Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Rais Shein alisema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona kuwa kila mara timu za Zanzibar zimekuwa wasindikizaji tu katika mashindano hayo, huku wageni wakiondoka na ubingwa
Alisema kuwa kitendo hicho ni dhahiri kuwa kinatia uchungu, kwa mashabiki na wapenzi wa soka Zanzibar, hivyo msimamo wake kuwa kombe hilo litaendelea kuchukuliwa na wageni basi mwakani hatii tena mguu wake katika fainali hizo
Dk Shein aliyasema hayo juzi baada ya kumaliza kufanya mazoezi maalum ya viungo kwa vikundi mbalimbali yaliofanyika kwenye uwanja wa Amani Amani
Alisema itakuwa ni jambo la faraja kuona Kombe la Mapinduzi mwaka huu linabaki Zanzibar
Alisema kuwa ni matarajio yake kuwa katika mwaliko aliopata mwaka huu wa kukabidhi zawadi katika fainali za mashindano hayo atapata moyo kuona anakabidhi kombe kwa timu ya Zanzibar
"Mwaka huu nimealikwa tena kuwa mgeni rasmi katika fainali za Kombe la Mapinduzi, hivyo naziomba klabu za Zanzibar zilibakize kombe visiwani humu na kinyume ya hapo mwaka ujao nikialikwa nitashindwa kuhudhuria".alisisitiza
Chanzo : Mwananchi