Dr. Slaa kesho atasema nini?


Hii kitu, kama rushwa kwa slaha na mpenzi wake, inafanya Tanzania isiendelee! Ni lini viongozi wetu wata simama na kusema pesa hapana! Kama unakemea ufisadi na kisha kununulika kirahisi hata kwa bei gani na wewe ni fisadi tena fisadi nguli! Tutawaweka wote kwenye historia ili vizazi vyao viwatambue baadae.
 

Mkuu umenikumbusha suala la ku-revoke hati za watu kwa kisingizio cha matumizi ya Serikali! Alikuwa anazunguka na wapiga picha wa baadhi ya vituo vya television, rafiki yangu aliponea chupu chupu kunyanganywa kiwanja chake baada ya Lowassa kuondolewa Wizara ya aridhi fasta!!
 

Kwa hiyo kura tumpe mgombea gani mbali na CHADEMA &CCM?
 
Nchi hii naona ni ya walambaji. Kila mtu anaambiwa kalamba. Oooh unajua Mbowe kalamba ...mara ooh Slaa kalamba. Mara ooh Zitto kalamba mara ooh Kitila kalamba. Yaaani ni shiiiida. Upigaji tu kwa kwenda mbele. Najua hata wewe unaeisoma post yangu unakosa fursa tu. Ukipata najua lazima utalamba tu.
Nchi hii ni ulambaji tu. Kwa kweli inakatisha tamaa saaaaana.
 

WEWE mtu km huna PHD basi nakuzawadia bureeee . una akili sana mkuu
 
Hivi naye NI mgombea na anafanya kampeni? Hebu nikumbusheni chama chake NI kipi na sera yake NI ipi?
 
Tumeingia wiki ya pili sasa, amepewa majina yote, wamesema watampuuza au wamempuuza, lakini hayaishi. Akinyamaza shida, akizungumza shida. What next? Tusubiri. Tarehe 25 OKTOBA 2015 sio mbali-Tanzania bila CCM inawezekana lakini mikakati ya ushindi na kufaidi ushindi inahitajika au sivyo giza mbeleni.
 
SIO KWEEELI, Dr. Slaa amekuwa akiishi na ameendelea kuishi kwa kuamini CCM ni ngome kuu ya mafisadi na hajawahi kubadili msimamo huo. Yeye Slaa ni nani ndani ya chadema amkatae Lowassa peke yake. Wajumbe woooote walikubaliana kumpokea Lowassa, yeye Slaa ni nani Chadema? Hata CCM waliwahi kukwaruzana na katibu wao mkuu ndugu Horace Kolimba (rip) alipotamka hadharani kuwa CCM haina dira wala mwelekeo, alilaumiwa na wana CCM kwa kuchukuwa msimamo wa peke yake na kuutangaza hadharani nje ya vikao. Dr. Slaa kama Kolimba, hafai na anastahili kuhojiwa na kuadhibiwa na chama kama vile Horace alivyoadhibiwa na CCM. Chama ni vikao na maamuzi ya pamoja sio utashi wa mtu mmoja mmoja na familia yake, maana chama kiko juu kuliko mtu hata kama awe ndo mwenyekiti, jenga hoja za kuwashawishi viongozi na wanachama wenzio kwa kutumia utaratibu wa kichama na vikao halali vya chama chako, watakuelewa tu kama una hoja. Kama hoja yako haikuungwa mkono na wengi kaa kimya. Lowassa kapiga U-turn na kuiacha hoja yake ya tangu mwaka 1995 kuwa CCM hakifai, inafuga wezi, imesababisha rushwa, umaskini, ufisadi, ni wezi wa kura, n.k na kumshambulia Lowassa tu kana kwamba Lowassa ndiye chanzo cha uchafu woote wa CCM na serikali zake zote zilizopita tunaoushuhudia Tanzania. Hakuna haja ya kufanya utafiti ili kujua kama Dr. Slaa kwa hili amehongwa, ana uchu wa madaraka, ana ugomvi binafsi na Lowassa, ni muongo, haaminiki, ni mwana CCM halisi.
 
