Dr. Slaa: Mafisadi hawana nafasi CHADEMA

Dr. Slaa: Mafisadi hawana nafasi CHADEMA

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,060
Reaction score
309
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa wako radhi kuchukiwa kwa uamuzi wao mgumu wa kuwafukuza mafisadi ndani ya chama hicho.

Akizungumza jana katika mahojiano na moja ya kituo cha runinga, Dk. Slaa alisema Kamati Kuu ya chama hicho ilifikia uamuzi kuwachukulia hatua baadhi ya madiwani akiwemo mmoja wao aliyekiri mbele ya kamati hiyo kuwa alipewa sh milioni 20 na CCM.

Dk. Slaa alisema kuwa litakuwa ni jambo la ajabu kwa chama hicho kukubali kukumbatia mafisadi na wala rushwa wakati kila siku wamekuwa wakipigania matatizo hayo yaondolewe ndani ya serikali.

"CHADEMA haimuonei mtu, inatenda kwa mujibu wa katiba; hivi kweli tunaweza kumvumilia kiongozi ambaye amekiri hadharani kupokea kiasi cha fedha kama rushwa kutoka CCM? Hii itakuwa ni aibu kwa chama ambacho kinawanyooshea kidole kila siku walarushwa na kutaka waondolewe serikalini," alisema.

Kuhusu kuwepo kwa watu wanaolalamikia ukali wake, Dk. Slaa alisema kuwa kwa nafasi aliyonayo ni lazima awe mkali kutokana na kulazimika kusimamia misingi ya chama. Dk. Slaa alisema kuwa afadhali achukiwe na watu wachache, lakini apendwe na Watanzania walio wengi.

Alisema kuwa, suala la madiwani wa Karatu hawezi kulizungumza kwa kuwa Kamati Kuu iliunda tume ya uchunguzi ili kuchunguza suala hilo ambapo jukumu hilo amepewa mwenyekiti wa chama hicho.

"CHADEMA hatuwezi kuvumilia harufu yoyote ya ubadhirifu inayotajwa mahali popote …tunalazimika kuchukua hatua ili kuhakikisha
tunalijenga taifa lililo na misingi kama ile iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere," alisema.

Alisema kuwa hawawezi kuinyooshea kidole CCM halafu ndani ya CHADEMA waachie uozo.

Dk. Slaa alitolea mfano uamuzi ya Kamati Kuu iliyoamua kuwafukuza madiwani watano wa jijini Arusha na hata uamuzi wa mahakama ulipotoka ilionekana kuwa chama kilisimamia haki. Alisema kuwa ni vizuri kuwa na watendaji wachache wanaozingatia maadili.

"Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kuwafukuza wabunge sita wa CCM walioshindwa kuzingatia maadili, lakini kwa sasa wameamua kulindana ndiyo maana wanashindwa kuwachukulia hatua mafisadi wa Meremeta, walioweka fedha zetu Uswisi, Fedha za Richmond, EPA na hata zile za rada," alisema.

Alisema kuwa ni lazima Watanzania wadai fedha zao ambazo wanaamini zinawafaidisha watu wachache tu.
 
Huyu mzee hanaga jipya zaidi ya kuongelea mafisadi??
 
Hahahahahahahahahahahahaha
huyu mzee ana wasumbua sana ambaye hana jipya!
Ana msumbua hadi Makamba!

Huyu mzee hanaga jipya zaidi ya kuongelea mafisadi??
 
Hakika Slaa unakubalika, kila mtu kapewa mdomo ili aongee na vidole ili aandike. Wataongea sana lakini ukweli Mungu kakutuma. Jua tu wao wanaweza kuwa na Mungu wao. Tunaisubiria 2015 kwa hamu najua wengi wetu tutafika. Hawa wara rushwa hiyo ndo dawa yao. Asante sana mtumish for your kindness ur giving as watanzania tunaokuamini
 
Babu kwanza arudishe pesa za ruzuku alizojikopesha ili akamjengee nyumba girlfriend wake (au woman friend for that matter). Chama siyo bank!!!
 
Huyu mzee hanaga jipya zaidi ya kuongelea mafisadi??

sasa wewe unaona ufisadi sio tatizo? matatizo yetu mengi yanasababishwa na ufisadi wa viongozi walioko madarakani.
 
