Dr. Kigwangalla aja juu alipoulizwa kuhusiana na ForePlan Clinic

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,388
24,947
Itakumbukwa siku za nyuma, Naibu waziri wa afya, Dk. Hamisi Kigwangalla, aliwahi kufanya ziara ya kushtukiza na kufanya ukaguzi kwenye kituo cha Foreplan Clinic cha Dkt. Mwaka.

Huko Twitter ameibuka jamaa mmoja na kumuuliza Kigwangalla hiviii; "Hivi suala la Dr. Mwaka liliishia wapi? Mh. HKigwangalla ulilijia juu sana lkn hv sasa hakuna mrejesho.

Au tuamini nyaraka zake alizozitoa?" Majibu ya Kigwangalla yakawa haya; "Sina la kusema. Muulize msemaji wa Wizara"Nini maoni yako?

d3f5668a808a87daa5bb6dc2261157b3.jpg
 
Mlitaka aseme nini wakati alikuja kugundua kuwa Dr Mwaka anawazidi hata madaktari wake pale Muhumbili na Agha?? Wanawake waliokuwa wameambiwa ni tasa kabisa na madaktari wake Muhumbili na Agha wakaenda kwa Dr. Mwaka, leo wananyonyesha.
Anataka wampelekee watoto waliowapata kwa Dr. Mwaka? Acheni jamani, ukiendekeza sana Muhumbili waweza pata kichaa. Mnauona ule msongamano?? Kila kukicha wagonjwa wamejaa, vitendea kazi hakuna. Kweli muulizeni tu msemaji wala sio muhishimika waziri
 
Chanzo : EATV

d3f5668a808a87daa5bb6dc2261157b3.jpg
Kukurupuka kutafuta sifa kumfurahisha bosi
 
Huyu sijui digrii yake aliipata wapi..hata Ummy Mwalimu anamzidi japo siyo dokta. Kingine jamaa ni mpenda kick instead of kuonyesha ufanisi kazini.
 
Mlitaka aseme nini wakati alikuja kugundua kuwa Dr Mwaka anawazidi hata madaktari wake pale Muhumbili na Agha?? Wanawake waliokuwa wameambiwa ni tasa kabisa na madaktari wake Muhumbili na Agha wakaenda kwa Dr. Mwaka, leo wananyonyesha.
Anataka wampelekee watoto waliowapata kwa Dr. Mwaka? Acheni jamani, ukiendekeza sana Muhumbili waweza pata kichaa. Mnauona ule msongamano?? Kila kukicha wagonjwa wamejaa, vitendea kazi hakuna. Kweli muulizeni tu msemaji wala sio muhishimika waziri
Una uhakika ni hiyo mitishamba au ni coincidence. Kuna wanawake wametolewa fallopian tubes anawaambia chukua dawa mtazaa, shit!
 
Madhara ya kufanya kazi kwa mizuka..
Hawa wengi walikuwa wanafanya kazi kwa kuogopa ngazi za uteuzi, ili kwamba waonekane ni watingaji wazuri. Ina maana gani kuita media wakati unataka usikike, na ukiona umekosea unaenda kimya. Nadhani ifike mahali tuwe na blog ya kuwalipua hawa wanaoanzisha mambo ambayo hawawezi kuyapeleka hadi mwisho. Inaishia kuwa kama sinema za kitoto ambazo star ndio kila kitu.
 
Kigwangwala alikuwa right sana ila feedback ya jamii ilimfanya Ummy alete siasa kwenye hili na ndio aliotoa maamuzi ya mwisho. Ummy ndio msemaji wa wizara.
 
Mizuka,mihemko na kukurupuka at work.Alilijia juu hilo suala kwa mbwembwe,leo hii chaliiii!!Siku ile alivyokuwa anauza sura mbele ya makamera mbona hakusema akaulizwe msemaji wa Wizara?
 
Hivi sukari bei gani hapo mitaa ya magogoni? mm nipo mbali na serikali nipo huku Ngara, Bigombo. sie sukari 2600/-
 
ndio shida ya kukurupuka na kufanya kazi kwa maelekezo ya akina mange ..teh teh yeye si alifuata maelekezo ya mange... akamuulize mange nini cha kufanya tena
 
Una uhakika ni hiyo mitishamba au ni coincidence. Kuna wanawake wametolewa fallopian tubes anawaambia chukua dawa mtazaa, shit!

CHUAKACHARA;
Naanza kwa declare interests. Simjui Dr Mwaka wala sijawahi kukutana na Dr. Kigwa hivyo sina ninaye mtetea.
Kama hao wamama wako weshatolewa hizo tubu zao, walienda kwa Mwaka kutafuta nini?? Mayai yao yatapitia wapi mpaka yaufikie mfuko wa uzazi?
Basi aliwaona ni mataahira tu. Dr. Mwaka hawaombei miujiza, anawapa dawa wazibuke hiyo mirija sio kutengeneza mirija mipya.
 
Back
Top Bottom