Threesixteen Himself
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 8,349
- 8,081
Jino linaniuma sana kwa kweli. Huu uzi uwe kwa kiswahili jamani wengine tuna matatizo ya meno hatuelewi
Basi kama vipi wewe tuambie Slaa alipo.
Yericko,
Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.
sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.
Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.
Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome.
==========
Moderator:
Baada ya wadau kutaka maoni ya Dr. Slaa yajitegemee na hoja ya Yericko ifungwe, tumeona ni vema kuiweka hoja hii ikijitegemea kama ilivyopendekezwa. Majibu ya msingi yapo hapa