Dr. Kitila Mkumbo: Kushangilia utekelezaji wa majukumu ya serikali ni Uzuzu!

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
1,084
Pamoja na mambo mengine akiongea katika kipindi cha changamoto kinachorushwa na startv Dr.Kitila Mkumbo wa Udsm amesema kushangilia utekelezaji wa majukumu ya serikali ni uzuzu.

"Watu wanashangilia kama mazuzu eti serikali imetujengea barabara ya lami wakati ni haki yao kujengewa barabara na huo ni wajibu wa serikali kuwaletea wananchi maendeleo hakuna haja ya kushangilia na kuwapongeza mawaziri"

Amesema miongoni mwa mambo yanayofanya huduma za jamii kuwa mbovu ni pamoja na gharama kubwa ya uendeshaji wa serikali(utawala),"serikali inaacha kuwajengea wananchi zahanati,shule lakini inakimbilia kuongeza mikoa na wilaya jambo ambalo ni mzigo mkubwa kwa mwananchi wa kawaida."Hiyo mikoa mipya inamsaidia nini mwananchi?amehoji.

"Ukitaka kuharibu taifa ua elimu,Somalia wamefika pale walipo kwa sababu waliua elimu na ndio maana mpaka leo wako vile walivyo.

Akiongelea Swala la katiba mpya amesema ilitakiwa utaratibu wa ukusanywaji wa maoni uboreshwe zaidi kwa kushirikisha mawazo ya vyama vya siasa kama Chadema na vinginevyo,Amesema mwananchi hana haja ya kujua maana ya katiba bali aseme nini anataka kifanyike kwa ajili ya maisha yake.

Nawasilisha kwa mjadala zaidi wa kauli hizi.
 
Ni kweli hauwezi kuipongeza serikali eti kwa ajili imejenga barabara ya lami! ni jukumu lake kumfanyia mwnanchi wake na ndio maana zikawekwa serikali kwa ajlili ya kusimamia mambo haya. Nitaipongeza serikali siku nikiona maisha ya mtanzania yanakuwa angalau, na ukizingatia nchi ni tajiri na ndio maana sera zao ccm huwa ni barabara hapa barabara pale kuwadanganya watanzania. Ndio maana Mwalimu Nyerere alikuwa akiwatukana kwa kuwaambia wanakuja na mawazo ya KIJINGAJINGA.
 
Ni kweli kabisa kuishangilia serikali ni sawa na kumpongeza baba kaleta mboga nyumbani wakati ni jukumu lake.
 
Ili serikali ishangiliwe inapaswa imefanye mambo magumu yaliyoshindikana,mfano kuondoa kero ya rushwa,umaskini uliokithiri,kuondoa msongamano wa magari ndani ya jiji la dar es salaam sio kuupa aspirin kama wanavyofanya sasa,kuunda mfumo bora wa elimu sio mfumo mbovu kama wa sasa.Akina mulugo ni zao la mfumo mbovu wa elimu,kama mfumo ungekuwa mzuri asingekuwa na nafasi ktk uongozi wa juu serikalini.
 
Kweli ni mazuzu watu wanashabikia wajibu wa serikali wakati inatukamua na kodi kichizi Huku wakiiba rasilimali zetu kwi! Kwi! Kwi! Mishabiki ya ccm ni mizee yote kimawazo na kifikra muda wote wanawaza pilau na Tshirt

Ndio maana Dr Slaa kwenye hotuba zake 2010 alisema yeye hatoi ahadi za kujenga barabara kwa sababu yeye si afisa miradi hiyo ni kazi ya serikali yoyote iliyopo madarakani,alisema serikali inatakiwa ije na mikakati madhubuti ya kuwaondoa wananchi wake katika lindi la umaskini ikiwemo kuondoa kabisa nyumba za tembe tanzania,siyo nitajenga barabara mara viwanja vya ndege,mara visima mara nitachimba mitaro.
 
Mimi nitaanza kuishangilia serikali endapo itaanza kutekeleza kwa vitendo (sio maneno matupu) utaratibu wa kutupatia mashamba na viwanja katika sayari nyingine na usafiri wa uhakika wa kwenda na kurudi. Hili sio miongoni mwa majukumu yake lakini ikiweza kuja na ubunifu huu nitashangilia.

Lakini kulinda mipaka yetu na kuhakikisha Ziwa Nyasa halichukuliwi na adui wala sishangilii kwani ni moja ya majukumu yake kikatiba na ikishindwa katika hili inatakiwa kuondoka madarakani.
 
