DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mwanza. Mahakama ya Wilaya ya Ilemela imewaachia huru watuhumiwa 57 wa kesi ya uhaini waliokuwa wakishikiliwa tangu Oktoba 29, 2025 kufuatia matukio ya vurugu za baada ya uchaguzi.
Uamuzi wa kufuta mashtaka hayo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Stella Kiama, katika Mahakama ya Wilaya ya Ilemela iliyopo kwenye Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, Buswelu.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya upande wa mashtaka, kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Safi Amani, kuwasilisha ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) la kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya watuhumiwa hao 57 kati ya 61 waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali.
Shauri hilo namba 26641/2025 limeletwa kwa ajili ya kutajwa kwa mara ya pili mahakamani hapo leo Jumatatu Novemba 24, 2025, ambapo kwa mara ya kwanza lilitajwa Novemba 24, mwaka huu.
Pia Soma: Washitakiwa 114 wafunguliwa kesi ya uhaini Mwanza, kufuatia maandamano Jumla yafikia 320 nchi nzima