Dr. Magufuli aunganisha CCM na Upinzani

Dr. Magufuli aunganisha CCM na Upinzani

happymalya

Senior Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
116
Reaction score
27
MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, ameanza mkakati wa kukusanya kura kutoka vyama tofauti, ikiwemo vyama vinavyounda kundi la Ukawa.

Kwa muda mrefu sasa baada ya kuelezea sera za CCM na namna zitakavyogusa maisha ya wananchi, kuanzia katika afya, elimu na miundombinu mpaka katika kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na kuboresha makazi, Dk Magufuli amekuwa akiomba kura kutoka vyama hivyo.

Katika mikutano mbalimbali ikiwemo ya Mvomero mkoani Morogoro na wa Kilindi, Tanga juzi, Dk Magufuli alisema maendeleo hayana chama na kuwataka wananchi wa vyama mbalimbali, kumpigia kura ili awatumikie.

Huku akitumia sifa zinazomtambulisha zaidi kwa wananchi kuliko ilivyo kwa wagombea wengine za uadilifu na uchapakazi, Dk Magufuli amekuwa akiwataka wanachama wa Chadema, wanaposalimiwa kwa neno ‘peoples' na wanapojibu ‘power', wakumbuke kumpa kura Magufuli ili akawatumikie.
Kwa wanachama wa CUF, ambao wakisalimiana hukunja ngumi yenye vidole vitano, amewataka wakati wakikunja ngumi kuhakikisha wanakwenda kumpigia kura yeye awe Rais wa Awamu ya Tano.

Kwa wanaCCM ambao huonesha alama ya kidole gumba, alichosema kuwa ni alama ya namba moja, nao amewataka wanapokwenda kupiga kura, wampigie kura na kuhakikisha anakuwa namba moja.

Akielezea sababu za kutoa salamu za vyama tofauti katika mikutano yake wakati yeye ni mgombea wa CCM, Dk Magufuli amekuwa akisema kuwa kwanza hakuna Mtanzania hata mmoja aliyezaliwa na kujikuta akiwa katika chama fulani cha siasa.

Pili, Dk Magufuli alisema wanaokwenda katika mikutano yake si wana CCM peke yao, bali pia wapo wanaChadema, wanaCUF, wanaACT na wa vyama vingine na wasio na vyama.

Dk Magufuli pia alisisitiza umuhimu kwa wananchi kutunza umoja, amani na mshikamano wa Watanzania kwa sababu bila vitu hivyo, hakuna kitakachofanyika kuanzia siasa, shughuli za kijamii wala za kiuchumi.

Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusufu Makamba, aliwataka wananchi katika uchaguzi huu kutazama sifa za mgombea na sifa za chama. Akitaja baadhi ya sifa za Dk Magufuli, mbali na uadilifu na uchapakazi, Makamba alisema mgombea huyo pia ni msomi kuliko wagombea wengine kwa kuwa ndiye mwenye shahada ya uzamivu (PHD).
 
Kuna mwananchi ambaye anaweza kumtenganisha magufuli na ccm?
Au magufuli ni mgombea binafsh?
 
Namaanisha kupitia nguvu za upinzani MAGUFULI aelekea IKULU kwa mbwembwe zoteeee
 
"Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira".

Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha "wateule" na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao.

Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakatutazama na kuuliza, "kulikoni?".

Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya "malofa" wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: "Kama ni hivyo, kwa nini wasile keki na mihogo?"

Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara yao pendwa,vijana wenye vipaji vya mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu",wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wanaambiwa ni majangili huku tembo na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia.

Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona wanawapigia madai yao sahihi yamekuwa kelele wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwatesa waandishi wa habari zao.

Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni "vijisenti", au fedha ya mboga, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa "Wapige mbizi" na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa "Ni heri wale nyasi.

Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili.

Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM."ALUTA Continua, Victoria Ascerta".... "The Struggle Continues, Victory is Certain"; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!
 
Hatumpingi Magufuli, tumechoshwa na hicho chama chake tu baasi. Labda wabadilishe jina wakiite kitu kingine hata UKAWIYAAAA. Labda ndo tutamchagua. Ati hao wapiga debe wake haswa huyo wa wazazi wanasema ati wao tiyari weshajua kura zao. Safi saana tu ila mwambieni, kwa kipondo walichokwisha pondwa Watz ccm imeshawatoka siku nyingiiiii. Magofuli kishagundua hilo. Ndo maana anasema; Chagua Magufuli. Hasemi tena chagua ccm. Hilo jina ccm ni sumu ya mamba. Wala usiiguse.
 
Back
Top Bottom