Nadhan jamvi hili ni kwa ajili ya kujadili mambo muhim yatakayoisaidia nchi yetu. Sidhan kama waliobuni, walikua na maana ya kuweka sehemu ya malumbano baina ya vyama. Mtu kuwa na shahada ya Uzamivu kwa wananchi sio tija sana kama maisha yanazidi kuwa magumu. Tusiwe kama kasuku, kwenye hoja tujadili hoja. Kama ahadi zinashindwa kutimizwa tujadili tatizo liko wapi. Kwangu mimi ni bora ya kiongoz ambaye amemaliza form IV tu lakini maisha ya wananchi yanaboreshwa kuliko Prof. ambaye hawasaidii wananchi na anabaki kulalamika tu. Kwa hiyo acheni kutuyeyusha na hoja zenu zisizokuwa na mashiko.