Dr. Mashinji kwa haya hufai kuwa Katibu Mkuu CHADEMA

Enzymes

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
4,332
3,008
Samahani kama nitakukosea ila ukweli lazima ni useme. Naomba nieleweke mimi siyo mfuasi wa chama chochote bali ni.mfuasi wa kiongizi bora toka chama chochote.

Nimejikita katika vipengele vifuatavyo:-

1. HOJA
Mimi binafsi nimefuatilia uongozi wako toka mwanzo, kwa sasa nimeridhika kabisa bila shaka kuwa hufai kuwa Katibu mkuu wa chama kinacho itafuta dola. CHAMA kimekosa ubunifu. CHADEMA imekosa hoja za msingi kupambana na serikali. Serikali imekuwa ikionekana njema licha ya maovu kukithiri. Hoja za msingi zimebaki kwa T. Lissu pekee huku akiatarisha maisha yake. Wekezeni katika kutafuta Scandal mbalimbali za CCM au serikali ili muwe Popular. Chama ni uwekezaji. Wafundisheni wabunge wenu jinsi ya kujenga hoja. Pia wapatieni HINTS zenye ushahidi tosha mf CAG REPORTS.

2. NIDHAMU NDANI YA CHAMA

Nidhahiri ndani ya chama kuna kutokuelewana au mpasuko mkubwa sana. Chama ni mali wa watu na si taasisi. Mf. Saed Kubenea kupitia Magazeti yake ya MAWIO/MWANAHALISI aliwahi kuandika kuwa Ben Saanane ameonekana mitaani na atafuta kiki tu wala hajatekwa, hii ni ishara mbaya sana ndani ya chama. Mimi binafsi natambua na nakiri mchango mkubwa sana wa SAED KUBENEA kuichamba CCM na kuineza CHADEMA toka miaka ya 2000 hadi kufikia kumwagiwa Tindikali. kusameana ni jambo la mhimu sana.

Kuna vijana kama MALISA GJ na timu yake wamekuwa wakiposti hoja au vitu vya hovyo hovyo Fb na mitandao mbalimbali dhidi ya Wabunge (hasa Saed Kubenea) au wanachama wenzao. Hujawahi kuwa kemea ndio maana wanaendelea. Hii ni dhahiri umeshindwa kudhibiti nidhamu ndani ya chama. Jenga chama kama taasisi na si SACCOS ya watu. Vijana wadogo kama Malisa na wengine wote wadhibitiwe mapema.

3. UCHAGUZI EALA

Uchaguzi huu ni dhahiri wewe kweli ni Daktari wa binadamu siyo wa siasa. CCM ni mabingwa wa hujuma, wanafiki, nk lakini hilo ulijidai hulijui!! (Hawa wanacheka na wewe dk1; dk inayo fuata wana kucheka-mpuuzi yule.

Binafsi kwa mtizamo wangu ungepeleka majina 3 tu.
1. EZEKIAH WENJE
2. LAWRENCE KEGO MASHA
3. JOSEPHINE L.

Namuondoa Pamela coz hafai na hana sifa kuwa Mbunge EALA. Alipaswa asubiri hadi 2020 awanie viti maalum Tz au awanie Jimboni. Uwezo wake bado ni mdogo na English hajui ikumbukwe lugha katika EALA ni English. Hapa nahisi kuna mahusiano yapo nyuma ya huyu binti. Pia kuna kampeni kubwa sana ilipigwa ndani ya chama kumpitisha. Kwa style hii vijana wazuri watazidi kujiondoa na kurudi CCM. Yaani mnawakatisha tamaa.

Nitumie nafasi hii kuishauri CHADEMA kuwa Makini sana na Dr. Mashinji. Huyu na JPM ni kanda moja, kamwe hawezi kumtupa. Itakula kwenu endeleeni kusinzia usingizi wa Nyangumi mtashituka 2020 hii hapa mnapigwa KO.

Mungu ibariki Tz.
 
Kwa taarifa yako asilimia 90 ya misimamo ya Dr Slaa ilitokana na juhudi binafsi za Tundu Lissu. Hilo jina unalichukulia kiwepesi wepesi, lakini JK alikuwa radhi kuikosa ikulu ilimradi Tundu Lissu asiwe Mbunge. Kwa hints hiyo unaweza kujiuliza who is Tundu Antipas Lissu?
 
Nisome vzr tena unielewe. Mm nimesema.
: Muibua hoja amebaki T. Lissu pekee huku akiatarisha maisha yake.
 
Hapa bila kuremba wala kuchengesha maneno, huyo Mashinji ni mzigo wa hatari. Kwa namna cdm ilivyokuwa imejijenga sikutugemea kama inaweza kupata katibu mkuu aliyepoa kama yeye? Najiuliza mara mbilimbili nini kimeipata cdm mpaka kufikia mahali pa kumpa mtu kama yeye ukatibu mkuu. Kuna mtu mzuri kama Marcus Albanie mbona hakupewa hiyo nafasi badala ya huyo jamaa aliyezubaa hivyo? Kwa ukatibu mkuu huu wa huyu jamaa basi cdm tumejichimbia shimo wenyewe.
 
Kwa taarifa yako asilimia 90 ya misimamo ya Dr Slaa ilitokana na juhudi binafsi za Tundu Lissu. Hilo jina unalichukulia kiwepesi wepesi, lakini JK alikuwa radhi kuikosa ikulu ilimradi Tundu Lissu asiwe Mbunge. Kwa hints hiyo unaweza kujiuliza who is Tundu Antipas Lissu?
Watu mna imani za ajabu sijui huwa mnazipata wapi ???
 
Kwa taarifa yako asilimia 90 ya misimamo ya Dr Slaa ilitokana na juhudi binafsi za Tundu Lissu. Hilo jina unalichukulia kiwepesi wepesi, lakini JK alikuwa radhi kuikosa ikulu ilimradi Tundu Lissu asiwe Mbunge. Kwa hints hiyo unaweza kujiuliza who is Tundu Antipas Lissu?
Acha ujinga kwa hiyo huyo Tundu Lissu anashindwa nini kuonyesha hiyo misimamo kwa Mashinji ili awe kama Dr. Slaa ama zaidi ya Dr Slaa.!
 
Hapa bila kuremba wala kuchengesha maneno, huyo Mashinji ni mzigo wa hatari. Kwa namna cdm ilivyokuwa imejijenga sikutugemea kama inaweza kupata katibu mkuu aliyepoa kama yeye? Najiuliza mara mbilimbili nini kimeipata cdm mpaka kufikia mahali pa kumpa mtu kama yeye ukatibu mkuu. Kuna mtu mzuri kama Marcus Albanie mbona hakupewa hiyo nafasi badala ya huyo jamaa aliyezubaa hivyo? Kwa ukatibu mkuu huu wa huyu jamaa basi cdm tumejichimbia shimo wenyewe.
Hongera mkuu umeliona hili la Dk albanie..... huyu ni asset cjui kwanni chama hakikumpandisha cheo kuwa katibu mkuu!!! Kwa uongozi huu wa magu na ubabe wa ccm tulihitaji katibu mkuu "very active" ili kuweza kubalance power ya kisiasa za ushindani hapa tanzania!!! Kwa namna yoyote hyu katibu mkuu abadilishwe kabla ya 2020 otherwise uchaguzi ujao tutaangukia pua hta bila ccm kuiba
 
Back
Top Bottom