Kinachofanywa na Kigwangala ni uhuni na unafiki tu, si kweli kwamba anakubali kuwa serikali ya Kikwete si sikivu; na sio kwamba haijali wafanyakazi tu bali na hata wananchi kwa ujumla wao. Rais mwenyewe alishaonyesha kwa mifano jinsi ambavyo wafanyakazi wa nchi hii wasivyo na kipaumbele chochote kwake cha maana, alishaahidi kuwatwanga risasi endapo watamkosesha usingizi, sasa wafanyakazi wategemee nini kutoka kwa watendaji wengine?
Hawa wote ni sawa na nyani, tumbili, ngedele, kima na nguruwe kwenye shamba linaloitwa Tanzania, na wataendelea kuliharibu mpaka pale wenye shamba (waTanzania) watakapoamua kulilinda shamba lao!