Dr. Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza muhimbili na kukagua mashine za MRI na CT-SCAN

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,768
3,621
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Januari 4, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi.

Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na Kitengo cha dharura, Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU), wodi ya Mwaisela, duka la dawa la MSD na kukagua ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI.

Akizungumzia ziara hiyo mara baada ya kutembelea Hospitalini hapo, Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa ili kuweza kuona hali ya utendaji wa kazi iliyopo katika hospitali hiyo ya taifa tangu ambapo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza na kutokuridhishwa na utendaji kazi wa hospitali hiyo hali iliyopelekea kuivunja bodi iliyokuwa ikisimamia hospitali.

Dk. Kingwangalla alisema amefurahishwa na utoaji wa huduma katika upimaji kwa kutumia mashine ya CT-Scan na MRI ambazo awali wakati wanaingia madarakani hazikuwa katika hali nzuri ya ufanyaji wa kazi na kuwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuifanya hospitali hiyo kuonekana yenye hadhi ya kuwa hospitali ya taifa.

Alisema limekuwa jambo ambalo linasikitisha kuona huduma zinazopatikana katika hospitali ya taifa zinashindwa na huduma zinazotolewa katika hospitali za watu binafsi na akilinganisha huduma za kulipia vitanda zinazotolewa Muhimbili kuwa hazina viwango vya juu ambavyo vinaweza kuwashawishi wananchi wenye uwezo kuacha kwenda hospitali binafsi na kwenda hospitalini hapo.

“Ni jambo la kushangaza hospitali za watu binafsi zinakuwa na watu wengi kuliko hapa na wakati sisi tuna madaktari bingwa zaidi ya 500 hapa Muhimbili lakini hizo hospitali zao hazina hata daktari mmoja bingwa lakini na huduma zinazopatikana katika madaraja ya juu zinatakiwa kuboreshwa,

“Kama tunaweza kuwa na huduma nzuri katika first class (daraja la kwanza) tunaweza kuwavuta wananchi wengi waje hapa na waache kwenda hospitali binafsi, wanatakiwa kutengwa madaraja ya juu ambayo huduma zake zinakuwa zimeboreshwa sio mtu anakuwa daraja la kwanza alafu bado anachangia choo na wengine au anaelala nae hapewi kitanda,” alisema Mhe. Kingwangalla.

Aidha Mhe. Dkt.Kingwangalla aliwatupia lawama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa jinsi wanavyopanga madaraja ya hospitali na kuilinganisha Muhimbili na hospitali zingine za watu binafsi kuwa jambo hilo siyo sahihi kwa kuiweka hospitali ya taifa sawa na hospitali za watu binafsi.

“NHIF wanaweka sehemu moja hospitali ya taifa na hospitali binafsi hili haliwezekani walinganishe huduma zilizopo hospitali ya taifa na zile zingine, nina mpango wa kuwatembelea hivi karibuni nitazungumza nao,” alisema Kingwangalla.

Aidha Mhe. Naibu Waziri aliupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuongeza vitanda katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo awali ilikuwa na vitanda sita hali ambayo ilikuwa ikiwashangaza wananchi wengi kutokana na kuwepo kwa vitanda zaidi ya 1350 katika hospitali hiyo na hivyo kuongezeka kwa vitanda katika wodi hiyo kutasaidia upatikanaji wa wa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.

Awali akitoa taarifa mbele ya Mhe. Dkt. Kingwangalla, Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo, Dkt. Flora Rwakatare alisema tangu kuanza kwa kutumika kwa mashine ya MRI mwishoni kwa mwezi Novemba mwaka jana jumla ya wagonjwa 560 wamefanyiwa vipimo katika mashine hiyo na ndani ya siku tatu amabazo wamefunga mashine mpya ya CT-Scan wameshawapima wagonjwa 26.

Alisema kufungwa kwa mashine ya CT-Scan kunaonekana kuwepo kwa matumaini mapya kwa watanzania kutokana na kasi ya ufanyaji kazi kwa mashine hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya Siemens ambayo inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde 6.

“Mashine ya CT-Scan ambayo imefungwa ina ubora mkubwa na ni ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki na kwasasa tunategemea kufanya kazi kwa ubora zaidi kutokana na ukubwa iliyonayo na inaweza kufanya kazi kwa kasi tofauti na ile iliyokuwa ikitumika awali,” alisema Dkt. Flora.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru alisema awali hawakuwa wakifanya visingizo ili wasifanye kazi lakini ni hali halisi iliyokuwepo kuwa mashine iliyokuwepo awali ilikuwa na matatizo lakini kufanikisha kufungwa kwa mashine mpya ambayo imeigharimu serikali Dola za Kimarekani Milioni 1.7 ambapo ni zaidi ya Milioni 400 za kitanzania kutawapa wao motisha ya kufanya kazi kwa kutumia kifaa cha kisasa na chenye kufanya kazi kwa haraka.