Watanzania acheni kumjadili huyo babu. Ameshastaafu siasa. Tunachotakiwa kufanya ni Mabadiliko tu mana tumechoka.
 
WEWE mtu km huna PHD basi nakuzawadia bureeee . una akili sana mkuu
karibu sana, tusaidiane kwa njia mbalimbali kuifanya tanzania iwe ya watanzania wote bila kujali itikadi za vyama, dini wala kabila. Sisi tuliobahatika kusoma na kupata uelewa tusaidie wale ambao mungu hajawajalia uwezo huo bado.
 
Great traitor aliyeshtua bongo zenu na mkaijua CCM na makando yake ...... huyu shujaa wenu wa sasa ana impact gani kwa vijana wa sasa .....

Dr kafanya kazi nzuri kuijenga CDM, but anachokifanya sasa hatukukitegemea kwa mtu kama yeye. Yaani kawa mfanya propaganda wa CCM. Kwa hili kafanikiwa sana kwa kujifanya yupo neutral.
 
Jinsi dr Slaa anavyozidi kuongea na kujibu hoja mbalimbali sidhan kama anapata heshima anayoitafuta, atazidi kupoteza heshima...Hii ndivyo ilivyo historia ukijisemeasemea saaaaana, yaani unatumia nguvu nyingi kujitetea binafsi tu mwisho hata kama una hoja unapwaya tu unaanza kuonekana hovyo hovyo tu. Kama kweli Dr Slaa atarudi kuongea mara ya tatu hakuna attention yoyote kwa watu , Na watu wajanja kweli kweli wamemtegeshea kuhangaika na hoja za wakeze na yule swaiba wake wa karibu wa kiroho. Wakati Mh Lowasa anaendelea na speed zake 120-140km/hr du!
 
karibu sana, tusaidiane kwa njia mbalimbali kuifanya tanzania iwe ya watanzania wote bila kujali itikadi za vyama, dini wala kabila. Sisi tuliobahatika kusoma na kupata uelewa tusaidie wale ambao mungu hajawajalia uwezo huo bado.

amen ubarikiwe sana mkuu
 
mi binafsi naona angenyamaza pia asome majira huu upepo c wa kawaida
 
Jamani huyu Dr. Slaa mbona hana hata thamani ya kumjadili. Kwa maana watu walimwaminia kwa makubwa lakini tazama jinsi alivyojiangusha mwenyewe tena kwa madogo kabisa. Waswahili husema... 'lipitalo hupishwa'​
 
