Tujisahihishe Tz
Platinum Member
- Nov 17, 2011
- 3,061
- 1,367
Mrithi wa Ubunge wa Igunga mh. Dalali Kafumu leo itajulikana ama kusuka au kunyoa. Mpingaji mkuu wa kesi hiyo ni aliyekuwa mgombea wa CDM na kawaailiaha hoja 15 za kupinga ushindi huo
Leo ni leo. Ushindi wa Kashindye kupigwa tena mnada na Dalali? Watu wameshajaa Mahakamani tangu saa 12 asubuhi. Hukumu kuanza kusomwa saa 3 hii. Ni CHADEMA na CCM...
Baada ya hukumu kutolewa Igunga wananchi wa Igunga wameripuka kwa furaha na nderemo na kuzunguka katika viunga vya mji huu huku wakiimba nyimbo za kuipongeza CDM na kumpongeza Magufuri kwa kusaidia ushindi huu.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga amefunguka na kusema kuwa hakuwa na imani na jaji kwa kuwa aliegemea upande wa CHADEMA na matokeo yake ameipa CHADEMA ushindi.
Dk. Kafumu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa yeye siyo mbunge tena na ataendelea na kazi yake ya utafiti wa madini.
Source: EATV