IMG_0891.jpg

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya chumba cha vipimo vya MRI katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016.

IMG_0903.jpg

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.

IMG_0950.jpg

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akikagua wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru akimtembeza Mh. Naibu Waziri kwenye wodi hiyo.

IMG_0951.jpg

SOURCE: MO DEWJI BLOG
 
Kigwangala aache bla blaa. Aseme kwamba serikali itajenga jengo la kisasa kubwa na zuri zaidi kuliko lile la Agha Khan kwa ajili ya hao first class citzens. Mkono mtupu haulambwi. Tuboreshe mapato yetu kwanza, mambo mengine yatakuja tu. Kipaumbele ni kwa the last citzens. kwanza!
 
Last edited:
Kigwangala aache bla blaa. Aseme kwamba. serikali. itajenga jengo la kisasa kubwa na zuri zaidi kuliko lile la Agha Khan kwa ajili ya hao first. class citzens.. Mkono mtupu haulambwi. Tuboreshe mapato yetu.kwanza, mambo mengine yatakuja tu. Kipaumbele ni kwa the last citzens. kwanza!
.......

Kama kuna mawaziri watakaofeli kazi mapema ni huyu Dr Kigwangwalla na Ummy Mwalimu. Viongozi hawa wa Wizara ya Afya kila kukicha ni kuuza sura kwenye blogs na vyombo vingine vya habari.

Sekta ya afya ni sekta muhimu sana lakini ni moja ya sekta zilizovuruguka vibaya vibaya vibaya. Ni holela, kila mtu anajianzishia hospitali yake, kila mtu anajiita daktari, na kila mtu anamgeuza mgonjwa kuwa cash cow! Nilitegemea hawa mawaziri wangekaa chini na kuanza kupitia sera, sheria na miongozo ya sekta ili kuwa na mfumo unaeleweka wa kutoa na kusimamia huduma. Waje jawabu la kueleweka kuhusu utoaji huduma za afya nchi nzima na sio huu usanii wa kuibukia kwenye hospitali na waandishi wa habari kila siku.

Lakini pia, ifike mahala Dr Kigwangwala awape nafasi watendaji wa Muhimbili wafanye kazi. Ziara za kila siku na utititiri wa media ni kupotezeana muda. Mnachosha watu!
 
MRI na CT Scan sio issue sana swala ni Upatikanaji wa madawa nchini hasa vijijini... hilo ndio jipu kuu
 
Mi nashangaa ni dar tu...yaani wamejichimbia huko..kwanini wasije huku vijijini ambapo hata panadol hamna???
 
NA WAENDELEE KUSHTUKIZA KILA SIKU ZIARA HIZO NA KUSIMAMISHA WATUMISHI WAPATE PUBLICITY KWA UMMA BADALA YA KUANGALIA NAMNA BORA YA UTATUZI WA CHANGAMOTO. OBVIOUSLY UNAPOMFUKUZA AU KUMSIMAMISHA MTUMISHI UNARUDI HATUA 3 AU 4 NYUMA KWA MIPANGO ILIYOKUWA ON PROGRESS. LAST WARNING ILIWAFAA SAMA HAWA WANAOSIMAMISHWA WANGEKUWA MAKINI ZAIDI BADALA YA KUWASIMAMISHA HUKU WAKIPATA MISHAHARA. ILIPASWA GOVT I COPE NA TAASISI BINAFSI ZINAVYOENDESHWA. NA IWEPO MIKATABA YA 5 YRS. WATAJITUMA
 
Mi nashangaa ni dar tu...yaani wamejichimbia huko..kwanini wasije huku vijijini ambapo hata panadol hamna???
una uhakika na hicho unachokinena?, Kigwangalla alikuwa mikoa ya kusini na baada ya hapo alikuwa singida, usipende kuyategemea sana magazeti ya udaku ni lazima yatakupa takwimu feki
 
Bw.Kigwangallah
Najua umo huku,naomba nikuulize
Je tatizo la afya nchi hii ni CT SCAN &MRI pekee?
Watu wengi wanaugua na kufa (hasa watoto) kwa kukosa hizo mashine au kwa malaria na kuhara?
Respectfully,get your priorities right
 
Jamani milioni 400 tu kweli tunashindwa kuwa na mashine hizi kila hospitali ya mkoa?
 
Huyo Dk. wa mionzi nilionaga humu ni Dk. Lwakatare. ni Dk mchapa kazi sana

Natumaini madaktari wengi wanafurahia siatimu ya sasa ya kuyovutwa huku na kule na watoaji pesa ili waendelee kufanya kazi wanayoipenda kuhudumia na kutibu wagonjwa vizuri.

Nilisoma pahala wameandika naibu waziri alisema watanunua za kwenda hosp zingine kubwa mikoani nadhani Dodoma na Mwanza kama hiyo juu.
 
Back
Top Bottom