Dr. Shein afuturisha wananchi wa mkanyageni pemba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika futari na wananchi wazee wa kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba, aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni.

Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya kiislamu wa Kijiji cha Mkanyageni na vitongoji vyake, wakifutari pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wazee,pamoja na wananchi wa kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba,baada ya kufutari pamoja na wananchi hao katika futari maalum aliyowaandalia katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni.

Picha na Ramadhan Othman/IKULU ZANZIBAR :clap2::first:​



5481.jpg aaq.jpg ax.jpg
 
Bora Dr Shein kafuturisha watu kijijini. Amani iwe nanyi wapemba nduguzetuni, siye huku nafisadiwa ka nini.
Hatuna umeme, maji hakuna, mafuta ndo hivyo yameshakuwa siasa. Sijasikia kama Zanzibar haya matatizo yapo!! Vijana wetu wakienda shuleni wanaishia kucheza na kutongozana kwenye michongoma tu huku elimu ikishuka kwa kasi ya mwanga. Walimu wa shule ya msingi ndo walimu wa shule za kata (maajabu lakini ndo ukweli niliokutana nao). Ukienda hospitali unaonana na Dr. kumbe ni medical Assistant, unapigwa dawa ya mseto wakati una typhoid, usiombe jamani. Ukipanda daladala kila mtu kanuna, anasubiri mtu alianzishe lakini hakuna wa kulianzisha.
 
Back
Top Bottom