MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Wakati Mbuge wa viti maalum Cecilia Pareso akiuliza swali bungeni kutaka majibu kutoka serikalini juu ya gharama kubwa za pesa zinazotumika kufunga mashine za kielekroniki kwa ajili ya mifumo ya ukusanyaji taarifa za zote za afya na mapato ni kubwa katika mahospitali ya umma kuliko mahospitali binafsi, kitu ambacho kinaashiria kua kuna harufu za ufisadi ndani yake.
Mradi huu kwa baadhi hospitali kubwa za umma za majaribio ya awali unafadhiliwa na mfuko wa bima ya afya nchini NHIF.Akijibu swali hili naibu waziri Dr Hamisi Kigwangala ametetea kua hospitali kubwa za umma mfano MOI na BOMBO zimetumia gharama kubwa kwa sababu zinafungiwa mifumo yote ya ukusanyaji taarifa kwamba huwezi kulinganisha na hospitali zingine! Sijui kama majibu ya waziri Kigwangala yalilenga kujibu maswali yaliyoulizwa!mfano hospitali ya Cellian ya mkoani Arusha ambayo inefungiwa mifumo yote, Hospitali ya Agakhani ya Dar es salaam nk, ni Miongoni mwa hispitali binafsi ambazo ukifanyia utafiti wa kina utaona zimefunga vifaa hivyo kwa gharama ndogo kuliko hispitali za umma! hapa ndiko yaliko maswali! Waziri badala ya kusema anafanyia uchunguzi lakini yeye enatetea?
NHIF hawa hawa ambao waliwahi kupigiwa kelele kumhonga gari aina ya shangingi mmoja wa mawaziri wa awamu ya nne katika wizara hiyo. Dr Kigwangala amejibu kwa maslahi ya umma au kuna kitu kinajificha hapa? Kwa akili ya haraka haraka mashine kufungwa kwenye hospitali za umma gharama haziwezi kua kubwa kuliko hospitali za binafsi huku kazi zake zinafanana.