Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Chuo cha mafunzo kiliasisiwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Karume baada ya kulifunga Gereza kuu Zanzibar na kuwapa msamaha wafungwa wote, mahabusu na kuzifuta kesi zote zilioko polisi na mahakamani.
Katika sherehe hiyo ya kufana ilifanyika uwanja wa Amaan mbele ya wafungwa wote. Mzee Karume mbali na kuwasamehe pia aliwapa pesa na vifaa vya kazi ya kuanzia maisha mapya uraiani.
Sababu Kuu iliotolewa ni kuwa hakuna mantiki ya kuwa na wafungwa wananchi kwenye nchi huru
Sababu pinzani zinadai kuwa , hatua ya kulifunga gereza hilo ni hila za kisiasa za "kutakatisha" tuhuma za uhalifu wa ubakaji uliofanywa na " vijana maarufu wasiojuulikana" uliopelekea kifo cha msichana na maiti yake kutupwa kwenye mtaro.
Chuo cha mafunzo kilichoanzishwa kilisimamiwa na Mwalimu Mkuu Mandera (a.k.a Bamkwe) kilikuja kuwa kitovu cha uonevu, utesaji na mauaji na kupoteza heshima na muelekeo wake kama chuo. Mwanafunzi mashuhuri alikuwa Bibi Titi Mohammed na wenzake pale walipoletwa Zanzibar kuja " kuhifadhiwa"
Kwa vile chuo hiki kilikosa " mitaala rasmi" hakikuweza kukuza taaluma, vinginevyo sasa kilikuwa kiwe Chuo Kikuu cha Mafunzo.
Kwavile sababu za msingi za kuundwa chuo hicho sasa hazipo au zimedoda kutokana na kinavyoendeshwa , na mabadiliko ya sheria na utawala bora, ni bora tusijitenge na na jumuiya za kimataifa/madola kuwa nchi isiokuwa na Gereza
Aidha hata hao waliokuwa watuhumiwa hivi sasa inasemekana wanashikilia madaraka makubwa serikalini!
Mpendwa Dr. Shein turejeshee Magereza ZANZIBAR