Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Mkuu Pasco naona Mh Raisi Shein ameitikia wito wako kama ulivyoagiza. Bila shaka nawe ni 'amiri jeshi' kinamna maana maagizo yako yametekelezwa haraka iwezekanavyo
 
Mkuu, kama ulifuatilia vizuri nyendo zote za mwanasheria huyu toka awali mchakato ulipoanza utakubaliana na mimi kuwa hakuwa peke yake, hili la kufutwa kazi ni amri toka kwa bosi mkuu Tanganyika, Dr. Shein hana altenative.

Kwani Dkt Shein atakokea chama kipi tena?
 
dr shein ni domo zege masikini kila anachoambiwa jibu lake ndio mzee ..ccm bara wajanja sana wanahakikisha rais wa zanzibar anachaguliwa dodoma na awe mtu wa kuendeshwa endeshwa kwa remote control.fact zanzibar ni koloni lisilo rasmi la tanganyika
 
Dah... Mkuu Pasco takaa ama kubali uko kwenye System aisee... What a coincidence!!!
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Baada ya kupitishwa kwa katiba mpya tuipendayo ya serikali mbili, watu wote wenye hoja za serikali tatu, ni watu wa hatari sana kwa taifa hili.



Na baada ya kukubaliwa, si ni ndio akafanya kituko kile cha kupiga kura ya hapana iliyohatarisha kupatikana kwa katiba yetu tuipendayo!, yaani just imagine, ungekuwa sio ule utaratibu wa "zisipo tosha zinatosheshwa!", hali ingekuwaje na watu hatari kama hawa mpaka sasa, wameachwa tuu hivi hivi!.

Kama Hamid ambaye ni shemeji kabisa wa Rais Karume, alifutwa kazi mara moja, na kutimuliwa kama mwizi toka ndani ya tukipendacho, Chama cha Mapinduzi!, sasa huyu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, yeye ni nani haswa, mpaka saa hii yuko kazini?!.


Pasco.


Usichokijua ni kama usiku wa Giza .Huna haja ya kutoka pofu.Kama unaona hii ni hoja nenda mbele zaidi Mshauri Shein amfukuze na Maalim Seif.
Hilo unalozungumzia la ushawishi eti kumwaga sumu ,tayari umwekwisha mwagika toka wamfukuze Mansoor Hamid na kwa taarifa yako bado sana,subiri Vikao vya Baraza la Wawakilishi lianze.

Ila kabla huja..bwa..bwa..ja sana rejea hii nukuu hapo chini. Hivyo Shein kuamua kumfukuza Mwanasheria ni uoga ule ule na kulinda masilahi yake binafsi na si ya wanZanzibar wengi,na hili ni suala la muda


Kura ya hapana: Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar atimuliwa


“Katika suala la Katiba, Serikali ilishatamka kwenye Baraza la Wawakilishi na hata nje ya Baraza kwamba haina msimamo. Ndiyo maana uliona misimamo ilikuwa imeachwa kwenye vyama vya siasa, mimi siyo Mwanasheria Mkuu wa chama chochote.
“Kwa hiyo kama Serikali haikuwa na msimamo kwa maana ya upande… nilipiga kura kwa kuzingatia utashi wangu na maoni yangu.”
 
Mkuu Pasco yametimia. CHAMInglady huyo yuko kambi tarajiwa urais 2015; ni kambi yenye uwezo wa kupata chochote toka srikali hii maana walishiriki kuijenga hapo mwanzo!
 
Last edited by a moderator:
dr shein ni domo zege masikini kila anachoambiwa jibu lake ndio mzee ..ccm bara wajanja sana wanahakikisha rais wa zanzibar anachaguliwa dodoma na awe mtu wa kuendeshwa endeshwa kwa remote control.fact zanzibar ni koloni lisilo rasmi la tanganyika
 
Mwanasheria gani huyo ambaye hata ethics za taaluma yake hazijui?

Ethics zipi ambazo hazitambui? Alichokifanya ndicho alicho apa kukifanya,yeye haongozwi kwa mawazo ya wanasiasa,yeye anaongozwa na taratibu za kazi yake
 
Hii ndiyo Demokrasia Tanzania... Kwa hili linatuonesha wazi viongozi wetu ni majuha pia hawana nia njema na maisha ya watanzania... kama mtu anaingiliwa kwenye UHURU wake binafsi tena wa kikatiba.

