Dr. Hassy Kitine kutangaza nia ya urais Dodoma

Dr. Hassy Kitine kutangaza nia ya urais Dodoma

Marilo

Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
5
Reaction score
3

"Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais ambaye atalitambua hilo na ataichukia rushwa hata ukimuangalia anaonyesha kweli anaiichukia rushwa, sio Rais ambaye anayesema kweli rushwa ni adui wa haki....lakini ukimuangalia usoni unashangaa na kusema.... aaaah kweli huyu?

Ee bwana, kumbuka yaliyotupata; utazame na kuiona aibu yetu. Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni.

Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; mama zetu wamekuwa kama wajane.
Tumekunywa maji yetu kwa fedha; kuni zetu twauziwa

Sasa Mungu amesikia maombi yetu , kama anavyosema Isaya 8:6 nimtume nani wa kwenda kuokoa watu wangu, Isaya akasema nitumie mie hapa, Mungu ametuletea Rais ambaye ni chaguo lake naye Dr. Hassy Kitine, tusifanye makosa,

Nyerere amerudi
.
 
Hapa sasa kama kweli CCM wanamaanisha basi kama si Makongoro huyu mzee anaweza akafaa ila tatizo linabaki je, watampitisha yeye?
 
Huyu si ndiye aliyedanganya kwamba mkewe anaumwa taabani kitandani huko Uingereza? Akapewa kiasi cha Sh 60ml kwa wakati huo, kumbe mkewe ni buheri wa afya tena yuko kwao hakua Uingereza wala wapi..!!!

Leo nae anataka Urais kwa kukemea Rushwa na kuhimiza Uadilifu??? Ama kweli Shetani kaokoka! Hivi ni kwanini wanatuchezea kiasi hiki?

BACK TANGANYIKA
 
Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais ambaye atalitambua hilo na ataichukia rushwa hata ukimuangalia anaonyesha kweli anaiichukia rushwa, sio rais ambaye anayesema kweli rushwa ni adui wa haki lakini ukimuangalia usoni unashangaa na kusema. Kweli huyu?

Ee bwana, kumbuka yaliyotupata; utazame na kuiona aibu yetu.

urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni.

Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; mama zetu wamekuwa kama wajane.

tumekunywa maji yetu kwa fedha; kuni zetu twauziwa

Sasa mungu amesikia maombi yetu , kama anavyosema isaya 8:6 nimtume nani wa kwenda kuokoa watu wangu, Isaya akasema nitumie mie hapa, Mungu ametuletea rais ambaye ni chaguo lake naye ni Dr Hassy Kitine, tusifanye makosa,

Nyerere amerudi.
 
yeye akawe rais wa huko huko kwa kina isaya (galilaya)
 
Huyu Bwana nakumbuka kama vile alipata kascandal fulani enzi za Mkapa ............... Wenye data tukumbusheni!!
 
Huyu ndio HATUFAI hata kidogo.
Alitumia pesa za bajeti ya wizara kumpeleka mkewe matibabu nje ya nchi.
Aende akaendeshe shamba lake hukooo, urais HATUFAI.
 
yeye akawe rais wa huko huko kwa kina isaya (galilaya)

Mijitu mingine bana. Dr.Hassy Kitine ni mtu wa swala tano. Msikiti wake upo karibu na double tree hotel. Kwa kifupi Hassy ni kifupi cha Hassani. Ufinyu wa kufikiri. Ukisikia mtu anaitwa Athumani basi unajua ni mwislamu. Wakati mwingine jina halina uhusiano na imani ya mtu. jinga sana wewe

 
Akawe raisi huko huko kama alikuwa waziri tu akaenda kumtibu mkewe chunusi ulaya je akiwa raisi si ndio tumekwisha
 
Hiyo ilikuwa Zengwe tu! Huwezi watenganisha viongozi na wake zao!!! ... Mbona wanaendelea kuwatibia hadi vimada wao nje?.... Inamaana Nchemba akikupeleka kwenye matibabu India itakuwa Scandal ?
Aligushi matibabu ya mkewe
 
Back
Top Bottom