Dr Slaa alinitia moyo mkuu Igunga-Kashindye

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Aliyekuwa mgombea ubunge wa CDM jimbo la Igunga Joseph Kashindye amesema baada ya matokeo kutangazwa na kumpa ushindi batili mgombea wa CCM hakujua hatima yake itakuwaje.

Hata hivyo amesema Dr Slaa alimtaka kukata rufaa mara moja mahakamani kupinga ushindi wa CCM.Kashindye ameendelea kusema kuwa alisita kutokana na kwamba hakuwa na fedha.Baada ya kumueleza katibu mkuu huyo hana fedha haraharaka Dr Slaa alimjibu maneno yafuatayo'' Wewe nenda kafungue kesi kwani hiyo kesi si yako bali ni ya wananchi wa Igunga,wao ndiyo watakaoisimamia wenyewe''

Kashindye amedai baada ya maneno hayo mazito kutoka kwa mtu anayependwa na watanzania alienda kufungua kesi,na baada ya kufungua wananchi wa Igunga wameisimamia kesi yao wenyewe,wamemlisha na kumpa malazi akifuatilia kesi mjini Tabora muda wote wa kesi na kubwa zaidi wamemchangia fedha taslim sh milioni 6 hatimaye ushindi ukapatikana.
 
Aliyekuwa mgombea ubunge wa CDM jimbo la Igunga Joseph Kashindye amesema baada ya matokeo kutangazwa na kumpa ushindi batili mgombea wa CCM hakujua hatima yake itakuwaje.
Hata hivyo amesema Dr Slaa alimtaka kukata rufaa mara moja mahakamani kupinga ushindi wa CCM.Kashindye ameendelea kusema kuwa alisita kutokana na kwamba hakuwa na fedha.Baada ya kumueleza katibu mkuu huyo hana fedha haraharaka Dr Slaa alimjibu maneno yafuatayo'' Wewe nenda kafungue kesi kwani hiyo kesi si yako bali ni ya wananchi wa Igunga,wao ndiyo watakaoisimamia wenyewe''
Kashindye amedai baada ya maneno hayo mazito kutoka kwa mtu anayependwa na watanzania alienda kufungua kesi,na baada ya kufungua wananchi wa Igunga wameisimamia kesi yao wenyewe,wamemlisha na kumpa malazi muda wote wa kesi na kubwa zaidi wamemchangia fedha taslim sh milioni 6 hatimaye ushindi ukapatikana.
Sasa mtu kama huyu mwenye njaa akiingia bungeni si atapokea hongo hata la elfu kumi.
 
Kumbe alikua hana hata pa kulala? Duh ,bora wampe ubunge na yeye apate pa kuishi na kula vizuri.
 
Afadhali huyu atapokea eflu kumi kwani hiyo haiwezi kufilisi nchi. Haya magamba yaliyoshiba ya CCM yanapokea matrillioni ya shilingi na kuifilisi nchi kabisa.
 
Dk ni muadilifu sana,umaskini wetu umetokana na viongozi walafi na wendawazimu wa madaraka. Sishangai kuambiwa kwamb hakuwa na nyumba kwani hali vifaa vya ujenzi bei juu,kila kitu hakishikiki,ni bora kuwaondoa hao viongozi wa aina hiyo akina kafumu,over.
 
Akishinda ubunge kwa usalama wake bora Makinda amuwekee dreva maana jamaa amezoea kupanda mabus asije na yeye kutaka kuendesha.
 
Dk ni muadilifu sana,umaskini wetu umetokana na viongozi walafi na wendawazimu wa madaraka. Sishangai kuambiwa kwamb hakuwa na nyumba kwani hali vifaa vya ujenzi bei juu,kila kitu hakishikiki,ni bora kuwaondoa hao viongozi wa aina hiyo akina kafumu,over.
Mbona Slaa kaweza kujenga, kwani kajenga kwa makuti?
 
Kumbe alikua hana hata pa kulala? Duh ,bora wampe ubunge na yeye apate pa kuishi na kula vizuri.

Chura anapenda maji ila siyo ya motto jombaa!Ubunge ni uwakilishi wa wananchi hauna uhusiano na utajiri nyie magamba ndiyo mmeugeuza vichaka vya kuficha ufisadi wa wafanyabiashara au wenye pesa
 
Huyu lazima atawekwa kwenye tume fulani akishinda ubunge. Dau lake ni dogo sana.
 
Pamoja na kipato chote cha CDM wameshindwa hata kumsaidi mgombea wao sehemu ya kulala na gharama za kesi, eti anaambiwa awafate wananchi wamsaidie. Je gharama za kesi ya lema zinalipiwa na nani?
 
kama hakuwa na hela kwann wananchi wasimkatae wakaendelea na huyu mwenye hela? suala siyo atapokea hongo bali utendaji na utekelezaji wa ilani ya chama na pia hata pokea hongo kwani yuko na makanda, ila sasa tunacho subiri ni maendeleo ya wana Igunga na siyo kuwaza kuwa hana pa kulala,
 
Sasa mtu kama huyu mwenye njaa akiingia bungeni si atapokea hongo hata la elfu kumi.

Nitajie Kiasi cha pesa alichoingia nacho David Silinde na utaje hongo aliyopokea.NEXT TIME THINK GREAT B4.HAPO KASHINDYE[MB.MDHURUMIWA]ANAKUONESHA UMUHIMU WA KUTEGEMEA NGUVU YA UMMA.
 
Slaa akiwa Rais cement itakuwa sh. elfu 5.

bila shida inawezekana ni mipango tu hebu nambie ni kwa nini bei ya nyama ni kubwa wakati ngombe na mbuzi ni wengi sana mpaka tunashauriwa tuwapunguze?
 
Bora maskini kuwa MP kuliko kuwa na MP tajiri anayezidi kuiba mamilion na pia kupitisha hoja kwa sauti ya ndiyo hata kama hazina tija kwa watanzania ili aweze kuendelea kutafuna mali za walala hoi
 
Slaa akiwa Rais cement itakuwa sh. elfu 5.

bila shida inawezekana ni mipango tu hebu nambie ni kwa nini bei ya nyama ni kubwa wakati ngombe na mbuzi ni wengi sana mpaka tunashauriwa tuwapunguze?

Kweli kabisa inawezekana, na elimu itakuwa bure mpaka form six, huduma za afya zitakuwa bure na vifaa vyote vitapatikana mahospitali. Barabara kuu zote zitawekewa lami na mishahara ya watumishi wa umma itaboreshwa.
Halafu kodi ya vifaa vya akinamama zitafutwa na kodi za kuingiza magari zitapunguzwa. Na rushwa haitakuwepo seerikalini.
 
Kumbe alikua hana hata pa kulala? Duh ,bora wampe ubunge na yeye apate pa kuishi na kula vizuri.

Je jamaa zako ambao wana bilioni nje ya nchi huku bado wanaviita vijisenti unawaambia nini?
 
Sasa mtu kama huyu mwenye njaa akiingia bungeni si atapokea hongo hata la elfu kumi.

jk, chenge, lowasa, rostam, idrisa, mkapa, ngereja, shimbo, mramba, yona, wasira, lukuvi, a makinda, aliyeramba 1m mbunge, fedha uswisi, epa nyinyiemu, kagoda, meremeta, pori mbuga, madini, tanesco, richmond, tanroad, ticts, iptl, puma energy,mapanki, rada, ndege rais, s/wagon, pamoja na magamba etc?
 
Hizi nyimbo zilipigwa sana radio JF,we ndio unazisikia leo?
 
Back
Top Bottom