Babu kwanza arudishe pesa za ruzuku alizojikopesha ili akamjengee nyumba girlfriend wake (au woman friend for that matter). Chama siyo bank!!!

Bila shaka wewe ni mmoja wa wale waliyo ficha fedha uswisi
 
Hao ni madiwani. Vipi kuhusu hili sakata la vijana wa chadema?
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasiafisadi ndani ya chama hicho. Akizungumza jana katika mahojiano na moja ya kituo cha runinga, Dk. Slaa alisema Kamati Kuu ya chama hicho ilifikia uamuzi kuwachukulia hatua baadhi ya madiwani akiwemo mmoja wao aliyekiri mbele ya kamati hiyo kuwa alipewa sh milioni 20 na CCM. Dk. Slaa alisema kuwa litakuwa ni jambo la ajabu kwa chama hicho kukubali kukumbatia mafisadi na wala rushwa wakati kila siku wamekuwa wakipigania matatizo hayo yaondolewe ndani ya serikali. “CHADEMA haimuonei mtu, inatenda kwa mujibu wa katiba; hivi kweli tunaweza kumvumilia kiongozi ambaye amekiri hadharani kupokea kiasi cha fedha kama rushwa kutoka CCM? Hii itakuwa ni aibu kwa chama ambacho kinawanyooshea kidole kila siku walarushwa na kutaka waondolewe serikalini,” alisema. Kuhusu kuwepo kwa watu wanaolalamikia ukali wake, Dk. Slaa alisema kuwa kwa nafasi aliyonayo ni lazima awe mkali kutokana na kulazimika kusimamia misingi ya chama. Dk. Slaa alisema kuwa afadhali achukiwe na watu wachache, lakini apendwe na Watanzania walio wengi. Alisema kuwa, suala la madiwani wa Karatu hawezi kulizungumza kwa kuwa Kamati Kuu iliunda tume ya uchunguzi ili kuchunguza suala hilo ambapo jukumu hilo amepewa mwenyekiti wa chama hicho. “CHADEMA hatuwezi kuvumilia harufu yoyote ya ubadhirifu inayotajwa mahali popote …tunalazimika kuchukua hatua ili kuhakikishatunalijenga taifa lililo na misingi kama ile
 
Tunasubiri amfukuze na Zitto kama anaubavu huo. Sio kujisifia kwa kufukuza watu wadogo kwenye chama, aonyeshe ukali wake kwa Shibuda na Zitto.
 
Ndio maana CCM hawalali wakimkumbuka Dr. Slaa.

Agenda moja tu imewashinda awamu zote ya 3 na ya 4, je vipi kuhusu hizo agenda nyingine?

Dr. Slaa weka mguu wako hapo hapo, ndipo penye kuwauma zaidi. Usiwape pumzi hawa majangili
 
Dk. Bado hizi tetesi za usaliti vipi? Si ndio harufu zenyewe hizi za ufisadi?
 
Ndiyo maana anapigwa Vita

Na wewe limekugusa mzee wa lumumba kwenye Bahasha za kaki

Hahahahahahahahahahahahaha
huyu mzee ana wasumbua sana ambaye hana jipya!
Ana msumbua hadi Makamba!

sasa wewe unaona ufisadi sio tatizo? matatizo yetu mengi yanasababishwa na ufisadi wa viongozi walioko madarakani.
Namshangaa anapataje nguvu ya kuongelea ufisadi wakati yeye ana tuhuma kibao zinamkabili ndani na nje ya chama chake. Angetumia muda wake mwingi kudeal na hizo tuhuma badala ya kuanza kuwanyooshea wengine vidole. BTW, yeye ana pakukimbilia CDM ikifa, je nyie maficha nyuso zenu wapi?? Soon we will be singing the same song, kidumu chama cha mapinduzi!!!
 
Huyu mzee hanaga jipya zaidi ya kuongelea mafisadi??

Kwani haujui athari za ufisadi katika jamii?ufisadi ni sumu inayoharibu kila jambo katika nchi!ni lazima upigiwe kelele usiku na mchana,jaribu kushirikisha ubongo wako hata kidogo na usukumwe na uzalendo sio ushabiki wa kichama
 
Back
Top Bottom