Dr.KITILA MKUMBO NAOMBA UFAFANUZI KATIKA HAYA!

Dr.KITILA MKUMBO NAOMBA UFAFANUZI KATIKA HAYA!

JATELO1

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
1,230
Reaction score
304
1. Ni kwanini ameendelea kufanya kazi UDSM ambayo VC (Prof. Mukandala) wake ni mtu muhimu sana katika serikali ya CCM, kwani Prof., ni mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Ni kwanini Dr. Mkumbo ameendelea kupewa vyeo UDSM, kwani baada ya kuwa Head wa Department of Psychology pale UDSM, sasa ni Dean School of Psychology DUCE?

Kumbuka kwamba hivi vyeo vyote ni vya kuteuliwa na VC pamoja na DVCs. Naelewa kuna watu watakuja kusema kwamba katika nafasi hizo alizoshikilia kuna Search Team inayopendekeza majina na teuzi husika. Ni kweli ki utaratibu ilitakiwa kuwa hivyo, lkn practically siyo. Nasema hivi kwasababu ya yanayoendelea pale UDSM. Kwa ufupi ni kwamba bila VC wa UDSM kukubali, wewe hutopata cheo kama hicho.Tuna mifano hai kwa yanayoendelea pale UDSM katika baadhi ya Shule ambapo uzoefu (hali halisi) inaonyesha kwamba BILA KUWA MTU WA VC, then sahau kabisa hizo posts kubwa za teuzi pale UDSM.

Pia naomba niwafahamishe wale watakaokuja na hoja ya seniority kwa Dr. Mkumbo. Ukweli ni kwamba posts kama za Dean pamoja na Heads wa Departments wanaangalia Senior Lectures. Lkn si kweli kwamba mara zote hili nalo linafanya kazi, kwani pale UDSM kwenye baadhi ya maidara kwenye shule mbalimbali zinaongozwa na Lecturers (siyo Siniors) pamoja na kwamba kwenye idara husika kuna senior lecturers wengi. Pia hata katika School of Education kuna Senior Lecturers wengi sana, hivyo siyo jambo jepesi kwa Dr. Mkumbo kupewa hizo nafasi bila kuwa na YES na Bwana mkubwa. Naomba nissisitize kwamba ili VC akupe nafasi za teuzi ni LAZIMA UWE MTU WAKE, sas swali hapa ni Je, Dr. Mkumbo ambaye amekuwa Senior Lecturer mwaka juzi naye ni mtu wa system?

3. Jambo lingine ambalo mimi toka awali ilinifanya niwe na mashaka na Dr. Kitila ni jinsi alivyomtetea Juliana Shonza kipindi kile anavuruga BAVICHA kwa kuita press conference na kuanza mashambulizi dhidi ya mwenyekiti wake ndugu Heche. Kama mtakumbuka vizuri ni kwamba huyu Dr. Mkumbo aliandika hapa JF na kwenye gazeti moja (nafikiri ni Raia Mwema kama kumbukumbu zangu zipo sahihi) akimtetea Juliana Shonza kwamba bado ni mtoto hivyo aachwe. Jambo hili lilinifanya niamini kwamba Dr. Mkumbo yuko CHADEMA kwa lengo maalumu na si vinginevyo.
Ahsanteni.
 
Dr Kitila kawaboa wengi baada ya kujulikana ni mamluki jamaa alikuwa anaheshimiwa sana sana ndani ya nchii hii anakazi sana ya kuja kuwarudisha watu wote waliomuamini
 
Haheshimiwi mtu kwa umbo na sura yake kauri na matendo ya mtu ndiyo humpa heshima.

Alichokifanya Kitila Mkumbo si Uhaini bali ni mkakati halali wa mageuzi wa ndani kwa ndani. Mkakati ambao, amini usiamini, haujafa wala haujajerihiwa kwa sababu haukuwa wa Kitila peke yake.

Piga ua, galagaza ng'oa hata kucha kama serikali ya CCM,mkakati huu ni lazima ufanyiwe kazi wakati wa uchaguzi kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi TAIFA.
 
Kama CHADEMA wamekuwa na macho ya kumwona Zito Zuberi Kabwe nyendo zake za kisiasa ndani na nje ya chama,Mapato yake anayoingiza nje na mshahara wake wa Ubunge,na kunasa madudu mengi ya matendo yake,Huo mtandao ulianzishwa kwa mkakati maalumu wa kukiua chama ni nini hata usitambulike? NASHAURI CHADEMA FUMUENI HUO MTANDAO WOTE MBAKI NA WATU SAHIHI WENYE KUNIA MAMOJA.
 
Nadhani CHADEMA siyo chama makini kama tunavyominishwa kwa sababu huwezi kuwa chama makini halafu ukawa na wanachama wengi ambao baadaye unakuja kuwagundua kuwa ni mamluki. Wengine wao wanakuwa mamluki kwa sababu ya njaa, ambayo kwa chama makini ilitakiwa kiwe kimejipanga vizuri kukabiliana nalo. Sasa iwapo chama kinatumia hela zote za luzuku kulipia deni la mwenyekiti wake tu, inakuwa ni vigumu kubaki na hela za kuwalipa watumishi wachama, na ndipo hapo wengine wao wanapoanza kuganga njaa kwa "mkombozi" yeyote atakayejitokeza. Njaa ni mwama malevya.
 
Chama makini kwakupora mapesa na mali kuweka uswisi,chama makini kung'oa watu meno?leo watumishi ukitaka kijiendeleza kielimu hupatiwi mkopo tena nasema ni mkopo sio kusomeshwa na serikali kama mlivyosomeshwa eti watu makini...........
 
ndugu yangu nimeisoma makala yako na nimeiona imeandikwa na mtoto au mwehu au mtu mabaye ametoka kulewa ama kuvuta bangi mara nyingi vyeo hupanda kazini sababu ya uwezo wa mtu kuongoza sio kila senior lecturer anaweza kuwa kiongozi uongozi ni kipaji mtu anachopewa na mungu....Kitila lazima awe karibu na VC sababu ni Boss wake hivyo hoja yako haina mashiko kabisa na hapa naanza kutilia mashaka uwezo wako wa kuelewa vitu na kuchanganua...ni kitila huyu huyu ndiye aliyeandaa ilani ya uchaguzi ya CDM ya mwaka 2010 Slaa alikuwa na kazi rahisi tu ya kubwabwaja alichokiaandaa kitila...sasa unataka jibu lipi suala la kazi na chama vinaingilianaje nyie vijana mliovamia chama juzi juzi ndio mnataka kupata majina kwa njia rahisi mimi ni mwana CDM damu na walichokiandika Mkumbo na Mwigamba ni sahihi kabisa hakuna ubishi katika hiloo.....vinajana wengi mlioingia CDM mnafanya kama ni mpo vitani na CCM ni adui na mwisho wa siku jazba zinawafanya muwe waropokaji na vibaraka wa kundi flanai ya watu au mmeona ajira ni ngumu sasa mnatafuta njia rahisi ya kutokea kwa kupitia siasa.....kazeni fikra zenu muwe wachanganuzi wazuri wa mambo CDM inanukaa
 
Back
Top Bottom