Slaa hatumhitaji tena. Mimi nimemformat kabisa kichwani mwangu
 
Kwa mleta mada,
Sioni kama unatambua unachokilaumu ama kulalamika kuhusu Dr.Slaa.! Ni ajabu sana kwa "Vijana" wenye akili inayotakiwa kufanya kazi kwa umakini kuandika mambo uliyoandika bila kufikiria kwamba mnajaribu kupotosha watu.
Dr.Slaa alieleza kwa ufasaha na uwazi sababu za yeye kujitoa CDM na kukaa kimya kwanza,na hili lilitoa matokeo yafuatayo:
1-Minong'ono na habari zisizokuwa za ukweli kutoka kwa watu wasiyo makini na wadandiaji wa habari kwa kutumia uzushi.Tukianzia ndani ya UKAWA yenyewe kuuficha ukweli wa nini kilichotokea.Tuliambiwa na Mbowe ya kwamba Slaa yupo mapumzikoni na atarejea pale atakapomaliza likizo yake.Tukasikia na kusubiri.
2-Mitandao ya kijamii tukashuhudia habari nyingi zisizo rasmi kwamba Dr.Slaa atahudhuria ufunguzi wa kampeni za CCM jangwani...nazo zikawa hazikuzaa matunda.Ziliandikwa na zikasemwa taarifa nyingi na hata nyingine za kutengeneza ionekane ya kwamba mzee huyu kaziandika.Lakini yote haya yalizushwa tu.
Kuna msemo "Silence means a lot.."Kwa hivyo ukimya wake huu uliibua mengi kutoka kwa wadau wa habari na matukio.
Sasa ukaja wakati akaamua kuachana na ukimya ule baada ya kuona kuna upotoshaji mwingi ambao nitauita uchokozi kwa Dr. Slaa atasema nini.Akaitisha mkutano wa wanahabari na wengi tukawa na shauku ya kujua mengi kutoka kwake ili kuondoa minong'ono iliyozagaa katika jamii yetu.
Kiukweli alijieleza kwa ufasaha na mpangilio mzuri tu hata kwa mtu aliyekunywa Whisky angemuelewa.
Hoja zile zilizungumzia ukweli wa mambo yalivyotokea na yalikuwa mambo ya msingi ikiwa ni pamoja na ushahidi wa nakala mbalimbali alizozionyesha pale.Nilitarajia wahusika waliotajwa katika mkutano ule na wao kujitokeza kujibu hoja zile ili sisi wanajamii tusikilize na kuweka kwenye mizani vichwani mwetu kupima na kutambua ukweli wake.
Cha ajabu kabisa tukashuhudia kelele za stand ya mabasi!!!!Kila mmoja ananadi biashara yake itoke!
Si CHADEMA,Lowassa,Prof.Safari waliyojitokeza kujibu tuhuma zile kifasaha.Ama UKAWA ambayo mpaka sasa hatumjui ni nani msemaji mkuu. Ni James Mbatia,"Askofu" Gwajima,Gazeti la Mawio au ni nani ili pawepo na mawasiliano rasmi kati yetu.
Kituko kingine,ni kwa "Askofu"Gwajima alipoamua kujitokeza na kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema yake.Hapa tukawa na shauku ya kujuwa mambo ya msingi kutoka kwa Askofu huyo.Badala ya kujibu tuhuma zile tukajikuta tukisimuliwa mambo BINAFSI kati ya Dr.Slaa na mwenzi wake Josephine!!!
Kimsingi watuhumiwa wa saga hili hawana muda wa kujibu lolote wanaona bora liende.Huu ndio ukweli wenyewe.
Kwa nchi za wenzetu jambo kama hili halichukuliwi kimzaha.Litatakiwa lipatiwe majibu yatokanayo na shutuma.Na umma unatakiwa uridhike na majibu yale.
Sasa tunahitaji mabadiliko ya aina gani kama anayepita kuomba kura,yeye na timu yake hawana hata msemaji rasmi?
Wanataka kushika dola na ya Mungu mengi.Katika masuala ya kiutawala kuna mipangilio na taratibu rasmi kwa ajili ya kiitwacho REFERENCE.
Leo hii ukimtuhumu Rais wa Tanzania kwamba ni mlevi,tuhuma hii haitajibiwa na Mchungaji Christopher Mtikila.Itajibiwa na Salva Rweyemamu wa Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu.Hili lipo wazi.
Ukiituhumu wizara,suala lile litajibiwa na katibu mkuu wa wizara husika au mtu maalumu ambaye ni msemaji kisheria.
Kwa hivyo nahitimisha hivi:
Maelezo ya Dr. Slaa na tuhuma zilizomo bado hatujapata majibu na badala yake zinaning'inia na kila mmoja anajibu anavyoona ni sawa kwa akili yake.MILUZI MINGI INAMPOTEZA MBWA.
Kiujumla suala hili lipo sawa kabisa na shughuli za sokoni.Dr.Slaa katoa hoja.....majibu ya hoja ni WORK DONE=ZERO!
Wasalaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…