dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 24,688
- 56,423
Wakuu Salaam.
Akijitetea mbele ya Bunge kwa nini hastahili kulaumiwa au kufukuzwa uwaziri wake kwa kadhia iliyotokana na Operesheni Tokomeza, pamoja na mambo mengine ikiwamo kutumia nukuu za kidini, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dr. Mathayo David Mathayo alitumia muda mwingi kuilamu "Serikali" kwa kushindwa kutoa mafungu ya kutosha kwa wizara yake hali ambayo iliifanya wizara kushindwa kutimiza malengo mengi ambayo yaliripotiwa na Kamati ya Lembeli kama chanzo kilichosababisha madhila kwa wananchi wakati wa Operesheni Tokomeza. Ikumbukwe baadhi ya madhila hayo ni pamoja na:-
(i) Wananchi kuzinishwa na miti (kidogo hili linanipa utata).
(ii) Wananchi kuuwawa na walioendesha operesheni hiyo.
(iii) Ndugu kulazimishwa kuingiliana hadharani na mafedhuli walioendesha operesheni husika.
(iv) Wananchi kuporwa mali zao - mifugo, mazao, fedha, n.k.
Tunaomba wataalamu wa Katiba na Sayansi ya Siasa watusaidie kwanza Serikali ni nini; pili kama waziri ni au sio sehemu ya Serikali na tatu kama ilikuwa sahihi kwa Waziri kuilamu Serikali. Waziri alipaswa kufanya nini zaidi ya aliyoyafanya (sababu alizozitoa wakati akijitetea)? Je, utetezi wake ulikuwa na hoja au pumba? Kama alikuwa na hoja ilikuwa sahihi kwa mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wake kwa mtindo ule?