Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Baraza la Mawaziri ametumwa kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ziara nchini Comoro.
Ikumbukwe Mambo ya nje, Mahusiano ya Kimataifa na Kikanda ni suala la Muungano. Rais wa Serikali ya Mapinduzi anatakiwa kugusa masuala ya Zanzibar tu, hagusi ya Muungano wala ya Tanganyika, kama ambavyo Magufuli hagusi masuala ya Zanzibar.
Iweje Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiuke kiapo chake cha kulinda Katiba ya nchi kwa kukasimu madaraka yake kwa mtu asiye na mamlaka ya kupewa majukumu hayo?
===========
Sahihisho. Dk Shein hakutumwa kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ziara nchini Comoro.
Dk.Shein amekwenda Comoro kuiwakilisha Tanzania katika sherehe za kumuapisha Rais wa visiwa hivyo, ambavyo vina uhusiano mkubwa, wa karibu na wa asili na Zanzibar.
Sherehe hizo zinafanyika wakati huu na mara tu baada ya sherehe atarudi Zanzibar mchana huu!