Sophist
Platinum Member
- Mar 26, 2009
- 4,486
- 3,407
Wandugu,
Ninapenda tujadili kauli ya Rasi wa Zanzibar, Dr. Mohamed Shein aliyoitoa mara baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais JPM kumpatia nafasi ya kutoa kauli yake wakati wa kumalizia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, leo March 12, mjini Dodoma.
Alisema, na hapa ninamnukuu, "Changamoto zitaendelea kuwepo licha ya kubadilisha Katiba" tafsiri ni ya kwangu.
Binafsi nimeona kauli hii kama ujumbe kuwa haamini/hakubaliani na kubadilisha Katiba ikiwa ni mkakati wa kuimarisha na kuongeza ufanisi katika chama chao.
Tunaweza kujiuliza maswali yafuatayo:-

- Je, Dr. Shein hakushiriki katika mchakato uliohitimishwa katika mkutano wa leo?
- Je, Dr. Shein alishiriki mchakato husika lakini mawazo yake hayakukubaliwa na wenzake naye akabaki na kinyongo?
- Je, Dr. Shein amehamishia mapambano/vita (battle) ya tishio la Zanzibar kukatiwa umeme (agizo la JPM) katika mkutano wa leo?
- Je, kauli ya Dr. Shein ni aina nyingine ya hangover ya kutoridhishwa na mfumo wa Muungano wa serikali 2?
- Je, Dr. Shein yuko indifferent katika mabadiliko ya Katiba ya chama chao?
- Kuna kitu gani hasa kilichomfanya Dr. Shein kutoa kauli hiyo?