Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 19,147
- 43,079
Zaidi ya watu 200 wamefariki kufuatia kuporomoka kwa mgodi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwa mujibu wa mamlaka za waasi.
Mgodi huo uliopo katika mji wa Rubaya uliporomoka siku ya Jumatano baada ya mvua kubwa kunyesha, amesema Lumumba Kambere Muyisa, msemaji wa gavana wa waasi wa mkoa wa Kivu Kaskazini, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Wakati huo, idadi kamili ya vifo ilikuwa bado haijulikani.
Wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakichimba coltan madini yanayotumika kutengeneza vifaa vya kielektroniki kama simu janja na kompyuta wakati mgodi huo ulipoporomoka.
Msimamizi wa zamani wa mgodi huo aliiambia BBC kuwa eneo hilo halikutunzwa ipasavyo, jambo lililoongeza uwezekano wa ajali na kufanya juhudi za uokoaji kuwa ngumu pindi ajali zinapotokea. Aliongeza kuwa udongo dhaifu wa eneo hilo ulizidisha hatari.
Wanawake, watoto na wachimbaji wadogo wadogo (artisanal miners) ambao hawajaajiriwa rasmi na kampuni za uchimbaji ni miongoni mwa waliopoteza maisha. Inasemekana takriban manusura 20 wanapatiwa matibabu hospitalini.
Chanzo kimoja ambacho binamu yake alifariki kwenye maporomoko hayo kimeeleza kushtushwa na tukio hilo, kikisema ni “hasara kubwa” kwa familia na jamii.
“Sikuamini angefariki katika mazingira kama haya,” chanzo hicho, ambacho hakikutaka kutajwa jina, kilisema kikiielezea BBC. Kilimuelezea marehemu kama mtu jasiri na mwenye malengo makubwa, ambaye lengo lake kuu lilikuwa kuwatunza mke wake na watoto wawili.
“Sikuamini alikuwa amekufa kwa sababu uchunguzi ulikuwa bado unaendelea. Mwili wake haukupatikana mara moja baada ya ajali, hivyo nilikuwa na matumaini angepatikana akiwa hai. Kwa bahati mbaya, saa kadhaa baadaye, mwili wake uligunduliwa.
Gavana Erasto Bahati Musanga, aliyeteuliwa na waasi wa M23 baada ya kutwaa maeneo makubwa ya Kivu Kaskazini, aliwatembelea manusura wa tukio hilo siku ya Ijumaa.
Rubaya ni miongoni mwa miji kadhaa ya Kivu Kaskazini iliyo chini ya udhibiti wa waasi wa M23, ambao waangalizi wa kimataifa wanasema wanaungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda.
Migodi ya Rubaya inakadiriwa kuwa na asilimia 15 ya coltan yote duniani na nusu ya hifadhi yote ya coltan ya DRC.
Madini hayo yana tantalum, metali inayotumika kutengeneza capacitor za ubora wa juu kwa vifaa mbalimbali vya kielektroniki, jambo linaloyafanya yawe na mahitaji makubwa duniani.
Wakati timu ya BBC ilipotembelea eneo hilo Julai 2025, ilishuhudia wachimbaji wakichimba kwa mikono ili kupata madini hayo ya thamani. Hali katika mgodi huo ni mbaya sana, huku mashimo hatarishi yakionekana kila mahali.
Tangu mwaka 2024, waasi wa M23 wamekuwa wakidhibiti migodi hiyo. Umoja wa Mataifa (UN) umeishtumu kundi hilo kwa kutoza kodi katika sekta ya madini kwa manufaa yao binafsi.
BBC imewasiliana na serikali ya Congo iliyoko Kinshasa kwa maoni, lakini bado haijapata majibu.