Ndio maana Dr Slaa kwenye hotuba zake 2010 alisema yeye hatoi ahadi za kujenga barabara kwa sababu yeye si afisa miradi hiyo ni kazi ya serikali yoyote iliyopo madarakani,alisema serikali inatakiwa ije na mikakati madhubuti ya kuwaondoa wananchi wake katika lindi la umaskini ikiwemo kuondoa kabisa nyumba za tembe tanzania,siyo nitajenga barabara mara viwanja vya ndege,mara visima mara nitachimba mitaro.
Hata siku moja huwezi kumsikia Obama akisema atajenga barabara lakini utasikia akizungumzia Afya ,Ajira ,Uhamiaji ,Elimu, Sayansi na Technojia lakini siyo kuahidi meli. Pia ccm hawachelewi kusema watamleta yesu
 
Oh Yes! Tena hiyo ni katika "policy levels" na sio kupeleka "chakula cha njaa" mahali fulani kipindi cha uchaguzi kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi au akina Magufuli walivyoahidi ujenzi wa "daraja la Mbutu" wakati wa uchaguzi mdogo Igunga halafu kama mazuzu tunashangilia na kucheza ngoma eti serikali yetu imetekeleza!

Wenzetu wana-discuss SERA na IDEAS sisi tunajadili WATU na VITU na kama tunacho tunachokiita sera basi ni sera chovu zisizo na tofauti na mipasho.
 
Mbaya zaidi ni pale baba anapozunguka mtaani kujisifia kuwa niliahidi nitawaletea nyama leo nimeleta.
Hivi kweli kuna haja ya mawaziri kuzunguka nchi nzima kujisifia na kuendelea kutoa ahadi kwa wananchi badala ya kufanya shuhuli za ofisi wanazopaswa kufanya??
TZ tunahitaji viongozi wawajibikaji na sio hawa ccm wazururaji.
Dr.Kitila ametoa hoja nzinto na ya msingi.
 
Nd yangu kitila acha wivu usituvunje moyo kwa nn tusishangilie maendeleo? pamoja na kuwa serikari ni wajibu wake watu kama wewe ni hatari ktk uhai wa taifa letu, hv hujuwi kama unapoongEza mkoa unapanua na kusogeza huduma karibu kwa wananchi pia ajira au wewe kwa kuwa umeajiriwa hapo chuo kikuu hutaki watnzania wengine wapate ajira na huduma zingine? hayo ni mawazo yako na usitake wengine waamini hivyo.
 
Yaani sifa zote hizo kwa kuwa kasema hayo tu? mbona ni mambo ya kawaida sana yanaweza kusemwa na karibu mtu yoyote sasa hizo sifa zote za nini? mimi sioni cha ajabu alichokisema hapo!

kwenye hoja za msingi lazima mponde,ingekuwa hoja zenu za kipumbavu za mapenzi mngeshadadia sana na wenzio akina Ritz na chama.
 
Mbaya zaidi ni pale baba anapozunguka mtaani kujisifia kuwa niliahidi nitawaletea nyama leo nimeleta.
Hivi kweli kuna haja ya mawaziri kuzunguka nchi nzima kujisifia na kuendelea kutoa ahadi kwa wananchi badala ya kufanya shuhuli za ofisi wanazopaswa kufanya??
TZ tunahitaji viongozi wawajibikaji na sio hawa ccm wazururaji.
Dr.Kitila ametoa hoja nzinto na ya msingi.

Ni sawa na kuzaa mtoto afu unanunua chandarua asipate malaria,unaanza kuzunguka kwa watu kutangaza ili wakusifie badala ya kuanza kumuandalia mwanao mazingira ili aje apate elimu bora baadaye,kumbe wenzio wanakudharau na kukuona hamnazo.ndio serikali hii tuliyonayo.
 
Nd yangu kitila acha wivu usituvunje moyo kwa nn tusishangilie maendeleo? pamoja na kuwa serikari ni wajibu wake watu kama wewe ni hatari ktk uhai wa taifa letu, hv hujuwi kama unapoongEza mkoa unapanua na kusogeza huduma karibu kwa wananchi pia ajira au wewe kwa kuwa umeajiriwa hapo chuo kikuu hutaki watnzania wengine wapate ajira na huduma zingine? hayo ni mawazo yako na usitake wengine waamini hivyo.
kwahiyo wewe ukipeleka mboga nyumbani kwako utaanza kuwatangazia majirani zako kwamba leo umeleta mboga nyumbani?
 
Pamoja na mambo mengine akiongea katika kipindi cha changamoto kinachorushwa na startv Dr.Kitila Mkumbo wa Udsm amesema kushangilia utekelezaji wa majukumu ya serikali ni uzuzu.

