Dr. Nchimbi RCO huyu unamfanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Nchimbi RCO huyu unamfanyaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kassim Awadh, Oct 8, 2012.

 1. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  "WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ametengua uamuzi wa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala (RCO) Duwani Nyanda, wa kujichukulia sheria mkononi na kutoa uamuzi ambao ulipaswa utolewe na mahakama.RCO Nyanda alijichukuli asheria mkononi kwa kutoa uamuzi nje ya mahakama kuhusiana na mgogoro wa umiliki wa gari aina ya Suzuki Escudo lenye namba za usajili T708 BZS, baina ya mfanyabiashara Said Kachenje, na mkazi wa Zanzibar, Mohamed Ismail.
  Gari hilo ambalo lilinunuliwa na Kachenje April mwaka huu, lilikamatwa na askari Polisi, kwa madai kuwa ni la wizi na kwamba ni mali ya Ismail.
  Kachenje ambaye anadai kuwa ana nyaraka zote halisi, licha ya kufunguliwa kesi ya wizi, hata hivyo baadaye RCO Nyanda aliamua kumkabidhi Ismail gari hilo, bila kufikisha kesi hiyo mahakamani.
  Hata hivyo, Waziri Nchimbi ameamuru gari hilo likamatwe na kurejeshwa katika kituo cha polisi wakati taratibu za kisheria zikifanyika kulipeleka suala hilo mahakamani ambayo ndio itakayoamua umiliki halali wa gari hilo.
  Katika barua yake ya Septemba 20, 2012 kwenda kwa Kachenje, iliyosainiwa na Kaimu Katibu wa Waziri, Nelson Kaminyoge, Waziri Nchimbi amesema kuwa uamuazi huo aliouchukua RCO haukuwa sahihi kwani ulipaswa kutolewa na Mahakama na si Polisi.
  “Kwa msingi huo, gari hiyo imeamriwa ikamatwe na kurudishwa kituo cha Polisi wakati taratibu za kisheria zikiendelea ili kulipeleka suala hilo mahakamani,” inasomeka sehemu ya barua ya Waziri Nchimbi.
  Waziri Nchimbi alilazimika kuingilia kati suala hilo, baada ya Kachenje kumwandikia barua ya malalamiko, akidai kuwa polisi wanafanya mpango wa kumdhulumu haki yake.
  Katika barua yake ya malalamiko kwenda kwa Waziri, Kachenje alidai kuwa alilinunua gari hilo April 19, 2012, kutoka kwa Suleiman Haji, baada ya kukutanishwa na madalali wawili, aliowataja kwa jina moja moja la Hamisi na Almasi.
  Alidai kuwa kabla ya kuingia mkataba wa ununuzi wa gari hilo alifanya uchunguzi wa umiliki wa gari hilo kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo alijiridhisha kuwa gari hilo limesajiliwa kwa jina la Suleiman Haji.
  “Tulifanya mkataba wa mauziano mbele ya Wakili Margaret Mngumi, na malipo na saini zote zilitiwa mbele yake kama Kamishna wa Viapo,” alidai Kachenje katika barua hiyo.
  Aliendelea kudai kuwa wakati akiendelea kulitumia gari hilo huku akitafuta mteja wa kulinunua, April 24, 2012 alikamatwa na askari polisi kwa maelezo kuwa gari hilo ni la wizi.
  Alidai kuwa aliwekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa muda wa siku tatu hadi alipowekewa dhamana na nduguzake, lakini akafunguliwa kesi na kuambiwa kuwa uchunguzi ulikuwa ukiendelea.
  Alidai kuwa Julai 24, 2012 alipigiwa simu na askari aliyejitambulisha kwa cheo na jina la Inspekta Benjamini, akimtaka apeleke nyaraka halisi za gari hilo.
  Hata hivyo, alidai kuwa alipeleka vivuli vya nyaraka hizo na akamwambia askari huyo kuwa nyaraka halisi ziko kwa wakili wake na kwamba alipotaka kujua sababu ya kutakiwa kupeleka nyaraka hizo, alimbiwa kuwa zinatakiwa ili jalada lipekekwe kwa mwanasheria wa Serikali.
  “Nilipata wasiwasi kuwa hapa kuna mchezo unataka kuchezwa dhidi yangu. Mheshimiwa Waziri, hofu yangu ilitimia tarehe 19 Julai, 2012, pale ambapo nilipita Kituo cha Polisi Kati na kukuta gari halipo,” alidai.
  Alidai kuwa baada ya kufuatilia, RCO Nyanda alimweleza kuwa gari hilo amemkabidhi mlalamikaji, baada ya kukamilisha upelelezi na kugundua kuwa ni mali yake halali."

  My take: Kwa utaratibu wa ccm wa kulindana sitashangaa inshu hii ikafa bila RCO huyu kuchukuliwa hatua zozote!
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hata hivyo uamuzi wa Nchimbi naupongeza sana.
  Sasa ni wakati wa kuonyesha makucha yake kwa kumuwajibisha RCO
   
Loading...