Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,068
- 151,316
Wadau,katika gazeti la Dira la leo Jumatatu,Juni 6-12,2016 toleo no:422, kuna habari kuu inayohusu tuhuma za ufisadi wa mishahara ya wafanyakazi wa hospitali ya CCBRT wa zaidi ya shilingi bilioni 300.
Habari hii ni ndefu kidogo ila kwa kifupi iko hivi:
November 24,2007 hospitali ya CCRBT iliingia makubaliano na kusaini mkataba na serikali kwa kuanzisha hospitali teule ya mkoa wa Dar-es-salaam kupitia jiji la Dar-es-salaam (City Council(DCT).
Mkataba huo unaonyesha kuwa serikali itakuwa na jukumu la kulipa mishahara kwa watumishi,kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu pale itakapowezekana na mengineyo.
Kwa mujibu wa mkataba huo,serikali ndio itakuwa ikilipa mishahara ya watumishi na CCRBT yenyewe itaendelea kutoa marupurupu (Additional payments) kwa watumishi hao.
Nyaraka zinaonyesha kuwa serikali ilikuwa ikiingiza fungu la fedha za mishahara kwenye akaunti za CCBRT kwa ajili ya watumishi,lakini inadaiwa kuwa watumishi hao hawakuwahi kulipwa mishahara hiyo ya serikali na badala yake walikuwa wakilipwa marupurupu na CCBRT.
Chanzo chetu(chanzo cha gazeti) ndani ya hospitali hiyo kilidai kuwa mkataba huo ulionyesha kuwa mshahara wa mfanyakazi utalipwa na serikali na CCRBT itatoa nyongeza ya mshahara huo kama posho lakini wafanyakazi hao wamekuwa wakilipwa nyongeza hiyo kama mshahara halisi kinyume na makubaliano ya mkataba.
Gazeti limeandika mengi na limeeleza kuwa baada ya watumishi kubaini mishara inaingizwa walianza kufanya migomo na mikutano mbalimbali hali iliyosababisha wao kutaka kukutana na mwenyekiti wa bodi,Dk.Willbroad Slaa.
Kwa mujibu wa gazeti,Dk.Slaa aliwaahidi watumishi hao kuwa jambo hilo ni zito na kwamba atalifuatilia na kulitolea majibu,lakini hadi sasa hajazungumza chochote na inadaiwa hayupo nchini kwa sasa.
ChanzoIRA
Dk.Slaa,wewe ukiwa kama member wa mtandao huu na mpinga ufisadi mkubwa, tunaomba ufafanuzi wa swala maana sasa limeshakuwa public.