DPW deal is not real

Kwamba hii DP WORLD ni geresha tu hapa TZ... ila behind the scene kuna another version of 'richmond' imeshasukwa?

Kwamba shamba la Bibi (Tz) linaenda 'kuvunwa' tena kwa mara nyingine?

-Kaveli-
 
Hili ni zaidi ya ukweli, so saaad...Watu wanataka kuwa wafalme katika nchi ya Jamuhuri...what a loss for our country...Waliopigania uhuru hawakufanya haya leo watu wachache wanataka kutumia mabeberu kutumiliki forever hasa baada ya kuonyeshwa na mzalendo JPM kuwa kuna watanzania ambao wanaweza kuiwezasha nchi kujinufaisha na kuwa miongoni mwa mataifa duniani bila msaada wa mabeberu...

The good thing is, listen and listen careful, niliona ndege yao ikiungua hewani huku wakisambaratika kabisa....Baada ya mtikisiko huu ambao tuombe Mungu usilete madhara kwa raia wema, nchi itaibuka na nguvu zaidi kuliko wakati wowote wa historia yake.

Wasichojua ni kuwa its a decree, Tanzania njema ni MUST PROJECT apende asipende mtu.

Wasalaam!
 
Ni kama saga la reli na kampuni ya Rites kama nimeandika vizuri jina.
Ni kweli. Hii ni ishu ya waswahili wenzetu na makanjanja meupe machache yamepanga dili. Na hapa jiulize,
- DP WORLD atake hadi bandari za maziwa?!! Za nini...

- DP World anataka hadi aendeshe reli /SGR?? Ya nini...

- Na ukiwatafuta wahusika wa upande wa pili yani DUBEI/UAE, hawaeleweki kwenye makaratasi ya IGA. Kwa nini wajifiche kama ni genuine?!

Hawa ni janjajanja mzungu wa reli wameungana, lengo kukamata misuli yote ya uwekezaji.

Wanataka reli, EPZ na Bandari kavu zote, ili malori yao ya mizigo wajue yana operate vipi.

Wanataka pia ku control usafirishaji wote ili madini na maliasili zingine kama magogo na vitu vya magendo, deal chafu, vitembee bila kuulizwa.

Hii ni deal chafu.
 
Kwamba hii DP WORLD ni geresha tu hapa TZ... ila behind the scene kuna another version of 'richmond' imeshasukwa?

Kwamba shamba la Bibi (Tz) linaenda 'kuvunwa' tena kwa mara nyingine?

-Kaveli-
Ni kweli kabisa - Kaveli-

Ni "dili" chafu hii. Watu wanajiwahi wa take control of every investment opportunities in the future.

Wameungana wenye malori na ma tanker, wana hofu, je SGR itaua ulaji wao.
Ndio maana wanataka mpaka 'transport corridors, na ICDs/bandari kavu'.

Hakuna DP World hapa, ni wenzetu wanataka kula na vizazi vyao miaka 200 ijayo.
 
Niwakati muafaka sasa watanzania kusema inatosha huu ndio muda sahihi wa kumkemea pepo mpaka akimbie

Hii siyo bule iri giza liliropo huu siowakati wake kwa sasa nchi inahitaji Nuru kuliko wakati wowote ule

kinacho takiwa hapa nikumtupa jongoo na mti wake hiyo ndio itakuwa tiba ya huu ugonjwa
 
Roma na Stamina
 
We ni msomi hebu usijivue nguo hivi ..
Huwezi hata Ku Google.. Dpworld??
Ndio ukweli wenyewe , ndio Yale Yale ya Richmond ya Kariakoo
Mleta uzi huu ndio ukweli wenyewe. Hawa akina The Boss ndio wafaidika wa hii kampuni. Kila mara huwa nasema hapa, bila machafuko hii nchi itaendelea kuchezewa tukiwa tunaona. Hii kampuni ya DP World inatumika na watawala wetu ili kujimilikisha bandari zetu. Na kwa bahati mbaya hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni ama hawajitambui, ama viongozi wao watakuwa sehemu ya ufaidika wa wizi huu.
 
We ni msomi hebu usijivue nguo hivi ..
Huwezi hata Ku Google.. Dpworld??
Umekuwa mpole kwasababu unajua fika huyu mleta uzi kaongea ukweli ambao unadhani watu hawajui, na hamtaki watu waujue. Wajinga wamekwisha nchi hii, sana sana wamebaki waoga. Ni juu ya vyombo vya dola kuamua kusimamia maslahi ya umma, na sio kusimamia matakwa ya viongozi wezi.
 
Hilo la ndege ndio hasa litaenda kutokea iwapo tuna wazalendo wa kweli ndani ya nchi hii. Na hilo likitokea inatakiwa iwe mwanzo wa mabadiliko ya kweli ya mifumo ndani ya nchi hii. Kwa post hii umesema kweli, umekosea hapo tu kumtaja huyo JPM, yeye alikuwa ni sehemu ya kuharibu checks and balances za mifumo nchi hii. Leo hii akina Rostam wanajua tuna mifumo dhaifu hivyo wanafanya watakavyo. Hiyo DP imesomewa ramani na Rostam baada ya kujua udhaifu wa kiutawala ndani ya nchi hii.
 
Baada ya kusoma mara kadhaa na kuelewa, comment yangu ya kwanza niliyoitoa ilikuwa kwamba Rais na Waziri waliwekwa kwenye poisoned room kwa ajili ya majadiliano au walipewa kahawa ilokuwa na sumu ya kufifisha uwezo wao wa akili huku wenzao wa upande wa pili wakiwa na protectives. Sikuelewa kwa nini waliweza kusaini mkataba huu ambao ni one sided.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi najiuliza tu. Je, kuna mkono wa Rwanda katika hili? Tunaambiwa bandari kavu kubwa iko Rwanda, na ilijengwa kabla ya kupata bandari ya ziwani wala ya baharini. Malisho makubwa ya Rwanda yako Congo. Maruweruwe!
 
Tunauzwa mchana kweupe.
Na bei yetu hata haieleweki
 
Wewe ndio uko uchi kabisaaaa kwenye hili tena umetapanya miguu kuanika nyeti nje ..
Huyu sio BOSS ninaemfahamu mimi humu siku zote!! Kama ndiye yeye ninayemfahamu basi kuna kitu kafanyiwa na kimembadilisha amekuwa hamnazo na sio mzalendo tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…