Wana JF,
Kwanza nawapa pole sana wale wote waluiokuwa wamestushwa na Uzushi wa Dr. Slaa kupata ajali na kufa". Poleni sana kwa usumbufu huo. Nawashukuru sana wale wote walionipigia simu kutaka kujua ukweli au mmoja kwa moja kwangu au kwa njia ya walio karibu nami. Asanteni sana kwa Concern yenu. Aidha nawashukuru sana wana Jamvi wote, kila mmoja kwa jinsi alivyojadili kwa hisia yake, ndio uhuru wa mawazo. Miminawashukuru wote. Sasa basi:
i) Ushahidi wa uzushi huo ni Simu nilizopigiwa mimi na watu mbali mbali jana jioni na leo asubuhi. Sidhani kama kuna hitajika ushahidi zaidi ya uwepo wa uzushi huo. Mimi mwenyewe nimepigiwa simu hizo. Tofauti ni kuwa Taarifa ya Dr Balele ilianzia hapa hapa JF, wale wanaofuatlia wanajua ilikoanzia.Tena kwa mtu aliyesema yuko Hospitalini Bugando, na baadaye kusema ameshuhudia mahema yakifungwa "nyumbani kwake kuashiria msiba. Ni dhahiri kama mtandao wetu umefikia hatua ya watu kuzushiana vifo, basi Taifa limefika pabaya, hasa kwa wasomi "mwenyewe uwezo wa kutumia mtandao hategemewi kuwa mtu wa Kawaida.
ii) Napenda kuwathibitishia wana JF na wapenzi wetu na watanzania wote kuwa niko salama salimini, hapakuwa na tukio lolote, hata la kuashiria ajali iwe ya gari au bafuni. Hii ndio tofauti na tukio la balele, Uzushi unatolewa ufafanuzi na siyo kugeuza kjuwa siasa kama baadhi ya WanaJF wasiopenda kufanya utafiti kabla ya kutoa kauli wanavyotaka kuonyesha hapa Jamvini. Ndiyo maana napenda wapenzi wetu na Watanzania kwa ujumla waelewe kuwa hakuna tukio lolote na wawe na amani. Linalokuja au lilikuwa linapangwa na wenye kuzusha siwezi kufahamu na wala si nia yangu kulizungumzia.
iii) Kwa Taarifa yenu jana kuanzia saa 6 Mchana nilitembelea Shule ya Sekondari ya Dr Willibrod Slaa, iliyoko Basodawish, Wilaya Karatu na kufanya mkutano na Waalimu hadi saa 9 mchana tukipanga mikakati mbalimbali ya kuendeleza shule hiyo ya Wananchi. Kuanzia saa 9.30 hadi saa 12.15 alasiriri nilifanya mkutano wa ndani na uongozi wa Chadema Wiliya ya Karatu na wadau mbalimbali. Kwa sasa niko mjini Arusha nikijiandaa kwenda Mahakamani kama mlivyokuwa mnafuatilia kwenye vyombo vya habari. Nawatakia heri sana wote.