Ni kweli hauwezi kuipongeza serikali eti kwa ajili imejenga barabara ya lami! ni jukumu lake kumfanyia mwnanchi wake na ndio maana zikawekwa serikali kwa ajlili ya kusimamia mambo haya. Nitaipongeza serikali siku nikiona maisha ya mtanzania yanakuwa angalau, na ukizingatia nchi ni tajiri na ndio maana sera zao ccm huwa ni barabara hapa barabara pale kuwadanganya watanzania. Ndio maana Mwalimu Nyerere alikuwa akiwatukana kwa kuwaambia wanakuja na mawazo ya KIJINGAJINGA.
Kweli ni mazuzu watu wanashabikia wajibu wa serikali wakati inatukamua na kodi kichizi Huku wakiiba rasilimali zetu kwi! Kwi! Kwi! Mishabiki ya ccm ni mizee yote kimawazo na kifikra muda wote wanawaza pilau na Tshirt
Hata siku moja huwezi kumsikia Obama akisema atajenga barabara lakini utasikia akizungumzia Afya ,Ajira ,Uhamiaji ,Elimu, Sayansi na Technojia lakini siyo kuahidi meli. Pia ccm hawachelewi kusema watamleta yesuNdio maana Dr Slaa kwenye hotuba zake 2010 alisema yeye hatoi ahadi za kujenga barabara kwa sababu yeye si afisa miradi hiyo ni kazi ya serikali yoyote iliyopo madarakani,alisema serikali inatakiwa ije na mikakati madhubuti ya kuwaondoa wananchi wake katika lindi la umaskini ikiwemo kuondoa kabisa nyumba za tembe tanzania,siyo nitajenga barabara mara viwanja vya ndege,mara visima mara nitachimba mitaro.
Hata siku moja huwezi kumsikia Obama akisema atajenga barabara lakini utasikia akizungumzia Afya ,Ajira ,Uhamiaji ,Elimu, Sayansi na Technojia lakini siyo kuahidi meli. Pia ccm hawachelewi kusema watamleta yesu
jamaa aha akili sana huyu.i think he is another shivji a critical thinker.
Yaani sifa zote hizo kwa kuwa kasema hayo tu? mbona ni mambo ya kawaida sana yanaweza kusemwa na karibu mtu yoyote sasa hizo sifa zote za nini? mimi sioni cha ajabu alichokisema hapo!
Mbaya zaidi ni pale baba anapozunguka mtaani kujisifia kuwa niliahidi nitawaletea nyama leo nimeleta.
Hivi kweli kuna haja ya mawaziri kuzunguka nchi nzima kujisifia na kuendelea kutoa ahadi kwa wananchi badala ya kufanya shuhuli za ofisi wanazopaswa kufanya??
TZ tunahitaji viongozi wawajibikaji na sio hawa ccm wazururaji.
Dr.Kitila ametoa hoja nzinto na ya msingi.
kwahiyo wewe ukipeleka mboga nyumbani kwako utaanza kuwatangazia majirani zako kwamba leo umeleta mboga nyumbani?Nd yangu kitila acha wivu usituvunje moyo kwa nn tusishangilie maendeleo? pamoja na kuwa serikari ni wajibu wake watu kama wewe ni hatari ktk uhai wa taifa letu, hv hujuwi kama unapoongEza mkoa unapanua na kusogeza huduma karibu kwa wananchi pia ajira au wewe kwa kuwa umeajiriwa hapo chuo kikuu hutaki watnzania wengine wapate ajira na huduma zingine? hayo ni mawazo yako na usitake wengine waamini hivyo.
Pamoja na mambo mengine akiongea katika kipindi cha changamoto kinachorushwa na startv Dr.Kitila Mkumbo wa Udsm amesema kushangilia utekelezaji wa majukumu ya serikali ni uzuzu.
"Watu wanashangilia kama mazuzu eti serikali imetujengea barabara ya lami wakati ni haki yao kujengewa barabara na huo ni wajibu wa serikali kuwaletea wananchi maendeleo hakuna haja ya kushangilia na kuwapongeza mawaziri"
Amesema miongoni mwa mambo yanayofanya huduma za jamii kuwa mbovu ni pamoja na gharama kubwa ya uendeshaji wa serikali(utawala),"serikali inaacha kuwajengea wananchi zahanati,shule lakini inakimbilia kuongeza mikoa na wilaya jambo ambalo ni mzigo mkubwa kwa mwananchi wa kawaida."Hiyo mikoa mipya inamsaidia nini mwananchi?amehoji.
"Ukitaka kuharibu taifa ua elimu,Somalia wamefika pale walipo kwa sababu waliua elimu na ndio maana mpaka leo wako vile walivyo.
Akiongelea Swala la katiba mpya amesema ilitakiwa utaratibu wa ukusanywaji wa maoni uboreshwe zaidi kwa kushirikisha mawazo ya vyama vya siasa kama Chadema na vinginevyo,Amesema mwananchi hana haja ya kujua maana ya katiba bali aseme nini anataka kifanyike kwa ajili ya maisha yake.
Nawasilisha kwa mjadala zaidi wa kauli hizi.
Nd yangu kitila acha wivu usituvunje moyo kwa nn tusishangilie maendeleo? pamoja na kuwa serikari ni wajibu wake watu kama wewe ni hatari ktk uhai wa taifa letu, hv hujuwi kama unapoongEza mkoa unapanua na kusogeza huduma karibu kwa wananchi pia ajira au wewe kwa kuwa umeajiriwa hapo chuo kikuu hutaki watnzania wengine wapate ajira na huduma zingine? hayo ni mawazo yako na usitake wengine waamini hivyo.
Nd yangu kitila acha wivu usituvunje moyo kwa nn tusishangilie maendeleo? pamoja na kuwa serikari ni wajibu wake watu kama wewe ni hatari ktk uhai wa taifa letu, hv hujuwi kama unapoongEza mkoa unapanua na kusogeza huduma karibu kwa wananchi pia ajira au wewe kwa kuwa umeajiriwa hapo chuo kikuu hutaki watnzania wengine wapate ajira na huduma zingine? hayo ni mawazo yako na usitake wengine waamini hivyo.