Dr. Slaa: Magufuli haogopi kupoteza kura kwa kukemea ufisadi na kusema atawafunga wala rushwa!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516



Mtangazaji anatambulisha mada. Ni yule yule Kamonte aliyemhoji mara mbili zilizopita.

Dr. Slaa: Nitaendelea kupigia kelele mambo yanayohusu taifa langu

Dr. Slaa: Uchaguzi huu ni wa kipekee. Watanzania wanataka mabadiliko. Umma haujatafsiri maana ya mabadiliko

Dr. Slaa: Dhana ya mabadiliko haijaelewa vyema. Dhana hii si mpya. Ilisemwa hata na Hayati Mwalimu Nyerere

Dr. Slaa: Mabadiliko yana sura mbili. Yapo ya kutoka pazuri kwenda kubaya na ile ya kutoka kubaya kwenda kuzuri. Anatoa mfano wa Dikteta Benito Mussolin wa Italia

Dr. Slaa: Ninahisi tafsiri ya mabadiliko haijaeleweka. Hata wasomi hawaelewi. Kwa upande wa wenzetu wapinzani wanachukua mifano ya hata Marekani ambapo Obama alikuwa na sifa..

Dr. Slaa: Msingi wa mabadiliko ni kutoka ulipo kwenda mahali kwingine. Kwenda kuzuri. Kuna dhana ya mabadiliko na mapinduzi. Kuna kauli za kutishia kuingia barabarani

Dr. Slaa: Wapo wenye tamaa ya kwenda Ikulu. Hiyo si ambition ya uongozi. Ambition inaambatana na maandalizi

Dr. Slaa: Kumchagua Rais si suala dogo. Tutavumilia kwa miaka mitano

Dr. Slaa: Amani inapaswa kuwa ajenda kuu kwakuwa ni zao la demokrasia.

Dr. Slaa: Naungana na Jaji Warioba kuwa rushwa ilikuwa inatisha. Serikali za Mitaa hupewa asilimia 23 za bajeti. Asilimia 75 ya 23 hupotea kwa rushwa. Kuna grand na petty corruption. Rushwa ndogo huumiza kuliko kubwa kwakuwa zinagusa watu wanyonge.

Dr. Slaa: Katika kampeni za mwaka huu,chama changu CHADEMA kimeacha ajenda ya rushwa. Hata nyimbo za hamasa za kupinga rushwa hazisikiki. ACT ni kama wanairithi CHADEMA kwenye ajenda ya rushwa. Nampongeza Zitto na chama chake. Yuko committed

Dr. Slaa: Msingi wa mabadiliko ni kutoka ulipo kwenda mahali kwingine. Kwenda kuzuri. Kuna dhana ya mabadiliko na mapinduzi. Kuna kauli za kutishia kuingia barabarani

Dr. Slaa: Dr. Magufuli anasisitiza kuwa anapiga vita rushwa. Sijaona jambo hilo kwa CHADEMA. Ukiwa mchafu huwezi kukemea. Dr. Magufuli anasema ataanzisha Mahakama Maalum za rushwa na ukimtazama anaaminika. Dr. Magufuli sijawahi kusema ni msafi. Lakini ana nafuu kati ya wagombea nane

Dr. Slaa: Tulimpinga Rais Kikwete mwaka 2010 kuwanyanyua Mramba,Chenge na Lowassa. Magufuli haogopi kupoteza kura kwa kukemea ufisadi na kusema atawafunga wala rushwa. Magufuli ni jasiri

Dr. Slaa: Kuna michakato inafanyika kama kuwaleta na malori na mabasi. Chama changu kilikuwa hakibebi watu. Lakini kilibeba kwenye mkutano wa Jangwani.

Dr. Slaa: Baada ya kusikiliza na kuona mikutano,kwanza tujiulize tunataka Rais wa aina gani. Mwenye vigezo vya kupambana na rushwa, Magufuli anafaa. Rais hawezi kuongea kwa dakika kumi, nani atakuwa Rais? Ni akina Sumaye?

Dr. Slaa: Tanzania ni mama yetu. Tukichezea amani ya Tanzania,sote tutaathirika. Nawaomba NEC wasimamie sheria. Watanzania tusimamie amani yetu.
 
Last edited by a moderator:
Dr slaa,dhana ya mabadiliko,haijafafanuliwa kwa wananchi na kwamba waweza pata mbadiliko lakini akakupeleka kubaya zaidi
 
Mtangazaji anatambulisha mada. Ni yule yule Kamonte aliyemhoji mara mbili zilizopita.

Dr. Slaa: Nitaendelea kupigia kelele mambo yanayohusu taifa langu

Dr. Slaa: Uchaguzi huu ni wa kipekee. Watanzania wanataka mabadiliko. Umma haujatafsiri maana ya mabadiliko

Dr. Slaa busara ilikuwa ni kukaa kimya kama ulivyoahidi maana hata tuliokuamini kwa miaka mingi tunaanza kuona unatumiwa.
 
Eti wagombea wote wawili hawajaelewa mabadiliko. Ina maana yeye slaa tu ndio anaelewa. Jamani...
 
Huyo mzee bana, Hivi anafikiri mabadiliko ni Slaa kua rais tu? pambaf zake eti shutuma, shutuma my foot yeye alizaa akiwa padre na tulimpa kura 2010 japo hazikutosha
 
Back
Top Bottom