Makoye Matale
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 6,490
- 2,104
Duh kweli CCM wababe sana Dr wetu ndio hivyo tena kwishey.
Nchimbi hakugombea ubunge kule Songea. Alitoka mbio kupinga maamuzi ya kamati kuu ya CCM kumpitisha Lowassa. Hakuhama chama. Akarudi kuiomba kamati kuu impitishe awe mgombea uspika, ikambwaga. Nini hatma yake? Je, ndio amefika ukingoni katika siasa?
Cha kujiuliza pia, ni sahihi kupinga maamuzi ya taasisi au chama chako hadharani? Anaonewa au ameponzwa na upofu wa kukurupuka?Ya Nchimbi; CCM na matumizi mabaya ya Vijana!. ''Ndiyo mzee''
Nchimbi anatakiwa kujifunza jambo namshauri ajiunge na Mhe.Zitto na kabla ya kufanya hivyo amtembelee Malema S.A!
cc Juliana Shonza
Atateuliwa kuwa mkuu wa mkoa au Balozi
Kama kuna kitu cha kijinga ambacho Nchimbi alifanya ni kupinga maamuzi ya CC hadharani.Nchimbi hakugombea ubunge kule Songea. Alitoka mbio kupinga maamuzi ya kamati kuu ya CCM kumpitisha Lowassa. Hakuhama chama. Akarudi kuiomba kamati kuu impitishe awe mgombea uspika, ikambwaga. Nini hatma yake? Je, ndio amefika ukingoni katika siasa?
Cha kujiuliza pia, ni sahihi kupinga maamuzi ya taasisi au chama chako hadharani? Anaonewa au ameponzwa na upofu wa kukurupuka?
ccm is the dying horse
Soon tutamsahau kwenye ulingo Wa siasa mbaya zaidi anasahaulika akiwa bado kijana..
hawa ndio waliosemwa wanafiki, mchana wako CCM usiku wako UKAWA.Hawezi kuteuliwa na Magufuli maana alionesha wazi kwa hisia kuwa yuko na Lowassa
Kimtazamo wa kiimani unaweza kusema hivyo. Kumbuka kwamba usipoweka misingi ya kinidhamu katika Taasisi kila mtu atakurupuka na kuropoka na heshima itapotea. Kila Taasisi ambayo ni imara ina njia na taratibu zake za kutatua matatizo. Ninachoweza kukiona ni kwamba CCM wamekuwa waoga saana wa kufukuza watu uanachama, huyu atawagharimu muda si mrefu. Inatakiwa Taasisi kwanza na si jina mtu. Ningependa nikutolee mfano wa kwenye mpira kama ni mfuatiliaji; Meneja aliyepita wa Manchester United alikuwa na falsafa kwamba hakuna mtu mkubwa kuliko klabu. David Beckham alivyoanza kupaa akamsogezea Madrid, vivyo hivyo kwa Ryan Giggs. Baadae Man Utd waliendelea kupata mafanikio. Isitokee mtu mmoja akawa mkubwa kuliko Taasisi, huo ni udhaifu.Kusema haki haikutumika ndani ya kamati kuu ndicho kinachomla Nchimbi! Visasi vya kijinga tena wakubwa ni vibaya na ni kiburi na machukizo hata kwa mola. na watoto wao watakuja kufanyiwa hivyo hivyo kwani ni laana!
Atateuliwa kuwa mkuu wa mkoa au Balozi
ccm is the dying horse
Huo mstari nimeanza kuusikia muda mrefu sana...lakini post-2015 inaonekana chama kinaongezeka umaarufu