DPP funua faili la mtoto aliyelawitiwa na Hakimu kupindisha haki ili Mh Rais ampe zawadi huyo Hakimu

Wanajamvi natumah mu wazima?

Nianze kwa kuwapa hongera watanzania kwa kila hali tuliyonayo,kwa kila maisha tunayoyaishi.

Kabla ya kuingia kwenye kiini cha mada yangu ndugu zangu niwajuze tu kuwa nchini Tanzania suala zima la ushirikina, na mauji yanayohusu imani hizo bado viko vingi sana.

Niende kwenye mada sasa,nitajitaidi kuelezea kwa jinsi nilivyokutana na ilo Faili na kujua liko kwa Dpp kwa sasa.

Mwaka 2018 mwanzoni kabisa nilifanikiwa kufika mkoani Morogoro kwa shughuli fulani ya kiserikali.

Nikiwa mkoani Morogoro nilifanikiwa kufika, eneo moja linaitwa Mang'ula ambapo ni Kata tu,nikiwa nimekaa akaja mama mmoja na sura ya huzuni sana, kwa ufupi hakujileta pale mimi ndio nilifanya kumuita kwa shughuli zilizokuwa zimenipeleka nae alikuwa miongoni mwa watu ambao nilitakiwa kuonana nao.

Basi baada ya kumuita nilimueleza kilichopelekea nikamuita nae alikubaliana na mimi na kuitikia wito na kufanya kile nilimwelekeza kwa kweli alifanya kile nilichotaka afanye nikampangia siku nyingine aje tena hapo kuna kitu kingine kilitakiwa kufanyika.

Nilivyomwambia aje siku nyingine nilishangaa yule mama anabubujikwa na machozi,nikamuuliza kwanini unalia?Akaniuliza hivi wewe kijana wangu si ndo umenipangia nije ofisini kwenu kule Dar kwa DPP?

Alivyotamka hivyo ikabdi mimi nimshike mkono na kutoka nae nje,hapo mgongoni alikuwa na mtoto wa miaka kama 6 hivi, ila hatembei na kinyesi kinamtoka muda wote

Nilipotoka nae nje,cha kwanza nilimwambia mimi sijatoka ofisi ya DPP na wala sijawai fanya kazi hapo, ila nikamwambia ninaweza msaidia kama kuna kitu kiko kwa DPP basi kwa kuwa ofisi naijua na nina wadau pale inawezekana kabisa.

Ndipo alipokubali na kuanza kunisimulia kwa kusema yafatayo,

Mwanangu,huyu mdogo wako unayemuona aliingiliwa Kinyume na maumbile na vijana ambao ni majirani zangu,kwa maelekezo ya mganga kuwa wakifanya hivyo watapata fedha,baada ya kumuingilia mwanangu tangu alipofanyiwa unyama huo hajawahi kukaa chini tena,na kinyesi kinamtoka muda wote

Baada ya mwanangu kuingiliwa,nilifungua kesi mahakama ya mwanzo, hapa hapa Mang'ula lakini huwezi amini washtakiwa ambao ni jirani zangu walipewa ushindi,mimi nikaamua kukata RUFAA kwenda mahakama ya Wilaya IFAKARA hapo ndipo nilipozidi kupoteza haki zangu kwa washtakiwa ambao niliwashitaki na ushahidi uko wazi,Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ifakara kwa jina moja la Liyoni nilikuwa nikimuona hapa kwetu na wahalifu mara nyingi sana.

Pamoja na kumuona wahalifu walimpa ongo Mh Hakimu ya mashamba ekari 50.Ninazijua,huwezi amini hakimu alielekeza mwangu akapimwe ili kupata ushahidi kama kweli aliingiliwa na majibu yakaja yanasema aliingiliwa lakini Hakimu aliwapa Ushindi hao vijana ambao ninaishi nao hapo mtaani.

Baada ya hapo hukumu kutoka mimi nimeenda mpaka Mahakama Kuu,ila naambiwa jambo liko kwa DPP na kila nikienda Mahakama Kuu huyo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya alikuwa akinipigia simu za vitisho na kweli nikifika Mahakama Kuu yale ambayo alikuwa akiniambia basi nakutana nayo kweli Mahakamani sasa suala hili nimelipeka mwenyewe pia kwa DPP Ila nako huyu bwana ameishaweka zuio sina pa kukanyaga ila ameweka zuio wakati nilishafungua faili liko huko.

Waliotenda ili kosa ninawajua sana na Hakimu mwenyewe anajua kabisa kuwa alikosea sana hakutenda haki.

