Dr.Kigwangala ukitumwa tumika

Dr.Kigwangala ukitumwa tumika

Ndugu yangu nakumbuka alimkunja daktarii hapo kwa maana mtoto wake alikaa siku 2 bila huduma zaidi ya kupewa dawa za kushusha homa tu.Ilipofika siku ya pili dogo akalegea kabisa, baba mtu(ambaye ndio ndugu yangu) akaenda kumsihi daktari amuangalie mtoto wake maana anakatisha tamaa.Daktari akamwambia asubiri mpaka muda wa kuzungukia wagonjwa ufike. Jamaa akasubiri.
Baada ya muda mfupi dogo akakata kauli, mama yake akaanza kulia huko wodini. Baba mtu akamuomba daktari kama amebanwa basi ampe rufaa mtoto ili apelekwe Muhimbili.Daktari akakataa kwamba hata rufaa ataitoa atakapofanya ziara wodini.

Hapo ndipo baba mtoto uvumilivu ukamshinda akamkunja daktari. Daktari akapiga kelele kuita mlinzi naye akapigwa. Mlinzi akaita wenzake wawili kutoka getini huko ikawa mshikemshike wakamkamata wakampeleka kwa mganga mkuu.
Mganga mkuu akamsikiliza akakimbia kumuona mtoto, akaamuru apelekwe Muhimbili na baba mtoto apelekwe polisi kwa kuleta vurugu. Mama mtoto akapewa ambulance mpaka Muhimbili mtoto akatibiwa akapona baada ya siku chache. Wengine tukaenda kuyamaliza na utawala huko Oysterbay police.

Cha kushangaza hakutokea daktari wala yeyote pale polisi mpaka polisi wakamruhusu baba mtoto ajiondokee zake.

Si njia nzuri kushinikiza madaktari kwa njia hiyo lakini ni muhimu tujue kuwa hata miongoni mwa madaktari wako pia ambao hawana utu na ukiwaogopa hawa wanakupotezea maisha.

Nawapongeza madaktari wazuri wanaojali uhai wa wagonjwa wao na wenye kuvumilia ugumu wa kazi zao.
 
Copy hiii threand ipeleke kwy twitter yake Kigwangala ataifanyia kazi! Hawa madaktari dawa yao kichapo tu mpk wajifunze adabu,mtu umesomeshwa kwa mkopo wa kozi zetu,umejiriwa ufanye kazi hutaki,mabossi wako hawajui kukusimamia kwa nini uspigwe?last walilalamika sana Oooh tumepigwa blah blah hatuna vifaaa,wanasoma mpk improvisation wajiongeze na wawajibike la sivyo apa kazi tu na kipigo juu!yaani mtoto anakufa alafu anajibu utumbo??kwanza jamaa amfungulie kesi ya uzembe uyo dk tuone km wengine hawatanyooka.
 
Back
Top Bottom