#COVID19 Dkt. Kasangala: Vyeti vya waliochanjwa Chanjo ya Corona vitatolewa baadae kidogo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,290
142,491
Mkurugenzi wa elimu kwa umma wizara ya afya Dr Kasangala amesema kwa sasa mkazo umewekwa kwenye kuchanja ili kwenda na muda then watu wote waliochanjwa watapatiwa vyeti vyao kwa utaratibu uliopangwa na watapewa taarifa.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
 
Isije ikawa kama vitambulisho vya NIDA.

Tumeambulia kupewa namba tu....
Nilipata chanjo Amana Hospital Ilala Dar siku ya tarehe 3 Aug sikupewa Certificate kwa madai kwamba zimekwisha. Leo nimekwenda kucheki nikaambulia NIL certificate.

Naona kama vile kuna ka uzembe fulani kwenye hii project ya chanjo.
Watu wameitikia wito saaana.
 
Hayo ndio mambo ya NiDa. Wahini Jamana fasta wawachapishie kadi za rangi ya Blue size ya kadi kama za Yellow fever, kadi zije blank na zijazwe kwa mkono mara baada ya mhusika kuchanjwa.

Vinginevyo mtapotezana maboya.
Pale juu kwenye kadi mnaweka Heading ya Covid 19 Vaccine Recipient card.

Ndani mnaweka jina la aliyechanjwa, tarehe ya kuchanjwa, Aina ya chanjo na sahihi ya verification officer pamoja na muhuri wa kituo cha chanjo.

At least hata kama kuna kadi za kimataifa zitatoka baadaye, basi itakakuwa rahisi kumfanyia mtu replacement.

Imeisha hiyo.
 
Hivi Tanzania kuna tatizo gani na documents

Vitambulisho vya NIDA,PASSPORT, HATI,VYETI VYA KUZALIWA vyote kuvipata ni msululu

Tunaishukuru serikali ya ccm kwa kuwawezesha hata wahamiaji haramu kumiliki kitamvulisho cha mpigakura
Mkuu yani inasikitisha sana..
Unapata chanjo halafu unawaambia watu eti vyeti bado havijatoka Dodoma..
Nimemuuliza jamaa yangu amechanja Dodoma yeye anasema wameambiwa vyeti vinaandaliwa Wizarani..
Yaani longolongo mtaani hadi ikulu..
Shame.
 
Au wanachanja maji kama Uganda,lakini mbona mi naona hakuna umuhimu wa chanjo kama huna safari ya ughaibuni
 
Mkurugenzi wa elimu kwa umma wizara ya afya Dr Kasangala amesema kwa sasa mkazo umewekwa kwenye kuchanja ili kwenda na muda then watu wote waliochanjwa watapatiwa vyeti vyao kwa utaratibu uliopangwa na watapewa taarifa.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Inagharama gani kuchapisha kijikaratasi
 
Mkurugenzi wa elimu kwa umma wizara ya afya Dr Kasangala amesema kwa sasa mkazo umewekwa kwenye kuchanja ili kwenda na muda then watu wote waliochanjwa watapatiwa vyeti vyao kwa utaratibu uliopangwa na watapewa taarifa.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Certificate zinatengenezwa na madaktari na chanjo inafanywa na madaktari. Tulieni kidogo hii ni bongo.
 
Mkurugenzi wa elimu kwa umma wizara ya afya Dr Kasangala amesema kwa sasa mkazo umewekwa kwenye kuchanja ili kwenda na muda then watu wote waliochanjwa watapatiwa vyeti vyao kwa utaratibu uliopangwa na watapewa taarifa.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Chanjo milioni Moja kwa watu milioni sitini
 
Hivi Tanzania kuna tatizo gani na documents

Vitambulisho vya NIDA,PASSPORT, HATI,VYETI VYA KUZALIWA vyote kuvipata ni msululu

Tunaishukuru serikali ya ccm kwa kuwawezesha hata wahamiaji haramu kumiliki kitamvulisho cha mpigakura
Mimi cheti cha kuzaliwa nilishajisemea sitasumbuka kufuatilia.

Ila sabasaba ya mwaka huu walitoa ofa ya mtu kwenda kujaza taarifa zake kule viwanja vya sabasaba, nilienda na jana nmefuata cheti changu bila usumbufu.

Hapa nasubiri sabasaba ya mwakani nije niende na huko NIDA.

Mambo ya kuzungushana kwenye foleni mwezi mzima sitaki kabisa mimi.
 
Mkurugenzi wa elimu kwa umma wizara ya afya Dr Kasangala amesema kwa sasa mkazo umewekwa kwenye kuchanja ili kwenda na muda then watu wote waliochanjwa watapatiwa vyeti vyao kwa utaratibu uliopangwa na watapewa taarifa.

Source: ITV Malumbano ya Hoja
Hapo ndy watu wanakapopata mwanya wa kupata vyeti bila kuchanja.

Tanzania hovyo kabisa...
 
aiseeee hahahahahah nacheka uku naogopa aisee
Hivi kweli serikali imeshindwa kujiongeza na kutumia mfumo au mtindo wa kusajili vitambulisho vya kupigia kura ambapo mtu upata pale pale...

Yani pale wizarani hakuna mtu wa kutengeneza tamplate na kuweka character zinazo hitajika kwenye vaccine card? yani wameshindwa kufanya kitu rahisi kama hichi tena kadi zinatakiwa kuwa za PVC na za papo kwa papo....yani mtu anachanjwa pale ana kwenda kwa mtu wa mfumo anaingizwa taarifa zake na anapewa kadi papo hapo kama watu wanavyo pata vya kupigia kura.
Hii ni aibu kubwa kwa serikali na nchii na huu ni utoto.
 
Back
Top Bottom