Hili lilofanya na mwenye nchi huku Zanzibar linakinzana na Sera ya utawala bora na uvunjifu wa haki za binadamu wa kuingilia Uhuru wa MTU..Tuna saini mikataba ya kimataifa ya nini bora tuishi bila misingi ya kikatiba wala hiyo mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu..bora tuishi tunajua kuwa tuna utawala wa kiimla...

Kuna maswala ya kumfukuza mtu kazi na si hili la mwanasheria wa Zanzibar alilofanyiwa maana tarehe 2.10.2014 huko bungeni Dodoma alichokifanya ni juu ya kile alichokiamini.K wa hali hii Katiba bora itapatikana ? au ndio tutapigwa virugu ili tupige kura ya ndiyo? Mungu ibariki Tanzania na tuondolee viongozi majuha.
 
Hii ndiyo Demokrasia Tanzania... Kwa hili linatuonesha wazi viongozi wetu ni majuha pia hawana nia njema na maisha ya watanzania... kama mtu anaingiliwa kwenye UHURU wake binafsi tena wa kikatiba.

Hili lilofanya na mwenye nchi huku Zanzibar linakinzana na Sera ya utawala bora na uvunjifu wa haki za binadamu wa kuingilia Uhuru wa MTU..Tuna saini mikataba ya kimataifa ya nini bora tuishi bila misingi ya kikatiba wala hiyo mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu..bora tuishi tunajua kuwa tuna utawala wa kiimla...

Kuna maswala ya kumfukuza mtu kazi na si hili la mwanasheria wa Zanzibar alilofanyiwa maana tarehe 2.10.2014 huko bungeni Dodoma alichokifanya ni juu ya kile alichokiamini.K wa hali hii Katiba bora itapatikana ? au ndio tutapigwa virugu ili tupige kura ya ndiyo? Mungu ibariki Tanzania na tuondolee viongozi majuha.

Mwambie mwanasheria wako ajifunze toka kwa MREMA. kama hukubaliani na msimamo wa serikali unayoitumikia unayatoa ya moyoni mwako na kujiudhuru hapohapo bungeni Hakutakiwa kungoja afukuzwe
 
Kaka sometimes nahisi unapenda Sana cheap credits zisizo na maana..huu mfano kila ukihitaji credibility you pull up hiyo your once in a lifetime right prediction.. True ulipatia ubashiri wako back then but kumbuka Rais John alikua waziri mwandamizi katika serikali ya jamuhuri ya TZ..ningeshangaa kama angekuwa mwalimu kule Sengerema akaja kuwa Rais au angekuwa waziri kule Congo au Burundi. So I suggest you use your journalist skills to write constructive journals zitakazosaidia jamii, Mambo ya kubashiri Mambo ambayo yako obvious waachie immatures au wapiga ramli...can you imagine an experienced soccer analyst predicting that Liverpool FC will finish in top 4 in premier League this season!!?... Ridiculous.
Mkuu Kabulala, just note the date and do your homework
P
 
Wanabodi,

Baada ya kupitishwa kwa katiba mpya tuipendayo ya serikali mbili, watu wote wenye hoja za serikali tatu, ni watu wa hatari sana kwa mustakabali wa taifa hili.

Mmoja wa watu hawa ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, huyu ni mtu hatari sana kwa mustakabali na majaaliwa ya kupitishwa kwa hii "Bora Katiba" kwa upande wa Zanzibar, hii ni kufuatia Mwanasheria huyo, kujitia kimbelembele kutetea hoja ya serikali tatu, inayolinda maslahi ya Zanzibar kwa mujibu wa mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, ambayo yameitambua rasmi Zanzibar kama ni nchi, na kulimega eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyemela na kuliita ni mipaka ya nchi ya Zanzibar kinyume kabisa cha katiba ya JMT ambayo inaitambua Zanzibar kama sii nchi, bali ni sehemu ya JMT, nchi ni Tanzania Pekee!.

Kwanza mwanasheria huyo, alipeleka hoja 17 za kuutetea ule upuuzi wa ile haramu iliyofanywa na marekebisho ya katiba ya Zanzibar, kuiita Zanzibar ni nchi, kitu ambacho kwa mujibu wa katiba katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni haramu. Kisha huyu jamaa akataka hiyo haramu kuigeuza halali, kwa kuilazimishia kwenye katiba mpya!, wajumbe makini wa kamati ya uandishi wa katiba wakiongozwa na mmoja wa viongozi waadilifu sana nchini, ambaye watu wenye husuda, wanamuonea tuu kijicho na wivu dhidi tujisenti twake, Mheshimiwa sana, Shujaa, Mtemi Chenge!, wakavitupilia mbali hivyo vipengele 17 haramu ndani ya katiba ya Zanzibar, visiingizwe kwenye rasimu ya katiba mpya!. Mwanasheria huyo hatari, aliyetaka kuvichomekea, ili kuigeuza haramu hiyo kuwa halali!, alikasirika sana baada ya kugonga mwamba.