MWISHO WA SIMULIZI,YAFATAYO NILIYAFANYA.

Baada ya yule Mama kumaliza kunisimilia ilo tukio cha kwanza kabisa nilitaka nijidhiilishie kama ni kweli.

Nilienda mpaka Ifakara, nikamuona Mh Hakimu kwa jina la Liyoni na kumuhoji kama kweli shauri ilo liko mezani kwake. Alinijibu kwa wasi wasi sana na mshutuko wa hali ya juu.

Alijibu kuwa ni kweli yeye ndiye aliyeamua shauri ilo,nikamuuliza je wajua kuwa huyu mama anaenda Ikulu kumuona Mh Rais kwa kukosa haki yake?

Yule Hakimu gafla alinyanyuka na kushika kiuno kwa mshangao,huku akionesha wasi wasi wa hali ya juu sana.

Baada kuzungumza nae kwa takribani dakika mbili niligundua kuwa kweli huyu bwana amefanya kosa kubwa la kumnyima haki huyu mama.

Baada ya hapo nilimtafuta mbunge wa Kilombero na kumwelezea jambo ilo ndipo huyo mbunge akawa amekubali kuwa atalifanyia kazi.

Baada ya hapo nikamtafuta Hakimu ambaye nae alihudumu kwenye mahakama ile ile kwa jina la Mashauri nikajaribu kumdodosya kama ili jambo nae aliliona nae alikili kulijua kabisa.

Na kunipa habari nyingi sana baadae nikamfuata yule mama na kumwelezea jinsi ambavyo anaweza ruka hivyo vizuio vya huyo Hakimu.

Bahati mbaya sana nilipoanza kulifuatilia suala ili nilipata uamisho na kuelekezwa nikafanye vijikazi vyangu wilaya nyingine.

Ninakumbuka nilibeba no ya simu ya yule mama ila bahati mbaya ilipotea na mpaka ninavyoandika nina imani huyo mama faili lake liko kwa DPP kwani na Mahakimu hawa nadhani watakuwa wameamishwa.

Mwisho mwana jf je huko tuliko hatuna hawa watu?
Daa, Asee mpaka mwili umesisimka.
Mkuu beba jukumu la kumsadia huyo mama kwa roho moja.
Tanzania hii kuna watu wangapi wa aina hiyo wanaopoteza haki zao kwa tamaa za watumishi wa uma?
 
Hii kesi ni ya yule mama aliyeenda mbele ya rais au ni nyingine?
... maana ulivyoandika kwamba ulielezwa na huyo mama haviendani na vile alivyosema mbele ya rais!
... mbele ya rais alisema mwanae alilawitiwa na mtu mwenye umri wa miaka 53, wewe unasema mama alisema mwanae alilawitiwa vijana majirani!
Nje ya mada
 
Daa, Asee mpaka mwili umesisimka.
Mkuu beba jukumu la kumsadia huyo mama kwa roho moja.
Tanzania hii kuna watu wangapi wa aina hiyo wanaopoteza haki zao kwa tamaa za watumishi wa uma?
Pole kwa kusisimukwa na mwili wako,niombe radhi kwani wako ambao wakisisimkwa mwili hali ya afya zao ubadilika na kuathilika badala ya kuimalika.
 
Mahakama kuu alienda kumshtaki hakimu na si rufaa.
Elezeeni mkijuacho kwa lengo la kujenga na sio kebei pata picha ungelawitiwa wewe mpaka muda wte ukawa unatoa kinyesi ungejiskiaje?au hata mwanao?jenga hoja tumsaidie niliyemfikisha hapo.
 
Kisa chako kinasikitisha lakini kina chumvi nyingi. Huyo mama alipata wapi mamlaka ya kufungua kesi ya jinai ikasikilizwa kwenye mahakama mbili na kushindwa?

hapo katikati inaonekana alitoka Mahakama ya Wilaya akaenda Mahakama Mkuu bila kupitia Mahakama ya Hakimu Makazi. Bila shaka na Mahakama Kuu angeshindwa kwa kutokufuata utaratibu.

Wewe unaonekana kuwa na elimu ya sheria kwa nini hukufuatilia shauri husika kwa waendesha mashtaka waliopo wilayani.

Je kama wahusika si hao vijana ila mtu mwingine ulitaka watiwe hatiani bila makosa?
Mkuu sina uelewa dhidi ya sheria mie ni mkulima wa mwanalumango mkuu wangu
Nisadie nondo za kisheria mkuu.
 
Back
Top Bottom