Dr. Slaa aiumiza CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa aiumiza CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, May 20, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tanzania Daima

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinadaiwa kuandaa fitina, mbinu na mikakati ya kukidhoofisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiwamo kumng’oa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

  Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa Dk. Slaa anaaminika ndiye amechangia kwa kiasi kikubwa kushamiri kwa CHADEMA na kudhoofika kwa CCM kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

  Hoja kubwa ya ufisadi na majina ya vigogo 11 wa serikali na chama tawala iliyotajwa na Dk. Slaa katika viwanja vya Mwembe Yanga vilivyopo jijini Dar es Salaam mwaka 2008 inasemekana ndiyo inayokitesa chama tawala.

  Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kitendo cha baadhi ya makada wa CCM kudakia hoja hiyo na kutaka wenzao watimuliwe ndani ya chama hicho imeleta mpasuko mkubwa na makundi yanayokinzana.

  Inadaiwa kuwa kuaminika kwa Dk. Slaa katika jamii ndiko kulikoifanya izidishe chuki na kukosa imani dhidi ya CCM na viongozi wa chama hicho wanaodaiwa kushindwa kuandaa na kuitekeleza mikakati ya kumuondoa Mtanzania kwenye lindi la umaskini.

  Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa hivi sasa CCM inamuona Dk. Slaa ni hatari kwao hasa kutokana na kiongozi huyo kutokuwapo bungeni.

  Inasemekana kutokuwapo bungeni kumemuwezesha Dk. Slaa kuzunguka maeneo mengi kuimarisha CHADEMA na kuidhoofisha CCM ambayo inayumba kila kukicha kutokana na kutafunwa na uhasama wa makundi.

  Inadaiwa baadhi ya vigogo wa CCM walikuwa wakiombea CHADEMA imteue Dk. Slaa awanie ubunge wa Arumeru Mashariki uliofanyika hivi karibuni ambao ungemfanya atumie muda mwingi kuangalia mambo ya kibunge, jimbo na hivyo kukosa muda wa kukiimarisha chama.

  Slaa anena

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Slaa alisema anajua CCM wana mbinu nyingi chafu za kumdhoofisha pamoja na CHADEMA, lakini kamwe hawataweza kuzifanikisha.

  Alisema hivi sasa akili yake imejikita katika kukiimarisha chama na ili azima ya kuing’oa CCM mwaka 2015 itimie.

  “Hao CCM wewe waache waendelee na fitina, hila na mbinu zao chafu maana muda wao wa kukaa madarakani unaelekea ukomo, CHADEMA inajiandaa kuchukua uongozi wa nchi,” alisema.

  Alipoulizwa kama haoni CCM inamtumia mbunge huyo kuivuruga CHADEMA, Dk. Slaa alikiri kuwa yawezekana, maana wana mbinu nyingi za hovyo, lakini akasisitiza kuwa hawako tayari kuruhusu migororo.

  Ampuuza Shibuda

  Dk. Slaa amesema hawezi kujibizana kwenye vyombo vya habari na Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda.

  Kauli hiyo ya Slaa imekuja siku chache baada ya Shibuda kuingia kwenye malumbano mazito na Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), kufuatia kauli yake ya kutangaza kugombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA, lakini akimwomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete awe meneja kampeni wake.

  “Kwangu mimi, Shibuda sina la kumzungumzia, tunayo mambo mengi ya msingi ya kufanya, hivyo naimarisha chama si kuendeleza malumbano kwenye vyombo vya habari, tuna taratibu zetu za vikao, atashughulikiwa huko kama kuna hoja,” alisisitiza.

  CCM yajitutumua

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alikana madai ya chama chake kumfanyia hila, fitina na mchezo mchafu Dk. Slaa na CHADEMA.

  Nape, alisema hakijampandikiza mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA) kukivuruga chama hicho.

  Alisema madai hayo ni ya kipuuzi na Shibuda ana haki ya kuwania nafasi yoyote ndani ya chama hicho.

  “Shibuda kama mwanachama ana haki yake kulinngana na katiba ya chama, hivyo wasimbague kwa kuwa anatoka Kanda ya Ziwa.

  “CHADEMA inafahamika ni chama cha Kanda ya Kaskazini na suala hili lingeibuliwa na mwanachama anayetoka yuko wala mambo yasingefika yaliyopo, hivyo CHADEMA wasitafute visingizio vya kuondoa hoja hii na kumnyima haki yake Shibuda,” alisema Nape.

  Alisema sheria za nchi zinaelekeza chama kiwe cha nchi nzima, lakini CHADEMA kimejieleza kuwa ni chama cha Kanda ya Kaskazini.

