Fabian the Jr
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 756
- 743
Binafsi nmefurahishwa sana na juhudi anazofanya huyu waziri katika kuhakikisha anarudisha nidhamu na ubora wa elimu yetu hapa Tanzania. Nasema haya kwa mambo makuu mawili aliyoyasimamia huyu mama:
1. Suala la wanafunzi wa St Joseph ambao walikuwa wanasoma degree huku wakiwa wametoka direct form 4 ambako pia hawakuwa na sifa hata za kuchukua cheti.
Inasadikika kwamba takribani wanafunzi 480 walikuwa wanaendelea na masomo yao ya degree katika chuo hicho. Hii ni dhahiri kwamba baaada ya miaka miwili ijayo tungekuuwa na waalimu ambao hawana sifa kabisa za kutufundishia watoto wetu.
Waziri kalisimaia suala hili na kwakweli anastahili pongezi na tumuunge mkono katika hili.
2. Suala la wanafunzi takribani 8000 wa special diploma ya ualimu UDOM. Nilishawahi kuhoji kuhusu uhalali wa hawa wanafunzi ambao walikuwa ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na wengi wao wakiwa na ufaulu hafifu wa div 3 (Tena ndo zilee za GPA). Program hii ilianzishwa kwa agizo la Raisi aliyepita ikiwa ni njia ya kupunguza uhaba wa waalimu wa science mashuleni.
Ni kweli kabisa kwa idadi yao wangeweza kuziba pengo la waalimu wa science mashuleni, lakini Je, ubora wao ukoje? wanastahili kweli na wanao uwezo wa kufundisha hesabu, physics na chemistry kwa ngazi ya o-level na mwanafunzi akaelewa?.
Ni dhahiri tulikuwa tunaandaa vijana weng wasio kuwa na sifa kwa ajili ya kuwafundisha vijana wetu. Naamini kwa waalimu wa haya masomo na yeyote aliyesoma PCM advance ataelewa ninachosema,
Ingawa suala hili bado lipo kwenye mjadala, ni dhahiri kuwa Waziri na wizara nzima wanalitafakari kwa makini jambo hili. Kwa ushauri wangu kwa kuwa vijana hawa wamepotezewa muda wao mwingi, wangesambazwa kwenye vyuo vya ualimu vilivyopo nchini kwetu wakamalizia masomo yao, halafu wakasambazwa kwenye shule zetu za msingi. Huko wangekuwa na ufanisi mkubwa sana kuliko kwenye shule za sekondari.
Tumuunge mkono waziri Ndalichako na serikali kwa ujumla kwa juhudi hizi wanazofanya za kufufua elimu yetu.