MSAMI KIZIMBANI MAHAKAMA KUU
* Adaiwa sh.Bil.5/= kumchafua Mwakyembe kwa makusudi,
* Kutinga Mahakamani Alhamisi ijayo.
Mwandishi na "Mhariri wa Habari" Mussa Mkama, wamiliki na wachapishaji wa DIRA YA MTANZANIA wamefikishwa Mahakama Kuu Dar es Salaam wakidaiwa mmoja mmoja na kwa ujumla wao kumlipa Dk. Harrison Mwakyembe sh. Bil.5 kwa madhara aliyopata kutokana na taarifa za gazeti hilo zinazodaiwa za uongo na zilizolengwa kumchafua kiongozi huyo kwa makusudi.
Dk. Mwakyembe ambaye vilevile ni mwanasheria wa siku nyingi, Mbunge wa Kyela na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, anawakilishwa katika shauri hili na mawakili wawili nguli wa Dar es Salaam, Mpale Mpoki na Alex Mgongolwa.
Katika maombi yake yaliyowasilishwa Masjala Kuu ya Mahakama Kuu Dar es Salaam wiki iliyopita, Dk. Mwakyembe ameiomba Mahakama Kuu kuwa mbali na kuwaamuru walalamikiwa wamwombe radhi, iwatake wamlipe sh. Bil.5 kwa kumchafua kwa makusudi kwa wiki mbili mfululizo bila kujali madhara ya hatua yao.
Shauri hili lililopewa namba 134/2016 linatajwa kwa mara ya kwanza mahakamani Almamisi wiki hii ambapo mmiliki wa gazeti hilo Alex Msami na wenzake wanategemewa kuieleza Mahakama Kuu mpangilio wao wa kujibu madai hayo.
Alipopigiwa simu jana kuelezea mwelekeo wa madai yake, Dk. Mwakyembe alisema mashauri huendeshwa mahakamani na siyo magazetini na kuelekeza tuongee na mawakili wake.
"Sina la kuficha na wala sina kinyongo na tasnia ya habari. Dhamira yangu ni njema - kuendeleza weledi na kuiokoa tasnia ya habari isitekwe na vishoka", aliongezea bila kufafanua.