MWENYEKITI wa Chama cha Wanawake Madaktari (Mewata), Dk. Marina Njelekela juzi alitunukiwa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Dk. Njelekela ambaye pia alishinda katika kipengele cha Mwanamke Bora katika Sekta ya Afya, katika nafasi hiyo alishindana na Dk. Mwale Malecela na Salome Yakieli.
Tuzo hizo ziliandaliwa na kutolewa na Kampuni ya matangazo na uhusiano wa umma, Frontline ambapo wanawake 24 walishindania tuzo hizo kupitia sekta mbalimbali.
Akizungumzia ushindi huo muda mfupi baada ya kukabidhiwa tuzo yake na Meneja wa Mradi wa Wanawake katika Umoja wa Mataifa hapa nchini, Anna Collins- Falk, Dk. Njelekela alisema tuzo hiyo imemuongezea moyo wa kutoa huduma ya afya kwa wananchi.
Kwa walio Jitokeza...ndio bora sio bora kwa wote...tupe na list za wengine walio shindanishwa tuone...vigezo na masharti kuzingatiwa.
I agree with you....hiyo title ni kubwa sana.....ningefurahi kujua alioshindanishwa nao na amefanya nini na kwa impact ya wangapi nchi hii?
Ishakuwa kwamba mtu akishateuliwa na Rais....ni mtoto wa fulani....anajuana na watu fulani basi anaweza pewa title yeyote......!!
hivi huwa ni vigezo gani vinatumika kumpata?
Hilo ndilo swali la msingi...Frontline ya Nancy Sumari na Irene Kiwia??? aya bwana.....
Hongera sana Dr....keep up the good work!
Trust me...Dr....bigwa wapo kibao...busy na kazi zao.....huyu profile yake kwa kweli inabidi iwekew hapa,hatuwezi tengua...kwanza hata frontline yenyewe hawa warembo ndio viongozi..sasa unategemea kuweza kumcredit Dr.Bigwa wa kisukari Mhimbili...kwanza hawezi hata jitokeza..Nawafahamu wengi tu wako busy kuhudumia wagonjwa..hawalali...akitoka kazini Muhimbili,anafundisha,anatibu at the same time asoma tena...achilia mbali kwenda hospitali zingine kutoka support.