"Watu wanashangilia kama mazuzu eti serikali imetujengea barabara ya lami wakati ni haki yao kujengewa barabara na huo ni wajibu wa serikali kuwaletea wananchi maendeleo hakuna haja ya kushangilia na kuwapongeza mawaziri"

Amesema miongoni mwa mambo yanayofanya huduma za jamii kuwa mbovu ni pamoja na gharama kubwa ya uendeshaji wa serikali(utawala),"serikali inaacha kuwajengea wananchi zahanati,shule lakini inakimbilia kuongeza mikoa na wilaya jambo ambalo ni mzigo mkubwa kwa mwananchi wa kawaida."Hiyo mikoa mipya inamsaidia nini mwananchi?amehoji.

"Ukitaka kuharibu taifa ua elimu,Somalia wamefika pale walipo kwa sababu waliua elimu na ndio maana mpaka leo wako vile walivyo.

Akiongelea Swala la katiba mpya amesema ilitakiwa utaratibu wa ukusanywaji wa maoni uboreshwe zaidi kwa kushirikisha mawazo ya vyama vya siasa kama Chadema na vinginevyo,Amesema mwananchi hana haja ya kujua maana ya katiba bali aseme nini anataka kifanyike kwa ajili ya maisha yake.

Nawasilisha kwa mjadala zaidi wa kauli hizi.

Hapo ndipo manapochemka, kwa maana Watanzania wengi wetu ndio tuko hivyo sasa, Serikali ikijenga Barabara tunaifagilia, kama mtaita ni uzuzu hayo ni maoni yenu na hayabadilishi chochote, mtaendelea kusema na kutuita majina yote manayoyajua sijui mazuzu, sijui vilaza lakini ndio tuko hivyo na kama mnataka kura zetu sisi mazuzu inabidi kwanza mtukubali vinginevyo mtaishia kuongea tu na kutukashifu lakini mwisho wa siku CCM wanachukua kura, na unajua kwa nini, wanatuelewa hawatukashifu kwa kutuita majina kama mazuzu!

Kinachowaangusha wapinzani na kitaendelea kuwaangusha huko mbele ya safari ni kwamba hamjawaelewa Watanzania wakoje, mnaiangalia jamii ya Kitanzania kutoka kwenye pembe nyingine kabisa ambayo sio ya uhalisia wa maisha yetu, matokeo yake ndio hayo mnawekeza muda na rasilimali nyingi kwenye kukampenia vitu ambavyo havina uhalisia na havieleweki na jamii na hilo linawagharimu na litaendelea kuwagharimu mpaka hapo mtakapotambua kuwa Watanzania tukoje, CCM wanatujua na ndio maana wanaendelea kushinda, Bw.Kinana huyo kila anapokwenda nyomi linamfuata nyie mmekalia kutuita mazuzu, mwisho wa siku CCM wanashinda!

Nd yangu kitila acha wivu usituvunje moyo kwa nn tusishangilie maendeleo? pamoja na kuwa serikari ni wajibu wake watu kama wewe ni hatari ktk uhai wa taifa letu, hv hujuwi kama unapoongEza mkoa unapanua na kusogeza huduma karibu kwa wananchi pia ajira au wewe kwa kuwa umeajiriwa hapo chuo kikuu hutaki watnzania wengine wapate ajira na huduma zingine? hayo ni mawazo yako na usitake wengine waamini hivyo.

hujamuelewa,maana yake serikali inatakiwa kutekeleza sera za kitaifa kama Afya bora,elimu bora,science na teknojojia,uchumi wa watu wako.hayo mengine waachie madiwani ndio kazi zao hizo,Rais kutoa ahadi ya kuchimba kisima ni ukichaa.
 
Nd yangu kitila acha wivu usituvunje moyo kwa nn tusishangilie maendeleo? pamoja na kuwa serikari ni wajibu wake watu kama wewe ni hatari ktk uhai wa taifa letu, hv hujuwi kama unapoongEza mkoa unapanua na kusogeza huduma karibu kwa wananchi pia ajira au wewe kwa kuwa umeajiriwa hapo chuo kikuu hutaki watnzania wengine wapate ajira na huduma zingine? hayo ni mawazo yako na usitake wengine waamini hivyo.

hiyo pesa mnayotumia kuzunguka nchi nzima kushangilia wajibu wenu zingetumika kufanya maendeleo makubwa tanzania, kuongeza mkoa mpya kuna haja gani ya kufanya kuwa ni jambo la kusherehekea kwa pesa nyingi badala ya kutumia pesa hizo kusimamia miundo mbinu na huduma za kijamii ndani ya mikoa iyo.
Tusipende kuendekeza shamra zisizo na tija kwenye nchi hii maskini.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom