Dr Slaa aporomosha matusi kuhusu suala la njama la kumuua Zitto

Status
Not open for further replies.
Pumbavu Mali tusi? Mwandishi nahisi hujaenda shule wewe.
Unakuza ilo neno kama ni tusi kubwa Daa..mwaka huu kazi mnayo , ila bado mbinu izo ni changa kuiuwa CDM.
"CDM itakufa kabla 2015" Haya yalikua maneneno ya Mh. wassira
 
Mwampamba. Nakuuliza angalia sehemu niliyochora alama

"Zitto anatakiwa aache tabia ya kufunika funika mambo, ajue nimemwokoa sana katika mambo mengi, mfano mauaji ya Morogoro yaliyopangwa na Chadema yalimlenga Zitto, alikuwa atolewe kafara. Yule muuza magazeti aliyepigwa risasi Morogoro akafa, siku hiyo ilikuwa afe Zitto," alidai Mwampamba.

Yule muuza magazeti aliyepigwa risasi Morogoro alipigwa na CHADEMA au alipigwa na POLISI ina maana siku hiyo Polisi walipanga kumuua Zitto. Au unasemaje Mwampamba.

Umeshahama chama yote haya ya nn kwanini musiendeleze sera za ccmafisi. Kama mlikuwa na taarifa zote izo na mkakaa kimya mjue ni kosa. Nakupa story fupi tu.
Hapa uingereza kuna mbunge/waziri katika serikali ya Cameron alijiuzulu baada ya kubainika kuwa alisema uongo baada ya kukamatwa kwa kuendesha gari kwa speed inayozidi miles 70 katika barabara zao kubwa. Alidanganya kuwa aliyekuwa anaendesha ni mke wake(walikubaliana na mkewe). Na kweli mke wake alipigwa faini na kutolewa point kwenye leseni yake. Baada ya muda/miaka kupita waliachana na mkewe, mke akatoa ile siri. Matokeo yake bwana ikabidi ajiuzulu kutokana na io issue. Kesi ikaenda mahakamani unajua matokeo yake ni nini. Wote wawili wako jela. Mke yuko jela kwa kutokusema ukweli wakati ule. Hivyo nanyi ni waganga njaa kama njama zilikuwepo ilitakiwa mkaripoti polisi kuliko kukaa kimya na kuanza kubwabwaja sasa. Kwanza nyie ndio watuhumiwa wa kwanza.
 
Watakaoleta machufuko nchi hii ni CCM, walipozidwa uchaguzi wa 2010 walianzisha propaganda za udini ambayo matokeo yake kwa sasa yanaendelea kuonekana, wameona hiyo haitoshi wameanza propaganda ya ugaidi ambayo nayo tutegemee matokeo yake muda si mrefu. Wangejikita kutekeleza ahadi zao badala ya kupoteza muda na resources kwenye mambo ya kipuuzi kama haya
 
Magazeti kama haya sidhani hata kama unaweza kufikri kulinunua usome kama unatumia akili zako sawasawa.na hata hapa kuwajibu ni kuwapa mabichwa tu hawa madada, ingawa si vema pia kuwaaucha waendelee kueneza ujinga wao. Maana ujing ukitjwa sana, watu wanaweza kuuamini.

To be honest Gazeti hili linaandika non-sense. Kwanza Dr. slaa tunamjua-hayo mwandishi anayoyaita matusi, Dr. hawezi kuyatamka, Ni ujinga kufikiri mawazo na njaa zako zitaisha kwa wewe kumripoti vibaya Dr. Slaa.
 
Hawa Shonza na Mwampamba hii aibu itawatafuna daima, na hadi sasa tuna wahesabu kama mmojawapo wa wasaliti wa haki za watz na kujaribu kuchelewesha ukombozi wa watz, ila wakamuulize kilichomtokea Savimbi na timu yake naJUA wana tumika na ccm na majambazi wa mali za umma juu wa kuisambaratisha chadema, Lakini kamwe hataweza milele bali udhalimu na unafiki hakuna sehemu yeyote imewahi kushinda haki.
Pole sana wanafiki ukweli ni kwamba chadema tutapeta daima juu ya haya yote mnayotufanyia.
Mungu daima yuko na wapenda haki.
 
hii sasa si ni habari ya zamani sana kuhusu hizi tuhuma ina maana hawa mtanzania ndio wameisikia leo?:nono:Charles Mulinda:nono: ina maana ni muandishi asieenda na wakati au makini wa habari za siasa na mhariri wake nae pia nae ni kichwa maji.. afu mimi labda cjaelewa hayo matusi ni yapi.... mbona hata hawajaindicate kama ni ya nguoni au!?
kaka waandishi wanakosa gani mbona wamelipoti hali halisi sasa kosa lao liko wapi.
 
“Zitto anatakiwa aache tabia ya kufunika funika mambo, ajue nimemwokoa sana katika mambo mengi, mfano mauaji ya Morogoro yaliyopangwa na Chadema yalimlenga Zitto, alikuwa atolewe kafara. Yule muuza magazeti aliyepigwa risasi Morogoro akafa, siku hiyo ilikuwa afe Zitto,” alidai Mwampamba.
Hawa vijana kweli kiboko kwa sihasa na sio siasa za kiTanzania!!Leo hii ndio nimefahamu kumbe wale Police waliomuuwa muuza magazeti pale Morogoro walikuwa PoliceChadema,na wale wale Police Chadema waliamua kumuua muuza magazeti baada ya kumkosa Mh Zitto Zuberi Kabwe ambaye ni makamu katibu mkuu Chadema,Mwampamba uko juu kaka jitahidi sana kusaidia upelezi japo kuwa ulichelewa but not so bad just try pia huenda ukaukwaa ukuu wa Wilaya kupitia Maccm.Bongo kweli mteremko yaani vibaka nao wako kwa siasa ahsanteni sana Watanganyika. LLlll llllllllll
 
Enhee Chapa chapa dengoo hadi padri anatukana sasa! au tu question credidibility ya mwandishi tuseme hakutukana aliongea maneno makali.
 
nilipoona matusi mazito nikajua sijui matusi ya nguoni kumbe ni matusi ya kawaida tu ambayo hata baba akimwona mwanae hafanyi isivyo atamwambia hivyo matusi anayajua kweli aliyeandika mada hii? , nchemba ndio anayajua matusi mazito.....
haya nayo yamo............
Nimtu aliye laanika peke yake ndiye anaweza asiyaone maneno haya kua ni matusi. Mtu mwenye nyazfa kama yake hastahili kutoa kauli kama hizi (matusi) tena kwenye vyombo vya habari.
 
is not an ishue hivi kaka kwa akili kama kweli unafuatilia mambo ya siasa zito hamjui saa nane aah hili hata mtoto humdanganyi.

Kuna kitu kinaitwa "inconsistency"...hawa jamaa waliungana na Zitto kipindi kile cha mtifuano kuwa hamjui Saa nane....leo wanakuja na hoja nyingine...its really fallacy...they cant twist us anyhow they want...
let them confuse those who blow hot and cold simultaneously!
 
Sasa, matusi ya Dr Slaa ni yepi hapo?

Kweli mkuu,sasa hawa wapuuzi hawajui kuwa kumwita mtu mpumba jina linalostahili sio tusi.hawa jamaa walijibiwa vizuri tena kwa ufasaha,kwa makusudi wanamwuliza swali lile lile la kipumbavu basi hapo mwandishi achukua sifa ya kuitwa mpumbavu!
 
huo ni upuuzi ulionona unategemea shonza na mwampanga wataongea mambo mazuri ya cdm, wakati wameingizwa chaka
 
Naanza kuwa na wasiwasi, huenda kibanda akawa ameteswa na watu wa Habari Corps anakofanyia kazai kwa sasa. Iweje Mtanzania ambako Kibanda ni bosi waje na hizi tuhuma kila siku ambazo hazina mashiko kama wanataka ku divert uchunguzi halisi.
hayo matusi ya Dr. Slaa mbona sijayaona?
Utayaona vipi nawewe umekunywa maji ya bendera?
 
Enhee Chapa chapa dengoo hadi padri anatukana sasa! au tu question credidibility ya mwandishi tuseme hakutukana aliongea maneno makali.

Mwandishi toleo lililopita alimnukuu Slaa...leo tena anamuuliza kitu alichokwisha jibiwa...it's really absurd!
 
then baada ya hapo nini toa suruhu acha kuongea vitu vepesi here we are tolking about tanzania hence yeyote anayegusa amani na usalama wa wa taifa na watu wake lazima tuwapige vita kwa nguvu zote.

Mtumishi..... yote yanayoendelea hapa nchini yapo wazi ila kwa wale ambao wameweka vibanzi kwenye macho na pamba kwenye masiko wanajifanya hawajui.
Tatizo kubwa linalotusumbua ni Kufanya kila kitu ni Siasa na Kila anayeikosoa Serikali ni Adui ambaye atakiwi kuwepo ili asilete usumbufu.Kubambika watu Kesi au tuma ili waonekane wabaya mbele ya jamii.
 
kaka kuwa muhalisia basi unayajua matusi wewe au unaleta unafiki wako hapa
:nono:yaani mpaka moyoni mwako unajua kuwa unafanya unafiki:nono:....hili gazeti ni makanjanja:nono: ilipaswa kuandika kuwa ametoa kauli kali ambazo mwanaume wa kweli yoyote angekuwa kwenye position ya docta slaa angeongea hivyo...unaf... wewe
Nimtu aliye laanika peke yake ndiye anaweza asiyaone maneno haya kua ni matusi. Mtu mwenye nyazfa kama yake hastahili kutoa kauli kama hizi (matusi) tena kwenye vyombo vya habari.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom