Zanzibar kuwa na wimbo wao wa taifa, bendera, Rais nk, nadhani sio kitu tunachotakiwa kutuumiza kichwa, muhimu ni jinsi gani ya huu Muungano kuuweka ili pande zote angalau ziridhike. Kusiwepo upande unaoona kuwa upande fulani una maslahi zaidi kuliko mwingine. Lakini yote haya yameharibiwa na waliouanzisha, na pia waliotakiwa kuulinda. Yale mambo muhimu yaliyokubalika kwa huu muungano hayafuatwi, ama yameondolewa kinyemela, ama kuna mambo yameongezwa bila kufanya utafiti wa athari zake.
Lakini kubwa ni kutoshirikishwa WANANCHI kuamua Muungano uwe vipi. Viongozi kukaa wenyewe na kupitisha wanavyofikiri/wanavyotaka uwe. Mfano ni pale ulipokuwa unaanza mfumo wa vyama vingi, wakaangalia wakaona yawezekana Bara ikashinda CCM, Zanzibar wakashinda wapizani, na wakati huo Rais wa Zanziba alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, wakaona haitafaa Rais wa Jamhuri ya Muungano atoke CCM, na makamu wake wa kwanza atoke upinzani. Hivyo cheo cha Rais wa Zanziba kuwa makamu wa kwanza wa Rais kikaondolewa.