Dkt. Rioba wa TBC ataka kupigana na Gerald Hando wa E-FM kwa kuambiwa TBC imemshinda

Ukitaka kujua kijana wako ni rijali mtafutie mwana-mwali alale nae usione ndevu ukajua damu inashuka kichwa cha chini.
Dr. Ryoba amekojolea CV yake vibaya mno yaani TBC ambayo inaendeshwa na kodi zetu imeporomoka vibaya mno.
 
Pale ulevu unapomkolea mtu hupata ujasiri wa kumpa mtu makavu live!
Hata hivyo Ryoba dont take it serious, jamaa alilewa...
 
TBC ikikuwa enzi za Tido muhando. Kingine kichoiharibia TBC ni kuwa kama televisheni ya chama tawala. Wasiwe biased. Kituo kinaweza kikawa na ubora hafifu wa picha na sauti ila habari zake zikawa kivutio tu. Dr Ryoba please fanyia kazi hili swala mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Habari Tanzania TBC, Dkt. AYOUB RYOBA kama siyo watu kumshika na kuwaamua, nusura apigane na Mtangazaji wa kituo cha Redio cha EFM Gerald Hando.

Tukio hilo lilitokea katika Bar ya LILLY'S iliyoko Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya Gerad Hando kumwambia RYOBA kuwa ameshindwa kabisa kulifanya Shirika la TBC lionekane linaongozwa na Mkurugenzi mwenye elimu ya kutosha Kabisa ya kiwango cha Phd na aliyefundisha wana taaluma mbalimbali wa habari.

Baada ya ugomvi huo kuzuiwa na watu waliokuwepo karibu, DR.Ryoba aliondoka kuelekea kwenye gari lake ambapo ilitafsiriwa kuwa alikuwa anakwenda kuchukua Bastola.

Aidha Bosi huyo wa TBC alisikika akisema kuw atamshughulikia Gerald Hando na hakuna wa kumfanya lolote.
....hawa wote wa huko huko, watu wanaoenda bar na mapanga ya kugetana !
 
Sasa ukiambiwa ukweli si ndii motivation ya kujipanga.. Mm nafurahi sana mtu anaponambia ukweli ambao naona yupo sahihi, najipanga kufanya bora aje anisifie.
 
Kwamba kama habari haina picha ni ya uongo? Na ikiwa na picha, hata kama ni ya uongo, inakuwa ya kweli?

Usinijazie maneno mdomoni... kujifikiria unazooooo eeeeh

Weka zionekane kwanza mengine yafate.. tukio lote hilo watu na simu zao wakaminya tu...mmmh
 
Hivi unapomchezea Mkurya tena kama Dkt. Ayub Ryoba aliye katika Ubora wake uliotukuka kabisa unategemea nini? Nawalaumu sana hao waliomshika Ryoba kwani ingependeza mno kama angempa kidogo dozi Gerald Hando ili ajue kwamba Wanaume wa Mkoa wa Mara ( Musoma ) huwa hatupendi Shobo tena hasa kutoka kwa Vitoto kama Yeye kisha akawasimulie wenzake. Hivi huyo Hando hashangai tu ni kwanini hawa akina Wahaya, Waha, Wanyiramba, Wanyaturu na Warangi wanatuogopa sana Watu wa Musoma ( Mara ) hadi wanatuozesha tu wenyewe Dada zao ili tusiwape Vipondo?

Chezeeni kote ila siyo Mkoani Mara ( Musoma ). Ha ha ha ha ha ha ha.....kama nawaona vile hao Watani zangu wapendwa niliowataja hapo juu watakavyonishambulia humu!
Mkuu heshima kwako,

Hivi kutoka Mara nayo ni sifaeehh.,...
 
Hivi kila Mtu akiamua kutiririka na kuserereka kwa Kilugha chao tutaelewana kweli humu? Umeogopa nini kuandika tu kwa Kiswahili ili Mimi na wengineo tukuelewe? au unadhani nitakutukana / nitakutusi Mkuu? Tayari nimeshaahidi humu JamiiForums kuwa sitokuja kumtukana tena Member yoyote kama ilivyokuwa mwanzo sana sana nitakuwa tu natania kwa kuchomekea yale maneno yangu ya Kiutani ila siyo Kumtukana Yoyote humu hivyo Wewe kuwa huru na nimekuruhusu unitukane au mnitukane muwezavyo ila Mimi sitorudishia au kuwatukana.

Hivyo kwa hayo machache nakuomba unitafsirie hicho ulichokiandika hapo ili nami pamoja na Wenzangu bila kuwasahau pia na Moderators wote wa JF nao waweze kujua / kufaidika nacho. Ni matumaini yangu ya dhati na makubwa kuwa utaonyesha ushirikiano wako katika hili ombi langu lenye mantiki na mashiko Kwako.

Akhsante.
Nilikua nakutania tu kinyumbani mtani (Kigoma)
 
Back
Top Bottom