Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,980
- 9,558
na Irene Mark na Janet Josiah
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeipa serikali sharti la kufanya mazungumzo ya kumaliza utata uliotokana na kinachodaiwa kuwa uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi.
Kimesema kiko tayari kukutana na serikali ilimradi ikubali kuunda tume huru ya kuchunguza uhalali wa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuunda upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuandika Katiba mpya.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, katika Ofisi za chama hicho, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema utayari wa CHADEMA kukutana utatokana na utayari wa serikali kukubali mapendekezo hayo, ili kujiridhisha na kuwapa haki Watanzania wanaolalamikia mfumo wa uchaguzi na katiba mbovu.
Alisema azma ya CHADEMA ni kushinikiza mabadiliko ya Katiba kabla ya 2015 ili kuepusha shari inayoweza kutokea siku za usoni kutokana na dhuluma inayolindwa na mfumo wa Katiba na sheria.
Alisema haikubaliki kimantiki kwamba matokeo ya ubunge yanaweza kuhojiwa lakini ya rais hayawezi kuhojiwa, hata kama kuna kasoro za wazi.
Alisema pia kuwa si sahihi kuacha Tume itangaze mshindi wa urais hata kama ameshinda kwa kura moja tu, kama ilivyo sasa. Anapendekeza mfumo uruhusu mshindi apatikane kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote.
Alisema pia ni vema Watanzania wapatiwe majibu kwa nini Tume ilitangaza kuwa waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 20, lakini waliojitokeza ni milioni nane (8); jambo ambalo linatia shaka kwamba huenda kulikuwa na hila katika mfumo mzima wa uchaguzi.
Ninaamini kwamba kama umeshindwa kupigiwa kura na Watanzania wapatao asilimia 70, ujue wananchi hawakupendi, na nchi haiwezi kutawalika, alisema Dk. Slaa.
Hata hivyo, alisema kutokana na kasoro hizo pamoja na nyingine zilizomo katika Katiba, kuna ulazima wa kuwapo kwa Katiba mpya ili chaguzi zitakazofuata zifanyike kwa uhuru na haki.
Hivi karibuni CHADEMA ilitoa tamko la kutoyatambua matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na NEC kwa madai kuwa taratibu nyingi zilivurugwa na Tume hiyo kwa lengo la kumbeba mgombea wa chama tawala, Rais Kikwete.
Alisema ingawa katika kipindi hicho cha kutangaza matokeo ya rais, CHADEMA iliipelekea NEC malalamiko ya kutoridhika na kuitaka isitishe na wao kuendelea kwa kukubali kasoro za jimbo moja la Geita ni udhaifu.
Msimamo wa tamko hilo ulionyeshwa kwa vitendo mwishoni mwa wiki iliyopita na wabunge wa chama hicho walipotoka kwenye ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Kikwete kuanza kuhutubia.