Dr Dalali Peter Kafumu alipokea posho ya laki tano na sitini(560000) kwa siku 1 Ktk kashfa ya Jairo

JOB SEEKER

Senior Member
Aug 1, 2011
145
33
Dr. Dalali Peter Kafumu ametajwa miongoni mwa wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini katika kashfa iliyomkumba waziri wa wizara hiyo Mh.ngeleja pamoja na naibu wake.

Katika sakata hilo Dr. Dalali Peter kafumu alipokea kiasi cha sh.560000TSH/= huku Mh.ngeleja Anatuhumiwa kwa kupokea posho ya sh. 4000000 TSH/= na naibu wake sh. 4000000 TSH/=

Je viongozi kama hawa na wengine wengi watawezaje hawana sifa wanastahili kuwajibika kisiasa.

source, Kikao cha bunge kilichofanyika asubuhi ya leo tarehe 19/112011.
 
Lakini yeye kama kamishna wa nishati na madini ile ni posho stahiki kabisa kwa level yake !!!
 
Huo ndiyo ujambazi wa ccm na serikali yake,hilo ni jambo dogo sana yapo mengi makubwa na ya ajabu yanafanyika ndani ya serikali hii legelege ya mheshimiwa Mr "Tabasamu".
 
Tumeyaona mengi mabaya ya ccm na kuyasikia na sasa yatosha yabaki wananchi sasa kufanya uamuzi thabiti
 
Inasikitisha sana. wanagawana kama vile wanahama nchi. Ndo mbunge mpya huyo anaanza kunuka rushwa, hata hajakomaa ubunge bado, akiwa mkubwa atatumeza na sisi. pole ni kwa waliomkosa Kashindye. Huyu ni wa kile chama na kwa ajili ya wale watu.
 
Lissu alifanya vizuri sana kuwataja wale maboya, ila alichonikera hakuwataja wadau wengine zaidi
 
Ila watu wa Igunga huwa hamuitendei haki tz,tukafikiri kua RA ametoka kumbe mumeturushia kombora la pili, ndo maana mkapa alikomaa sana kumbe wanajuana hawa magamba
 
Back
Top Bottom