Baada ya hilo kushindikana, kwanza akajitoa kwenye kamati ya uandishi wa katiba, akabakia Dodoma akiranda randa tuu!, ulipofika wakati wa kupiga kura!, kwanza alisusa kupiga kura ile siku ya kwanza ili hali yuko Dodoma, siku ya pili pia akasusa!, ila kabla ya upigaji kura kufungwa rasmi, sijui shetani gani, akamtembelea, mara akaingia bungeni mbio mbio na kuomba kupiga kura ya wazi!, Muungwana Sitta, akamkubalia!, ningekuwa mimi, kamwe nisingemkubalia!.

Na baada ya kukubaliwa, si ni ndio akafanya kituko kile cha kupiga kura ya hapana iliyohatarisha kupatikana kwa katiba yetu tuipendayo!, yaani just imagine, ungekuwa sio ule utaratibu wa "zisipo tosha zinatosheshwa!", hali ingekuwaje na watu hatari kama hawa mpaka sasa, wameachwa tuu hivi hivi?!.

Kama Hamid ambaye ni shemeji kabisa wa Rais Karume, alifutwa kazi mara moja, na kutimuliwa kama mwizi toka ndani ya tukipendacho, Chama chetu cha Mapinduzi!, sasa huyu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, yeye ni nani haswa, mpaka saa hii yuko kazini?!.

Kwa kadri anayoendelea kubaki kazini, ndio alivyo na chances kubwa zaidi kumwaga sumu kama hii, dhidi ya hii katiba mpya tuipendayo!, namshauri, rais Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein, amfute kazi mara moja, Mwanasheria Mkuu huyu, akaungane rasmi na kile chama cha kutetea serikali, tatu zinazotaka kutuvunjia huu muungano wetu adhimu!.

Kwa msiozijua hoja za sumu kwa serikali mbili, za Mwanasheria huyu Mkuu wa Zanzibar,

Msikilize hapa!.


Kamati ya Maridhiano Six:MWANASHERIA OTHMAN MASOUD AUCHAMBUA MUUNGANO NA KATIBA MPYA
Paskali

Kuna watu wanaitwa ni wamwaga sumu. Niliwahi kutoa angalizo kuhusu mmwaga sumu huyu, sasa ndio yumo serikali, hivyo kufikia 2025, kama hatadhibitiwa kabla, uchaguzi wa 2025 Zanzibar kuna kazi!.
P
 
Wanabodi,

Baada ya kupitishwa kwa katiba mpya tuipendayo ya serikali mbili, watu wote wenye hoja za serikali tatu, ni watu wa hatari sana kwa mustakabali mwema wa taifa hili.

Mmoja wa watu hawa ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, huyu ni mtu hatari sana kwa mustakabali mwema wa nchi yetu na majaaliwa ya kupitishwa kwa hii "Bora Katiba" kwa upande wa Zanzibar, hii ni kufuatia Mwanasheria huyo, kutetea hoja ya serikali tatu, inayolinda maslahi ya Zanzibar kwa mujibu wa mabadiliko ya kumi ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, ambayo yameitambua rasmi Zanzibar kama ni nchi, na kulimega eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyemela na kuliita ni mipaka ya nchi ya Zanzibar kinyume kabisa cha katiba ya JMT ambayo inaitambua Zanzibar kama sii nchi, bali ni sehemu ya JMT, nchi ni Tanzania Pekee!.

Paskali
Kumbe kama kuna mambo makubwa aliyasema na yakatokea
Kumbuka hata biblia imesema Yesu atarudi, hadi sasa ni miaka 2000+ hajaonekana ila bado watu wanaamini na kuifuata.

Sijui wewe unayepi ya maana umeyasema na yakatokea yote hapo hapo? Pascal Mayalla
Mkuu Nzwangendaba, kwanza hongera kwa jina zuri, linafanana na yule kiongozi wa Wangoni kutoka Africa Kusini kuja kuhamia Tanzania, Zongendamba.

Karibu mitaa hii, angalia tuu tarehe ya bandiko ni la lini na nini kilikuja kutokea.
P
 
Back
Top Bottom