  Mkakati na Dk. Slaa

  Akizungumzia madai kuwa chama hicho kina mpango wa chinichini wa kumrudisha bungeni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, Nape alisema chama hicho hakimhitaji na iwapo CHADEMA kimemchoka kimfukuze.

  Alisema kuwa katika vikao vyao hawana muda wa kumjadili Dk. Slaa kwa kuwa Watanzania wanafahamu kuwa ni mzushi.
   
 2. K

  Kichoncho Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nape vuvuzela tu
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hata mfanyaje Magamba we hate you, Nyie ni wezi wakubwa, hamfai hata kuongoza KAYA! 2015 tukichukua nchi lazima muende mahakamani, si mliuza Loliondo mkawaona wamasai wajinga sasa subirini muone moto wetu!! M4C
   
 4. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Vuvuzela.... Tarutaru.....
   
 5. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Siku zote mi huwa nasema kuwa Nape ni MBUMBUMBU hana akili kwani anatumia propaganda zilizopitwa na wakati eti za ukanda huo ni upuuzi kwani mimi sio mtu wa kabila la kaskazini wala sijawah kuishi huko kaskazin lakin ni mwanaCDM na watu kibao huku tupo CDM, Nape ni mpuuzi sana kwani anadhan sisi ni wa miaka ile 40 ambapo kila kitu watu walikuwa wanakubali.
  Note:
  "HIKI NI KIZAZI CHA DIGITAL AMBACHO KINAJISET CHENYEWE NA WALA SIO KIZAZI CHA ANALOGY AMBACHO MPAKA KISITIWE" by Halima Mdee.
   
 6. p

  pomoni Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  inahitajika busara ya hali ya juu, shibuda aachwe amalize ubunge wake, viongozi wa chadema endeleeni kuimarisha chama achaneni na mambo ya shibuda,huu si wakati wa kuwania urais, bali ni wakati wa kutatua matatizo waliyonayo wananchi walio wengi, ambao wanaishi katika lindi kubwa la umasikini.
   
 7. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Dr. Slaa umesema vyema
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Kwani Sugu naye ni wa kask,ama Halfi katokea Arusha?
   
 9. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nape anafanya siasa za kizamani sana yani anadiriki kusema kwamba shibuda anapingwa sababu anatoka kanda ya ziwa,hivi haya maneno yatamshawisho nani,hata mtoto wa shule ya msingi hawezi kubali,propaganda za hivyo zilishapitwa na wakati
   
 10. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Slaa hana jipya...yale yale ya 2008!
   
 11. msadapadasi

  msadapadasi JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ila Nape akili yake anaijua yeye mwenyewe... anahitaji kufanyiwa maombi ya mfungo wa mnyororo...
   
 12. W

  Wakurogwa JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata Zitto alipotangaza dhamira ya urais alishambuliwa hivi hivi muwe mnakuumbuka basi.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mwenye jipya ni Yule aliyetuahidi maisha bora kila mtanzania?
   
 14. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  dawa ya mtu kama shibuda ndiyo hiyo. KUMPUUZA!
   
 15. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi nawambia ni sumu kali mno mbunge au kiongozi mwingine kutokuwapo bungeni kuliko awapo bungeni. Vingozi wa cdm wanapokua bungeni, wanakasirishwa wao. Ila wanapokua 'kitaa' wanasababisha wananchi kukasirishwa na ccm. Umeona iyoeee. Twende mbele.
   
 16. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #16
  May 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hivi mtu anapojitokeza kupambana na hoja za Shibuda umma unaweza kubaini tofauti? Dawa ni moja tu, kumpuuza na kumnyamazia. Wakati utaamua maana vuvuzela kule South zilipulizwa lakini mwisho wa siku kikombe kikanyakuliwa na Ulaya
   
 17. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nimeipenda hii move ya Dk.Slaa dhidi ya huyu shibuda
   
 18. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  mkuu mahakamani ni kuwapoteza mda watanzania, mbona ushahidi uko wazi? Hawa mafisadi tutanyonga na kuwapiga risasi hadharani, ccm ni janga la kitaifa, wamaetocost kwa mda mrefu sana, wametufukarisha kwa mda mrefu sana,
   
 19. K-killer

  K-killer Senior Member

  #19
  May 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is when you Exactly see kua Shibuda wanamtumia.Mjing* nape anapata wapi details kama hizi na guts zakumtetea Shibuda?Ni lazima wanakula sahani moja.Ila tumewashtukia,Tumpuuze Shibuda apite kama upepo!hehehehe
   
 20. Imany John

  Imany John Verified User

  #20
  May 20, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 180
  Nape kuzungumzia ukanda ndani ya cdm ni aibu,kijana gani anawaza kiupuzi kama yeye?
   
Loading...