kutoa mawazo yangu kupitia forum hii ya JF nikisema kwamba wilaya, vijiji na hata mikoa kwa ujumla wake ile ambayo madini kama vile dhahabu, almasi, tanzanite na mengine yanapatikana ktk maeneo hayo basi wilaya na vijiji hivi vipewe japo asilimia 10 ya mrahaba utokanao na raslimali hiyo kwani wakazi wa maeneo hayo lazima wafaidike na mali iliyo ktk maeneo yao.

  Sasa nimesikia serikali ya CCM hawataki kabisa jambo hilo, najiuliza ni kwa nini?

  Kwa mtazamo wako wewe unalionaje hili??
   
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Kwa mtazamo wangu hili unalouliza Mkuu Magezi naona limo kwenye sera ya CHADEMA ya Majimbo. Mule wameeleza jinsi rasilimali za Taifa zinavyoweza kugawanywa kwenye majimbo ambayo rasilimali hizo zinapatikana. Angalia kwenye tovuti ya CHADEMA kwa maelezo zaidi nina imani itakuwepo.


   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Apr 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  S.S Pahres umejibu vema lakini pia aende kule kwenye sredi ya Dr Slaa kujibu hoja mablimbali iliyoanzishwa na Lunyungu ndi atapata majibu kirahisi kuliko kuanzisha nyu sredi.
   
 4. B

  Bull JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna uchaguzi CHADEMA kwa sababu Slaa Katumwa na Mungu
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Katika kampeni za uchaguzi mwaka 1995, bwana mapesa John Momose Cheyo akinadi sera za chama chake alisema: sehemu zenye dhahabu zifanane na dhahabu, akimaanisha maeneo husika yapate malipo kutokana na dhahabu inayochimbwa katika maeneo yao. Hili alilizungumza kwa raslimali zote. Kwa bahati mbaya au kwa ufinyu wa kuelewa, watu walimpuuza. Sasa miaka 15 baadae, hoja hii inarudi tena. Nimesikia hadi bungeni wakitaka sehemu ya mrahaba ipelekwe halmashauri ya wilaya! Kwa maana nyingine tuko nyuma miaka 15.
  Naunga mkono hoja, badala ya kuishia ngazi ya halmashauri, basi twende chini zaidi hadi kwenye serikali ya kijiji.
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Usiharibu mada
   
Loading...